IMEANDIKWA NA SAIDA ALI, PEMBA@@@@
Mohamed Omar Mohamed mkaazi wa Machomane Chake Chake Pemba mwenye ulemavu wa miguu, ameiomba Serikali na jamii kwa ujumla kumsaidia kupata kiti cha magurudumu (wheelchair) kitakachomuwezesha kuendeleza shughuli zake za kijamii na kiuchumi kwa wepesi zaidi.
Akizungumza na ZanzibarLeo hapo nyumbani kwake Machomane, Mohamed amesema kiti ambacho amekuwa akikitumia kwa sasa kina zaidi ya miaka mitano na kimechakaa vya kutosha kiasi cha kushindwa kutembelea kwa mwendo unaoridhisha.
Amesema kiti alichonacho hivi sasa kimepoteza nguvu na kimekuwa kikiharibika mara kwa mara, hali inayosabisha kubaki muda mrefu bila ya kiti hicho kutokana na ughali wa matengenezo yake.
Amesema mara nying kiti hicho huharibika betri ambayo imekuwa ikiuzwa kwa bei ya Tsh. 80,000, kiwango ambacho si rahisi kwake kukimudu kutokana kipato chake kidogo.
"Najiona dhaifu mno. Kiti mwendo ndio miguu yangu nilojaaliwa na Allah. Kutokana na hali ngumu ya kimaisha, nashindwa kununua chengine. Kiti changu kinatumia betri nne na kila betri moja ninainunua elfu thamanini, ni ghali sana," alifafanua Mohammed.

Amesema kipato chake ni kidogo sana kiasi ambacho hakimtoshelezi wala hakikidhi baadhi ya mahitaji yake kutokana na hali ya ugumu wa kimaisha na ukiangalia ana familia na watoto wanaomtegemea.
Aliendelea kusema haina haja ya kukaa barabarani akawa omba omba jambo ambalo halipendezi kutokana na taswira ya miji yao, hivyo aliziomba Taasisi husika kumsaidia kuendeleza genge lake linalojishughulisha na biasha ndogo ndogo za vyakula vikavu ili kujikwamua kimaisha.
Muhamed alitoa wito kwa Serikali na Taasisi na Mashirika binafsi kumuangalia kwa macho mawili kutokana na hali yake ya uhitaji wa watu maalumu angalau kumpatia kiti cha magurudumu(wheelchair) au kumuendelezea kigenge hilo linalompatia ruzuku zake za kila siku.
Kwa upande wake sheha wa Wara Masoud Mohamed Khamis amethibitisha kuwepo kwa Mohamed shehiani mwake kutokana na uhitaji wake wa watu wenye ulemavu amekuwa akimpatia fursa kubwa zinazotokea shehiani mwake.
"Nipo nae bega kwa bega pakitokea fursa ya aina yoyote ya ikiwa watu wenye mahitaji maalumu hata isiwe ya makundi maluum simuachi nyuma hata mafunzo na neema zinapokuja namuangalia kwa uono mpaka kutokana na hali yake" alifafanua sheha.
Alisema ndani ya shehia yake kupitia watu wenye mahitaji maalum kutokana na uhitaji wao amekuwa akiwashirikisha kwa kila fursa zinazotokea kupitia vikundi vya wajasiria mali, ili kujikwamua kiuchumi.
" Mpka sasa Watu wenye mahitaji maalumu tumekuwa tukishiriana nao juu ya mahitaji yao ili wajione na watambue wana haki ya kufanya kila kitu kama mtu mwengine". alivyoa alieleza sheha.
MWISHO.
Comments
Post a Comment