NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
WAANIKAKAJI dagaa wa shehia ya Ndagoni
wilaya ya Chake chake Pemba, wameshauriwa kuzitumia njia nzuri za uanikaji,
ikiwemo kutumia chanja za miti zilizoinuka ‘chanja’ ili kuepusha vumbi na taka taka,
zinzoweza kupunguza thamani ya bidhaa hiyo.
Walielezwa kuwa, njia nyingine ambayo ni
nzuri kwa uanikaji na kutumia sakafu iliyasafi, ambayo ni vyema ikazungumshiwa
kinga maalum, ambayo itazuia taka taka na wanyama kuliharibu wakati wa uanikaji.
Hayo yamelezwa na Kaimu Afisa Mkuu Idara ya
Maendeleo ya Uvuvi na Mazao ya Baharini Pemba Mayasa Hamad Ali, wakati akitoa
mada njia ya uanikaji bora dagaa, kwa waanikaji na wavuvi wa shehia ya Ndagoni,
mafunzo yaliyofanyika ukumbi wa Manispaa ya Chake chake.
Alisema, njia nyingine ambayo waanikaji
wanapaswa kuitumia ni kutumia wavu, ambao kitaratibu hutakiwa kuwekwa juu juu,
ili kuhakikisha dagaa haliingii wadudu na taka taka.
Alieleza kuwa, njia hizo pamoja na ile ya
kutumia moshi kwa magamba ya miti maalum, ndio ambazo zinasaidia kulitia
thamani dagaa, wakati linapopelekwa kwa wateja.
‘’Niwaombe sana kuwa, kwa wale ambao watatumia
chanja, ni vyema zikawa za miti, na sio zile za vyuma kwani zikipata unyevu
hutoa maji maji ‘kutu’ ambazo ni hatari kwa walaji,’’alieleza.
Katika hatua nyingine, Kaimu Afisa huyo
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi na Mazao ya Baharini Pemba, Mayasa Hamad
Ali aliwataka wavuvi wa dagaa, kujenga utamaduni wa usafi kuanzia nguo na
vyombo vyao.
Alieleza kuwa, vyombo kama ndoo wanazobebea
dagaa wahakikishe, wazisafishe kila siku, kabla ya kuingiza dagaa jingine,
wakifanya hivyo wataepusha uoza wa dagaa lao usiokuwa wa lazima.
‘’Wavuvi waliowengi, wamekuwa hawazingatii
usafi, jambo hili husababisha dagaa kupata unyevu unyevu na kupelekewa kuzaliwa
minyoo, yanayoharikisha uozaji wa dagaa,’’alifafanua.
Akifungua mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi
Idara ya Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa rais Zanzibar Alawi Haji
Hija, alisema mafunzo hayo ni maalum kwa waandikaji dagaa, ili kuongeza mnyororo
wa thamani, wa kazi yao.
Alieleza kuwa, waanika dagaa wamekuwa wakikumbwa
na changamoto za kutokuwa na thamani ya dagaa lao, jambo lililokuwa, likishusha
thamani ya bidhaa zao.
‘’Mafunzo haya ni maalum, kwa ajili ya
kuchapuza mnyororo wa thamani, maana sasa serikali kuu inatekeleza kwa vitendo,
dhana ya uchumi wa buluu, hivyo haya ni sehemu ya kukuza soko,’’alifafanua.
Katika hatua nyingine, alieleza kuwa
waanika dagaa hao, kisha watatakiwa kuwafikishia wenzao elimu hiyo, ili iwafikie
wengi zaidi kwa mujibu wa mahitaji yao.
‘’Na mafunzo haya zaidi yamewalenga waanika
dagaa kutoka shehia ya Ndagoni, kwani ndio ambao wanakusanya idadi kubwa ya
waanika dagaa hao na wavuvi kuliko eneo jingine,''alieleza.
Alifafanua kuwa, mafunzo hayo yatawasaidia
kujua mazingira rafiki ya uanikaji dagaa, ili kuepusha taka taka na mavumbi, yanayosababisha
kupungua thamani ya dagaa lao.
Hata hivyo alisema, serikali bado inaendelea
kuthamini kwa vitendo wavuvi na waanika dagaa, kwani inayodhamira ya kuongeza thamani
na pato kwa wananchi, walioekeza kwenye sekta hiyo.
Akiwasilisha kazi za vikundi, muanika dagaa
kutoka shehia ya Ndagoni Hakim Hamad Mmanga, alisema changamoto kubwa
inayowakabili, ni ukosefu wa vifaa rasmi vya kuanikkia.
‘’Nyingine alisema ni ndege kama Kunguru na
wingine wamekuwa wakiharibu dagaa lao, wakati wanapolianika na kusababisha
kuingia taka taka,’’alieleza.
Kwa upande wake mshiriki Abdull-hakim Salim
Ali wamekuwa wakitumia njia tatu kuu za ukaushaji dagaam ikiwemo kuanika kwa
jua, kaunika kwa jua baada ya kuchemshwa na kutumia moshi.
‘’Njia hii ya kukausha kwa moshi, kwanza dagaa
hukoshwa, hitiwa viungo kama chumvi, pili pili na kisha kuingizwa kwenye mtambo
maalum,’’alifafanua.
Mafunzo hayo ya siku moja, ni muendelezo wa
juhudi za serikali katika kuangalia njia bora za kukuza pato la wavuvi na hasa wa
sekta ya uanikaji wa dagaa na wavuvi wao.
Mwisho
Comments
Post a Comment