NA AMRAT KOMBO, ZANZIBAR@@@@
UONGOZI ni haki ya kila mtu, awe mwanaume au
mwanamke.
Tena hapa tunajifunza kuwa, hata kundi la watoto wa kike ama wakiume,
wanaweza kuwa viongozi kwa aina yao na sehemu waliyo ndani ya jamii yao.
Jamii imeshazowea kuona mwanaume ndio anaeweza kuwa kiongozi
na kusimamia nchi katika hali zote, kuliko wanawake na hii kutokana na mitazamo
yao isijengwa kimamtiki.
Ingawa mtazamo huu, unaweza ukaondoka kwasababu mwanamke
ameweza kuongoza familia na kuweza
kusimama imara, kwahivyo
hatoshindwa kuisimamia nchi nzima.
Mfano hai na wa kweli kwa sasa ndani ya taifa la Tanzania,
rais anayewaongoza wananchi wastani wa milioni 60 ni Dk. Samia Suluhu Hassan
(mwanamke), na kila mmoja ni shahidi hajatetereka kwenye nafasi hiyo.
Tena anasimamia vyema familia yake, pamoja na wananchi wake na
kutatua changamoto mbalimbali zinazotokea katika nchi na mengi yameongelewa
kuhusu yeye bali hakukata tamaa.
KWA NINI WANAWAKE HAWAONEKANA KWENYE SIASA?
Asiata Said Abdallah ambae ni mueka hazina wa Kanda ya Unguja
katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, anasema amejiunga katika siasa mwaka 1994
katika chama hicho na kugombea katika
nafasi ya vijana na hakubahatika kuipata.
"Nilipojiunga katika chama, nikaona nigombanie katika
upande wa vijana, mkoa wa Kilimanjaro ila sikubahatika kupata, na sikukata
tamaa nikaendelea kugombania tena mwaka mwingine pia sikubahatika kupata,"
anasema.
Anataja moja ya vikwazo vilivyopelekea
kushindwa kwanza ni elimu ya kutosha kuhusiana na siasa, kutokuwa na mahusiano
na vijana wengine pamoja na kutokuwa na uwezo wa kuwashawishi vijana.
"Mume wangu wa mwanzo alikuwa hapendi nijihusishe kwenye
siasa, na baada ya muda ndoa kuvunjika, nilindeleza ndoto zangu na nikabahatika
mume mwengine nashukuru ananipa nguvu katika kushiriki siasa,"anaeleza.
Anaona kwenye sisa zipo fursa mbali mbali, iwapo wanawake
watatuliza akili zao, ikiwemo kujenga uhusiano na wananchi pamoja na kujipima
kiuongozi kwa kule kugombea na wanaume mbali mbali.
" Miaka ya nyuma ilikuwa tunaona mwanamke wa kiislamu
hawezi kusimama katika jamii kutokana na imani yetu, lakini sasa hivi viongozi
wa dini nao wanatuelimisha,"anafafanua.
Sababu iliyopelekea kuingia kwenye siasa ni kurithi nyayo za mama yake kwasababu yeye ni mwasisi wa chama cha chadema maulidah Anna komu
Aidha alisema miongoni mwa sambabu zinazopelekea wanawake kuwa
kidogo katika siasa ikiwemo kutojiamini, woga, kutokuwa na moyo wa ujasiri,
ambapo haya yalishajiengwa na wanaume tokea asili.
Mgeni Ali Haji ambae amegombae nafsi ya uwakilishi wa viti
maalumu nafasi za wasomi katika chama cha Mapinduzi CCM mwaka 2020, na
kutobahatika kupata na kuelezezea sababu mbalimbali zilizopelekea kutopata
fursa hiyo.
"Sababu
iliyonifanya nikose kubwa ni kukosa matayarisho yangu binafsi,
ikiwemo wapiga kura kutonielewa kwa undani pamoja na kukosa uwezo wa kufanya
kampeni,’’anaeleza.
Lakini anaona wapiga kura wakati mwengine hawataki kubadili
mgombea mwingina hata kama yule waliyenae hawajatekeleza ahadi zao ambazo
aliwatangaazia wakati wa kampeni.
Sambamba na hayo
alisema sababu nyengine kura hazikutosha
kushinda nafasi hiyo na kubahatkika kupata kura 36 na mwezangu alipata kura
zaidi ya 100.
