NA
HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
WAZAZI
na walezi wenye watoto wao skuli ya sekondari ya Connecting Continent ya Mgogoni
wilaya ya Chake chake, wamesema wameridhishwa na juhudi binafsi za waalimu,
katika kuwafundisha wanafunzi skulini hapo.
Wakizungumza kwenye mkutano maalum uliofanyika skulini
hapo, wenye lengo la kupokea matokeo ya muhula wa kwanza, wazazi na walezi hao,
walisema kutokana na ugumu wa wanafunzi ulivyo, wanaridhishwa na juhudi zao.
Walisema, wengi wao wamekuwa wakikosa muda wa kuwauliza
watoto wao juu ya maendeleo ya elimu, lakini waalimu hao, wamekuwa wakibuni
mbinu za kuwaendeleza wanafunzi.
Wazazi hao walieleza kuwa, kwa muhula huu kwanza,
wameridhishwa na matokeo hayo, ambayo kwa yale ya darasa la 12, kama yengekuwa
ndio ya mitihani ya taifa, kusingekuwa na mwanafunzi aliyefeli.
Mmoja kati ya wazazi hao Omar Mjaka Ali, alisema kama sio
juhudi za waalimu hao na mbinu mbali mbali za kuwalazimisha wanafunzi kusoma,
matokeo ya muhula wa kwanza, yasingekuwa mazuri.
‘’Mimi niseme kuwa, jinsi wanafunzi walivyojiingiza kwenye
harakati mbali mbali kama michezo isiyowahusu, leo hii tusingekuwa na matokeo
mazuri kama haya,’’alieleza.
Mzazi Ali Yussuf Ali, alisema matokeo hayo ya muhula wa
kwanza, yanaashiria kuwa, waalimu wanafundisha kwa bidii na ukomavu wa hali ya
juu.
Nae mzazi Hidaya Mjaka Ali, alisema kama waalimu
wanaendelea kufanya juhudi hizo, sasa ni jukumu lao wazazi kufuatilia nyenendo
za watoto wao.
‘’Waalimu wanaendelea kuonesha juhudi zao, sasa na sisi
wazazi na walezi, tuwasaidie waalimu, maana mtoto analelewa na nguzo zaidi ya
moja,’’alishauri.
Kwa upande wake mazazi Mgeni Seif Mohamed, alisema pamoja
na mazuri yaliojitokeza kwenye muhula wa kwanza, lakini lazima mkazo uwekwe kwa
masomo ambayo hajakupasisha vizuri.
‘’Masomo ya fizikia na hesbati, lazima waalimu kwa
kushirikiana na sisi wazazi, tuangalie namna bora ya kubuni mbinu nyingine, ili
sasa mwakani ufaulu uongezeke,’’alishauri.
Hata hivyo mzazi Rashid Mjaka Mkuu, amependekeza wanafunzi
kuongezewa kazi za kufanya, hasa kwa masomo ya yanyoambatana na hesabu, kwani ndio
msingi wa masomo kadhaa.
Mwalimu mkuu wa skuli hiyo Mwache Juma Abdalla, alisema
wazazi, wataendelea kuwa mwalimu nambari mbili, katika kufikia ndoto za
mwanafunzi.
Alieleza kuwa, mwalimu pekee hata kama anaujuzi na uwelewa
kiasi gani, kama mzazi hakushughulika kwa nafasi yake, ufaulu wa mwanafunzi
utakuwa mashakani.
‘’Ingawa niwapongeze baadhi ya wazazi na walezi, wamekuwa
wakifuatilia kwa karibu maendeleo ya watoto wao, na njia hii sisi inatupa ari
zaidi ya kufundisha,’’alieleza.
Akizungumzia kwa wanafunzi walioko kambini, alishauri
kuwepo kwa mavazi maalum, ili kupunguza mrundikano wa nguo, kwenye makaazi yao.
Mwenyekiti wa bodi ya skuli hiyo Dk. Said Mohamed Ali,
aliwakumbusha wazazi na walezi, juu ya ulipaji wa ada kwa wakati, ili kuto
nafasi ya mtiririko mzuri wa usomeshaji.
‘’Kila mzazi wakati anamleta mtoto wake skulini hapa,
alijua kuna mchango wa masomo kila mwezi, sasa inakuaje wanafunzi wafikie miezi
20 au 30 wanadaiwa, hili halivumiliki,’’alifafanua.
Msimamizi wa kambi ya wanafunzi skuli hapo, Mwalimu Haji
Othman Haji, alisema changamoto zaidi ni kwa wanafunzi wa kiume, ambao bado hakujakuwa
na usimamizi madhubuti.
Akiwasilisha muhutasari wa matokeo hayo, mwalimu wa skuli
hiyo Fadhila Rashid Khamis, alisema kwa upande wadarasa la tisa, kulikuwa na
wanafunzi 35, waliofeli ni wanne pekee.
Alieleza kuwa, kwa upande wa darasa la 12, waliofanya mitihani
ni 58 wakiwa wanawake na wanaume idadi sawa, ingawa waliofeli ni 43 sawa na
asilimi 75.4.
Hata hivyo mwalimu huyo, alisema kwa upande wa somo
lililopasiha wanafunzi wengi zaidi ni kemia, bayolijia, Kiswahili na fizikia
kwa darasa la tisa.
Kwa upande wa darasa la 12, somo la uraia liliongoza,
likifuatiwa na lugha ya kiiengereza, jiografia, historia, pamoja na kemia.
Skuli ya sekondari ya Connecting Continent ambayo ina mdarasa
kuanzia la tisa hadi 12, ilianzishwa mwaka 2006 kwa sasa inawafaunzi 320, wakiwemo
wanawake ni 175 na wanaume ni 145.
Mwisho
Comments
Post a Comment