NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
WANAWAKE wanaolima na kilimo cha mwani cha kina
kirefu, wa kijiji cha Tundaua shehia ya Kilindi wilaya ya Chake chake Pemba, wamesema
baada ya kumalizika kwa mafunzo ya siku 15, sasa wanajiamini kuogelea, hadi
urefu wa uwanja wa mpira wa miguu bila ya kupumzika.
Walisema, mafunzo hayo, yamewajengea uthubutu
wa kuogelea na hata kuokoana, pindi ikitokezea ajali wakati wa kwenda ama
kurudi kwenye shughuli yao ya kilimo cha mwani, kwenye maji yenye kina kirefu.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi,
kwenye bahari ya Tundaua walikokuwa wakifundishwa, walisema kwa sasa wamejitoa
woga na wanajiamini kogelea hadi mita 100 (urefu wa uwanja wa mpira wa miguu), bila
ya kumpunzika.
Walieleza kuwa, wazo lililoibuliwa na Ofisi
ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar kipitia Idara ya Mazingira chini ya mradi
wa ‘SAPPHIRE’ umekuja kuwapa uhakika wa kazi zao.
Mmoja kati ya wanufaika wa mafunzo hayo
ambae ni mkulima wa mwani wa kina kirefu, Hassina Seif Baki, alisema hakuwa na
ndoto katika maisha yake, kwamba siku moja engeweza kujua kuogelea.
‘’Pamoja na kwamba mafunzo haya
yatanisaidia wakati wa kuendesha shuguli zangu za kilimo cha mwani maji
makubwa, lakini kujua kuogelea itanisiaida hata kuokoa wenzangu,’’alieleza.
Nae Raya Abdalla Rashid, alisema pamoja
kwamba alikuwa akiendesha shughuli mbali mbali zinazohusiana na habari, lakini
hakua anajua namna ya kuogelea.
Alieleza kuwa, kwa sasa anauwezo kwenda nusu
na robo ya masafa ya uwanja wa mpira wa miguu bila ya kuchoka, jambo ambalo
hapo kabla hakuwaliza katika maisha yake.
Nae mnuafika wa mafunzo hayo Fatma Suleiman
Sinei, alisema kilichobakia kwa sasa, ni kupatiwa vifaa maalum kama vile viatu na
nguo maalum za kuogelea, ili kupata urahisi wa shughuli zao.
Mwalimu wa mafunzo hayo Kaije Said Bakari,
alisema wanawake hao awali walikuwa na woga na wasi wasi mkubwa wa hata kuingia
baharini, ingawa baada ya mafunzo hayo, sasa wako vizuri.
‘’Nimeshahitimisha wanawake 45 ambao wameshapata
mafunzo ya siku 15, baada ya kumaliza mafunzo kama hayo kisiwa cha Fundo,’’alieleza.
Hata hivyo mwalimu huyo, alisema suala la
kugoelea haliwahusu wakulima wa mwani pekee, bali kila mtu anayeishi katika
mzungumko wa visiwa.
Mapema Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mazingira
kutoka Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Alawi Haji Hija, aliwataka
wanufaika wa mafunzo hayo, kuhakikisha wanawapa na wenzao.
‘’Lengo la serikali, ni kuona mafunzo hayo
yanawafikia wanawake wote wanaojishughulisha na kilimo cha mwani, kiwe cha maji
kidogo au wale wa kina kirefu,’’alieleza.
Aidha aliwaeleza kuwa, huo ni mwanzo mzuri
kwa wakulima hao, na hasa vile suala la kupatiwa vifaa na zana za kilimo cha
mwani, utaratibu wa wizara husika unaendelea.
Katika hatua nyingine, Kaimu huyo wa Idara
ya Mazingira Zanzibar, alimpongeza mwalimu huyo kwa ujasiri wake, wa kuacha
familia zake na kuwafundisha wanawake wenzake, jinsi ya kuogelea.
Alieleza kuwa, mradi huu kwa sasa
unatekelezwa zaidi kisiwani Pemba, katika ukanda wa mkondo wa Pemba PECA,
ambapo maeneo hayo yameshaathiriwa, na kukosekana kwa mapato kwa wakulima wa
mwani wanaolima maji kidogo.
Mratibu wa mradi huo Aisha Abdalla Rashid,
alisema wakulima walikuwa wakilima mwani katika maji madogo, na yanapotoka
huathiriwa na pia kuwa na mavuno kidogo.
‘’Kwa changamoto hiyo, ndio Idara ya
Mazingira ilipotafuta mradi maalum, ili kulima eneo dogo lenye mavuno makubwa,
na hasa baada ya kukamilisha mafunzo ya kuogelea,’’alieleza.
Hata hivyo Mratibu huyo, alimpongeza
mfukufunzi wa mafunzo hayo, kwa kuongeza idadi ya wanawake waliopatiwa mafunzo hayo,
kutoka 40 hadi 45, katika shehia za Fundo na Kilindi kisiwani Pemba.
Mwisho
Comments
Post a Comment