NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
WANAUSHIRIKA wa ‘tujikombowe’ wa
shehia ya Mkombeni wilaya ya Mkoani Pemba, unaojisghulisha na ufugaji wa chaza
lulu, wamepata hasara ya zaidi ya shilingi 600,000 baada ya bidhaa zitokanazo
na rasilimali hiyo, kukosa wateja.
Bidhaa hizo aina
herini pea 25, ambazo moja ni shilingi 25,000 wamelazimika kuzibakisha ofisini
kwao, baada ya kukosa wateja kwa muda mrefu sasa.
Wakizungumza
na mwandishi wa habari hizi, walisema awali walikuwa na changamoto ya ukosefu
wa mashine ya kusarifia bidhaa hizo, ingawa baada ya kuipata sasa changamoto ni
soko la bidhaa hizo.
Walisema,
kwa mara ya kwanza walizalisha herini hizo na kuziuza kwa thamani ya shilingi
300,000 ingawa kwa msimu mwengine walikosa wateja wa bidhaa hizo.
Mwenyekiti
wa ushirika huo Faida Faki Kombo, alisema kwa sasa hawajui herini hizo pea 25
wazifanye nini bali wanachoshuhudia ni kuendelea kuchakaa na kupoteza thamani.
Alieleza
kuwa, soko la wateja wao kwa sasa limepotea na kusababisha kupata hasara, jambo
ambalo wanafikiria namna ya kujitangaaza.
‘’Ni kweli
bidhaa za magamba ya chaza lulu ambazo ni herini pea 25, zimeganda ndani hazina
wateja kwa muda mrefu, jambo ambalo limetuvunja moyo,’’alieleza.
Kwa upande
wake Katibu wa ushirika huo Asha Nassor Makame, alisema baada ya kuona kwenye
mradi wa uzalishaji chaza lulu wamekosa wateja na mashine yao kuharibika, sasa
wameelekeza nguvu kwenye kuusarifu mwani.
‘’Kwa sasa tumeamua
kutengeneza sabuni, siki na mafuta ya bidhaa za mwani, na si haba matunda
yanapatikana, na tunaendesha maisha yetu,’’alieleza.
Hata hivyo
alisema changamoto wanayokumbana nayo ni ukosefu wa taalamu ya kutosha juu ya
utengenezaji wa bidhaa hizo.
Kuhusu wazo
la kuzalisha mwani, alisema ndio mpango wao wa baadae na tayari wameshapeleka
maombi serikali kwa ajili ya kuunganishwa ili kupatiwa vifaa.
Alifafanua
kuwa, wameona kwa sasa wapumzike kidogo kwenye kilimo cha chaza lulu, na nguvu
zao wazilelekeze kwenye kilimo cha mwani.
‘’Tukipata
uwelewa wa kilimo cha mwani na tukivuna tunauwezo wa kusarifu wenyewe, matunda
yanaweza kuonekana kwa muda mfupi kwenye ushirika wetu,’’alieleza.
Mshika fedha
wa ushirika huo wa ‘tujikombowe’ Miza Makame Silima, alisema mradi wa
kutengeneza bidhaa za mwani, umekuwa ukiwapatia manufaa.
‘’Kwa mfano
mara kwanza tujipatia shilingi 300,000 lakini tulipozalisha tena tukapata
shilingi 150,000 ingawa kwa mwaka jana tulijipatia shilingi
500,000,’’alifafanua.
Hivyo,
alisema kama watawezeshwa kimafunzo kupanda mwani wenyewe, huku wakiwa na
utaalamu wa kuusarifu kwa kutengeneza bidhaa kama mafuta, sabuni na siki
wanaweza kupinga hatua.
Kuhusu komba
mikopo serikali, walisema kwanza wanajipanga kuhakikisha wanapata mafunzo ya
upandaji mwani, ili watakapoomba iwe kazi rahisi ya uzalishaji.
Akizungumzia
soko la bidhaa hiyo, alisema sio bay asana ingawa hutegemeana na kipindi
maalum, kutokana na mzungumko wa fedha kuwa mdogo.
‘’Sabuni za
mwani, mafuta, mafusho pamoja na siki, tunaowateha hadi Unguja, na
tukishazalisha hazikai muda mrefu kupata wateja,’’alieleza.
Wateja wa
bidhaa za mwani shehiani humo, walisema wamekuwa wakitumia mafuta yatokanayo na
bidhaa ya mwani, ambayo ni mazuri kwa tiba ya ngozi.
Khamis Issa
Makame anasema, mafuta hayo yanasaidia pia kusafisha ngozi ikiwa mtu anapele
sugu au mba wa muda mrefu.
Aisha Othman
Haji, alisema amekuwa akitumia siki kwa ajili ya kuongeza uchachu kwenye
chakula, jambo ambalo kwa sasa hawezi kuikosa tenda siki hiyo ya mwani.
Sheha wa
shehia ya Makombeni Mwashum Makame Haji, alikiri kuwa ushirika huo, unakabiliwa
na changamoto ya soko kwa bidhaa zitokanazo na magamba ya chaza lulu.
Akizungumzia
kupatiwa mafunzo ili kuendeleza kilimo cha mwani, alisema amekuwa akizungumza
na uongozi wa wilaya na tasisi husika, ili kupatiwa pamoja na vifaa.
‘’Kama kuna
wafadhili ambao wanakiu ya kutaka wanawake kuendelea, waje shehiani mwangu,
kwani wapo wenye hamu ya kufikia ndoto zao,’’alieleza.
Ushirika wa
‘tujikombowe’ wa shehia ya Makombeni wilaya ya Mkoani Pemba, ambao ulianzishwa
mwaka 2007, kwa upandaji wa chaza lulu na utengenezaji wa bidhaa kama herini
zitokanazo na magamba yake, una wanachama 25.
Mwisho
Comments
Post a Comment