NA
HAJI NASSOR, PEMBA::
MAHKAMA ya maalum ya makosa ya udhalilishaji ya mkoa wa kusini Pemba, iliyopo Chake chake imesema, mwalimu wa skuli ya Madungu msingi Ali Makame Khatib miaka 25, anayetuhumiwa kumbaka mwanafunzi wake, anayo kesi ya kujibu juu ya tuhma hizo.
Hakimu wa mahakama hiyo
Muumin Ali Juma, alisema kilichobakia mbele yamtuhmiwa huyo, ni kujitayarisha kwa
ajili ya kujitetea, hasa baada ya upande wa mashtaka, kufunga ushahidi wake.
Aliyasema hayo Oktoba 12,
mwaka huu wakati mtuhumiwa huyo anayewakilishwa na mawakili wawili, juu ya
tuhma za kumbaka mtoto wa miaka 11, akiwa juu ya kizimba cha mahkama hiyo.
Hakimu huyo, aliuuliza
upande wa utetezi, juu njia watakayoitumia kufanya utetezi, ikiwa ni ya kiapo
ama bila ya kiapo, ambapo ukaeleza utatumia njia ya kiapo siku hiyo.
‘’Upande wa mashataka tokea
Oktoba 11, mwaka huu ulishafunga ushahidi wake, baada ya kumskiliza shahidi
wake wa mwisho, askari mpelelezi, hivyo mahkama imeona mtuhumiwa anayo kesi ya
kujibu,’’alisema Hakimu.
Wakili wa mtuhumiwa Suleiman
Omar Suleiman, alidai kuwa wako tayari kwa ajili ya kujitetea, juu ya tuhma
zinazomkabili mteja wao, kwa njia ya kiapo.
‘’Mheshimiwa tumeshauriana
sisi mawakili na mteja wetu kuwa, siku ambayo mahkama itapanga, tutajitetea kwa
njia ya kiapo na tunao mashahidi wetu wanne,’’alidai.
Hivyo baada ya pande zote
mbili kukubaliana, mahkama imelighairisha shauri hilo hadi Oktoba 17, mwaka huu,
huku upande wa utetezi ukitakiwa kuwasilisha mashahidi wao.
Wakili wa serikali kutoka
Ofisi ya Mkurugenzi wa mashataka Ali Amour Makame, alidai hana pingamizi yoyote
na uamuzi huo wa mahakama, juu ya kujitetea kwa mtuhumiwa huyo.
Wiki mbili zilizopita,
mtuhmiwa huyo, alilazimika kurejeshwa tena rumande hadi Oktoba 11, mwaka huu,
baada ya kuwasili mahakamani hapo, akisubiri shahidi mpelelezi, ingawa
hakuhudhuria mahkamani hapo.
Awali ilidaiwa mahakamani
hapo kuwa, mtuhumiwa huyo, bila ya halali na akijua kuwa mtoto huyo yuko chini
ya uangalizi wa wazazi wake, alimtorosha na kumpelekea nyumbani kwake.
Kufanya hivyo ni kosa,
kinyume na kifungu 113 (1) (a) cha sheria ya Adhabu nambari 6 ya mwaka 2018, sheria ya
Zanzibar.
Mwisho
Comments
Post a Comment