NA HAJI NASSOR, PEMBA:::::
WATAALAMU wa afya ya mama na mtoto kisiwani Pemba, wamewakumbusha
wanawake, kuhakikisha hawawalishi chakula au aina yoyote ya kimiminika, watoto
wao wachanga, kama bado hawajatimiza miezi miezi sita, kwani kufanya hivyo,
huwapa ukuaji bora na wenye afya.
Walisema ukuaji bora na wenye afya kwa mtoto, na
hasa baada ya kuzaliwa, huchangiwa na mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na wazazi
kuacha kuwalisha watoto wao chakula au aina ya yoyote ya maji.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, wataalamu
hao walisema, kumlisha chakula hata laini au aina yoyote ya maji mtoto ambae hajatimiza
miezi sita, ni kuilazimisha mishipa na mashine ya kusagia kufanya kazi
isiyoimudu.
Mmoja kati ya wataalamu ambae ni muuguzi wa mama
na mtoto wa Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani, Rabia Mohamed Ussi, alisema hali
hiyo, hupelekea kuzuka kwa magonjwa ikiwa ni pamoja na utampia mlo.
‘’Hata kama mtoto analia kwa ishara ya njaa,
lakini hakuna namna ya kumpa chakula au aina yoyote ya maji, na likifanyika
hilo ni kumpelekea kupata athari, na kubwa zaidi ni kudunisha ukuajia wake,’’amesema.
Kwa upande wake Msimamizi wa kitengo cha lishe
Wilaya ya Chake Chake, Harusi Masoud Ali, anasema kufuata utaratibu wa kumnyonyesha
kwa akina mama, huwapa ukuaji mzuri mtoto.
Alisema ndani ya miezi sita ya kwanza, mwili wa
mtoto hujitayarisha kwa ajiali ya chakula, au maji maji na ikifanyika vyenginevyo,
ni kulazimisha na kupelekea athari.
Alisema wapo baadhi ya akinamama, wamekuwa wakijishiriki
kwenye kazi za muda mrefu, na kucha utamaduni wa kuwanyonyesha watoto na kisha
kuwalisha kabla ya wakati.
‘’Tunasisitiza kuwa, ili mtoto apate makuzi
mazuri, afya njema na kujiepusha na utapia mlo ni vyema wazazi wachunge miezi
sita ya mwanzo wasiwalishe aina yoyote ya chakula,’’alieleza.
Nae mtaalamu wa malezi ya
kisayansi na makuzi ya awali ya mtoto ‘SECD’ Omar Mohamed Ali, alisema upo
uwezekano mkubwa wa mtoto kuwa na ufahamu wa kina, ikiwa wazazi watafuata
maelekezo ya wataalamu.
‘’Bado jamii wamekuwa wakiona
kama utani, wanapoambiwa wasiwalishe watoto wao chakula au maji, maana maziwa
ya mama yanavirutubisho na madini ya kutosha kwa ajili ya maisha ya mtoto,’’alifafanua.
Akizungumza hivi karibuni,
kwenye mafunzo ya siku sita kwa waandishi wa habari, maafisa ustawi na
maendeleo wa baadhi ya mikoa, na kufanyika Dodoma, mkufunzi wa mafunzo ya ‘ECD’
Davis Gisuka wa tasisi ya Children in Crossfire Tanzania, alisema jamii
inapaswa kushirikina katika malezi.
‘’Tukizungumzia makuzi na
maendeleo ya awali ya watoto, wanaume wamekuwa wakijitenga, jambo ambalo sio
sahihi, kwani mama peke yake, hawezi kuwa na mtoto bora,’’alieleza.
Meneja ‘ECD’ tasisi ya Maendeleo ya
Binadamu kutoka Chuo Kikuu cha Aga Khan, Mombasa Joyce Marangu, alisema
upatikanaji wa chakula bora kwa mama mzazi, humpa ari ya kunyonyesha mtoto
wake.
‘’Moja ya faida kubwa ya malezi ya ‘ECD’
kwa wazazi na walezi ni kugundua ufahamu na umahiri wa mtoto, tokea mapema,
lakini hata juu ya uwezo wake wa kutambua mambo kadhaa,’’alifafanua.
WAZAZI
Wazazi Asha Hilali Nassor na mwenzake
Aisha Othman Dadi wakaazi wa Mizingani Mkoani, wanasema wamekuwa
wakiwanyonyesha watoto kabla ya miezi sita ya mwanzo kumalizika, kutokana na
wao kukosa mlo kamili hapo awali.
Wanasema, bado jamii inaona suala la
makuzi na malezi bora ya mtoto ni jukumu la mama peke yake, wakisahau
wanayonafasi ya kuwapatia chakula na lishe bora wakati wote.
Omar Khamis Haji na Mohamed Issa Omar
wa Chake chake, wanasema elimu ya kuanzisha bustani ya mboga mboga, bado iko
chini na ndio maana waliowengi wanapoelezea lishe kwa mama, hufikiria mayai na
samaki mkubwa.
Khadija Hamza Shehe, mwenye watoto
wawili, anasema mtoto wake wa kwanza mwenye miaka sita, anaufahama duni,
ikilinganishwa na mwenye miaka minne.
‘’Wa kwanza alikuwa analia mno,
alipofika miezi mitatu, nilianza kumpa maji, na chakula laini, na huyu wa pili
alianza kula akiwa ni miezi saba, lakini wanatofautiana hata kiafya,’’anasema.
RIPOTI INASEMAJE YA UNICEF
Ripoti mpya ya ulimwengu iliyotolewa
na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto ‘UNICEF’ iitwayo siku za mwanzo za maisha ya kila mtoto ni muhimu ‘Early
Moments Matters for Every child’ inasema kipindi tokea kutunga kwa
mimba, ni mihimu.
Ripoti hiyo inasema ni kipindi
mwafaka na adimu kwa wazazi, katika kuandaa vyema na kuujenga ubongo wa mtoto
wao mchanga, na takuwa na wapesi wa ufahamu wa mambo kadhaa katika maisha yake.
Ripoti inafafanua kuwa, watoto hata
wakiwa tumboni wanahitaji huduma bora mfano afya, lishe, kuchangamshwa, fursa
za kujifunza na kuyaelewa mazingira yao kwa haraka.
‘’Watoto milioni 55, wameripotiwa
kudumaa duniani kote, na wengine milioni 230 wanaishi katika mazingira
yaliyoathiriwa na machafuko na wanakabiliwa na msongo wa mawazo, huku watoto
wengine milioni 300 wakiishi katika maeneo yalioathiriwa na uchafuzi na
uharibifu wa mazingira,’’aimefafanua.
Tanzania imetajwa kwenye ripoti hiyo
kuwa, inao maelfu ya watoto wanaokosa vichochezi vya ukuaji vinavyolea ubongo
wao, ikiwemo lishe duni sawa na asilimia 34 ya watoto waliochini ya miaka
mitano.
Mwisho
Comments
Post a Comment