Aidha alisema hatua
mbalimbali amechukua baada ya kushindwa, kuingia katika siasa ikiwemo kuzidi
kujifunza katika masuala ya uongozi na kushiriki katika mambo ya kijamii.
"Kwavile jamii ndiyo husika katika uongozi, ndiyo
wanaweza kukufahamu kwahiyo nimeona nifanye hivyo pia kuongeza elimu nalo
kiupande changu ni jambo muhimu sana,’’anasema.
Licha ya yote hayo aliyopitia mpango wake wa badae, ni kuja
kugombania tena uongozi na kupata matumaini ya kuja kushinda
kwasababu ameshapata taaluma ya uwongozi.
Anaona kuwa, wanawake wanaopate fursa ya kugombea ni lazima
wapewe elimu ya kutosha, kwanza kuyajua mazingira ya siasa, pili kuelimishwa
kuwa unapoomba unaweza kupata au kukosa, ambapo ni sawa na
asiyeomba ana hakika ya kukosa.
‘’Wapo wanawake wanadhani kama vile hawana haki ya kugombea,
na wanaona kuna familia ama watu maaluma ndio wenye haki ya kugombea, jambo
ambalo sio sahihi,’’anasema.
"Nasaha zangu kwa wanawake wanzangu waliopo
madarakani wawashajiishe wanawake
wengine, ili nao waweze kugombania na kuondoa hofu, na waendelee kufanya vizuri
katika majukumu yao kwasababu itawasaidia
kuwepo kwa wigo kwa wanawake
wegine,’’anasema.
"Wanawake tukiwa wengi katika uongozi tutapata fursa ya
kutoa mawazo na ushauri kuhusiana na maswali yanayowahusu wanawake na watoto na
jamii kwa ujumla kina mama ni lazima tubadilike uongozi ni tunu gombea uongozi
uwe mtetezi wa wanawake wengine,’’anaeleza.
Mwakilishi wa Jimbo la Konde Pemba, Zawadi Amour Nassor, anasema ametumia njia mbalimbali ya kuweza kutatua vikwanzo ambavyo amepitia kwa lengo la kuwa kiongozi.
"Kwanza sikukata tamaa, wakati nilipokuwa nagombania,
maana kwa vile nilishawafuata walionitangulia, waliniambia ambayo
yanawezakujitokeza katika safari yangu ya siasa,’’anasema.
Profesa Issa Haji Zidi, alifafanua kuwa dini ya kuislamu
haijakataza kuwepo kwa kiongozi mwanamke isipokuwa mwanamke anatakiwa kufata
taratibu na sheria za kiislamu.
Anaeleza kuwa katika enzi za Mtume Muhammad (S.A.W ) mwanamke
alikuwa kiongozi katika vita na mambo mengine tofauti na kote aliweza
kufanikisha.
"Mwanamke wa mwanzo aliyeshika na kukubaliwa wadhifa wa
ushauri kwa Mtume (SAW) alikuwa mama yetu mkubwa, Sayyidatuna
Khadija binti Khuwayld (RA), ambaye alikuwa mshauri wake mkuu,’’anafafanua.
Hapa Mratibu wa kuinua wanawake katika uongozi kutoka chama
cha wandishi wa habari wanawake Tanzania
(TAMWA
Zanzibar), Mariyam Ame, anasema wanatoa elimu mbalimbali, kwa wanawake ambao
wanahitaji kuwa kiongozi, ili wajitambua na kutatua changamoto za kiuongozi.
"Nahii inawapa hamasa na kuweza kutambua haki zao za
kidemokrasia, ikiwemo haki ya kupata elimu afya pamoja na
miundombinu .
Maryam anasema hadi sasa zaidi ya wanawake 172 wamepatiwa
mafunzo ya uwongozi kutoka Unguja na Pemba, pamoja na kutambua vikwazo na namna
ya kukabiliana navyo.
Aidha aliwanasihi wanawake wanaotaka kuingia kwenye uongozi
kutokuwa na hofu, kama Katiba inavyosema katika serikali zote mbili
inavyoelezea pamoja na mikataba mbalimbali ya kitaifa na kikanda pamoja na kuwa
karibu na chama chake.
MWISH0
Comments
Post a Comment