NA HAJI NASSOR, ALIPOKUWA UNGUJA
MWENYEKITI Kamati ya Maadili ya
Baraza la Habari Tanzania MCT- Jaji mstaafu Robart Makaramba, amesema nguvu
iliyonayo chombo cha habari ni kubwa, hivyo suala la kuzingatia na kufuata maadili
kwa vitendo halina njia mbadala.
Alisema,
maadili ndio msingi mkuu kwa vyombo vya habari, kutekeleza wajibu wao vyema, na
kinyume chake kikitumika vibaya nguvu zake, kinaweza kuleta madhara.
Mwenyekiti
huyo aliyaeleza hayo August 9, mwaka 2022 mjini Unguja, kwenye mkutano wa siku
moja, wa waandishi wa habari, wahariri na wadau wa habari, katika mkutano maalum
wa kujadili maadili ya wanahabari.
Alisema,
kila mwandishi akiamua kuyafuata kwa vitendo maadili ya kazi yake, jamii
hawatakwazwa na vyombo vya habari, kama ilivyo sasa kwa baadhi ya vyombo kuyapa
kisogo.
‘’Niwakumbushe
sana suala la kufuata maadili yenu, maana nyinyi waandishi na wahariri mnanguvu
kubwa mno, hata zadi ya bunduki na upanga,’’alieleza.
Akizungumza
kwenye mkutano huo, Katibu Mtendaji wa MCT-Kajubi Mukajanga, alisema baraza
limekuwa likikutana na vyombo vya habari mara kwa mara, ili kuwakumbusha wajibu
wao.
Alisema, mkutano
huo ambao pia ulihusisha wadau, ni muendelezo wa MCT, kuhakikisha vyombo vya
habari haviwi sehemu ya uchafuzi wa amani na utamaduni wa watanzania.
‘’Ijapokuwa
zipo sheria zinazokwaza utendaji wa waandishi wa habari, lakini ni vyema
tuhakikisha tunafanya utafiti na kuchambua habari kwa kina,’’alieleza.
Mapema Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya maadili ya MCT, Tanzania Eda Sanga, aliwakumbusha watangaazaji
kupunguza utani, lugha zisizo rasmi wanapokuwa studio.
‘’Wapo
watangaazaji wanaifanya studio kama vile ni vyumba vyao vya mapunziko,
wanatumia lugha zisizorasmi na kupotosha kazi ya utangaazaji,’’alieleza.
Kwa upande
wake Afisa Mdhamini wa Baraza la Habari Tanzania MCT ofisi ya Zanzibar, Shifaa
Said Hassan, amewakumbusha waandishi na wahariri, kuzidisha ushirikiano, ili
kuwapa habari nzuri wananchi.
Wadau wa
habari akiwemo Said Rashid kutoka Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’
ofisi ya Pemba, aliwataka waandishi kujiamini na kuacha woga, ili kuhakikisha
wanaibua habari zilizojificha.
Mkurugenzi
wa Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA-Zanzibar Dk. Mzuri
Issa, alisema wakati umefika kwa Zanzibar, kuwa na sheria mpya ya habari.
‘’Sheria inayotumika
sasa ya Magazeti nambari 5 ya mwaka 1988 ni ya zamani, na haiko rafiki katika
kutimiza majukumu ya waandhsi wa habari hapa Zanzibar,’’alieleza.
Mwandishi wa
habari Issa Yussuf na Mhariri wa habari Juma Khamis walisema, lazima sheria
rafiki ziwepo Zanzibar, ili tasnia ya habari iimarike kwa waandishi kufichua
maovu.
Mwisho
Comments
Post a Comment