NA
HAJI NASSOR, PEMBA:::
MWALIMU
wa skuli ya Madungu msingi Ali Makame Khatib miaka 25, anayetuhumiwa kumbaka
mwanafunzi wake, mwenye miaka 11, leo Oktoba 17 mwaka huu, anatarajiwa kuanza
kujitetea, katika mahkama ya makosa ya udhalilishi mkoa wa kusini Pemba.
Mtuhmiwa huyo anayesimamiwa
na wakili wake Suleiman Omar Suleiman, Oktoba 12, mwaka huu waliiahidi mahkama
hiyo kuwa, leo Oktoba 17, watawasilisha mashahidi wanne mahakamani hapo.
Walidai kuwa, mashahidi hao
wanne wanakuja kupinga juu ya tuhma zinazomkabili, ambazo walidai kuwa hazina
mashiko na nizakupangwa, ili kumchafulia jina lake.
‘’Mheshimiwa hakimu baada ya
kushauriana na mteja wangu, tumeamua kuwa leo hii, tutawasilisha mashahidi
wanne, ambao watawasilisha ushahidi wao, na kisha kuiachia mahakama iendelee na
utaratibu mwengine,’’alidai wakili huyo.
Upande huo wa utetezi,
uliamua kuwa leo hii, watajitetea kwa mtuhumiwa na mashahidi wao kwa njia ya
kiapo, ili ushahidi wao uweze kukidhi viwango vinavyotakiwa.
‘’Mheshimiwa hakim, wakati
ukifika wa kujitetea basi ntapenda nijitetee kwa njia ya kiapo, mimi pamoja na
mashahidi wangu wote wanne,’’alidai mtuhumiwa huyo.
Oktoba 11 mwaka huu, upande
wa mashtaka ulifunga usahidi wao na kuiachia mahakama kutoa uamuzi mdogo,
ambapo kisha Oktoba 12, ikasema kuwa, mtuhumiwa huyo anayo kesi ya kujibu dhidi
yake.
‘’Upande wa mashataka tokea Oktoba 11, mwaka
huu ulishafunga ushahidi wake, baada ya kumskiliza shahidi wake wa mwisho,
askari mpelelezi, hivyo mahkama imeona mtuhumiwa anayo kesi ya kujibu,’’alisema
Hakimu Muumin Ali Juma.
Wakili wa mtuhumiwa Suleiman
Omar Suleiman, alidai kuwa wako tayari kwa ajili ya kujitetea, juu ya tuhma
zinazomkabili mteja wake, kwa njia ya kiapo leo hii.
Wakili wa serikali kutoka
Ofisi ya Mkurugenzi wa mashataka Ali Amour Makame, alidai hana pingamizi yoyote
na uamuzi huo wa mahakama, juu ya kujitetea kwa mtuhumiwa huyo.
Awali ilidaiwa mahakamani
hapo kuwa, mtuhumiwa huyo Ali Makame Khatib miaka 25, mkaazi wa Matuleni wilaya
ya Chake chake, alidaiwa kumbaka mtoto wa miaka 11.
Ambapo kufanya hivyo ni kinyume
na kifungu 108 (1), (2) (e) na kifungu cha 109 (1) cha sheria ya Adhabu nambari
6 ya mwaka 2018, sheria ya Zanzibar.
Tuhma ya pili alilitenda
August 12, mwaka huu, majira ya saa 11:30 akiwa skuli ya Msingi Madungu wilaya
ya Chake chake, ambapo alidaiwa kumbaka mtoto huyo.
Mwisho
Comments
Post a Comment