NA SALMA LUSANGI, ZANZIBAR
NAIBU Waziri wizara ya Maji, Nishati na
Madini Zanzibar Shaaban Ali Othman, amesema Zanzibar hakuna biashara ya mchanga
hivyo, eneo la Taveta na maeneo mengine ya hawarusiki mtu kufanya biashara
hiyo.
Hayo aliyasema
wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati akikagua barabara ya ndani
iliyojengwa na Wizara yake, ili kurahisisha upatikanaji wa huduma ya hiyo
huko Donge Pangatupu Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Alisema wizara
ya kupitia Idara yake ya Nishati na Madini imeshatoa maelekezo, kwamba wananchi
wanatakiwa waombe huduma hiyo moja kwa moja kupitia mfumo maalum.
Alisema
hakuna ugumu katika upatikanaji wa huduma ya mchanga kwa njia ya mfumo
hadi huduma hiyo kumfikia mtumiaji, hivyo maeneo Taveta na maeneo mengine
sio rasmi kuuza mchanga na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, haiko tayari
kuruhusu mtu yeyote kufanya biashara hiyo.
“Kumekua
na ukaidi ambao sio walazima sana, hii inatusababisha sisi tuweze kutumia
sheria zaidi, kwasababu maelekezo yameshatolewa si mara moja si mara mbili
lakini bado, ufahamu umekuwa mdogo,’’alieleza.
Alisema
changamoto kubwa ilikuwa ni miundombinu ya barabara kutoka kwenye barabara kuu
hadi kwenye shimo la mchanga, lakini Wizara imetengeneza barabara hiyo yenye
urefu wa kilomita 2 kwa gharama kubwa, ili kuwaondolea usumbufu watumiaji.
Naye
dereva wa gari la mchanga Mussa Salum Haji, alisema Serikali, ikiwafikiria kuwaruhusu
wafanye biashara ya mchanga kama bidha nyengine, kwasababu wameshajiajiri katika
eneo hilo.
Mapema
Mwenyekiti wa upakiaji mchanga Willian Robert alisema, kamati yake inaishukuru
uongozi wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini, kwa kutengeza barabara hiyo ya
ndani.
Alieleza
kuwa, kwani gari za mchanga zilikuwa zinachukua muda mrefu kutoka kwenya
barabara kuu hadi kufika kwenye shimo la mchanga.
Mwisho.
Comments
Post a Comment