NA HAJI NASSOR, PEMBA:::-
MAMLAKA ya Kuzuia Rushwa
na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar 'ZAECA' Pemba, imesema iko katika hatua za mwisho
za kukamilisha uchunguuzi, kabla ya kumfikisha mahakamani Askari wa Jeshi la
Kujenga Uchumi Zanzibar 'JKU' anayetuhumiwa kupokea rushwa, kwa hadaa ya
kuwaajiri vijana.
Akizungumza
na waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa ‘ZAECA’ mkoa wa kaskazini Pemba Nassor
Hassan Nassir, alisema kwa sasa watendaji wake wako katika hatua za kumalizia
uchunguuzi huo, kabla ya hatua nyingine.
Alisema
kuwa, lazima wajiridhishe kila eneo kwenye uchunguuzi wao, maana ‘ZAEC’A
haikuanzishwa kwa lengo la kumuonea mtu, bali ni kufuata taratibu za sheria
kama zilivyo.
Alieleza
kuwa, baada ya kumshikilia mtu yeyote, hawawezi kumfikisha moja kwa moja
mhakamani, lazima kuna hatua za kiufundi na kisheria wazipitie, ili
litakapofikishwa kwa ofisi Mkurugenzi wa Mashtaka, jalada liwe na vigezo.
‘’Kuhusu
tuhma za Askari wa JKU kumshikilia, ni kweli tunae na hatujamuachia, na
tunaendelea na upelelezi ambao umeshafikia hatua za mwisho, na wananchi wasiwe
na wasi wasi,’’alieleza.
Hata
hivyo amewaka wananchi kuendelea kufuatilia vyombo vya habari juu ya kesi hiyo,
kwani wakati wowote atafikishwa mahakamani kujibu tuhma zinazomkabili.
Juni 3
mwaka huu, Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar ‘ZAECA’
ilimshikilia Askari wa ‘JKU’ Zaharan Mohamed Zaharan miaka 33 mkaazi wa
Chokocho wilaya ya Mkoani Pemba, kwa tuhuma za kuomba rushwa ya fedha.
Alieleza
kuwa, mtuhumiwa huyo kwa nyakati tofauti mwaka huu 2022, akiwa mtumishi wa
Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar 'JKU' akiwa na cheo cha ‘private’ bila ya halali
alijipatia fedha kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 2.4.
Kamanda
huyo wa ‘ZAECA’ alifafanua kuwa askari huyo akijua kuwa hana uwezo, alipokea
fedha kwa vijana watatu, akiwaeleza ana uwezo wa kuwapatia ajira, jambo ambalo
ni kosa kisheria.
Hata
hivyo amewataka wananchi kuendelea kuripoti matukio hayo, kila wanapoyasikia na
kuwaomba watumishi wa umma na wengine kujitenga mbali na rushwa.
mwisho
Comments
Post a Comment