IMEANDIKWA NA REHEMA MOHAMED PEMBA@@@@
JAMII inashauriwa kuwa karibu na watoto wenye ulemavu, ili kuwapatia haki zao za msingi ikiwemo elimu.zuh
Hayo yalizungumzwa na sheha wa shehia ya Chambani wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko kijijini kwao.
Alisema kuwa, watoto wenye ulemavu wanahitaji zaidi uangalizi wa mama na baba na sio kumuachia mzazi mmoja peke yake au kumtelekeza kwa bibi.
Alisema, katika jamii kuna baadhi ya watu mara baada ya kupata mtoto ambae ana ulemavu, huamua kumtenga na kumuachia katika uangalizi wa mzazi mmoja hususani mama ili kuweza kukaa nae na baadhi ya wakati kushindwa kuwapatia hata huduma.
Alieleza kuwa, si jambo la busara kabisa kwa watoto wenye ulemavu kuwaweka nyumbani bila ya kuwapatia elimu, kwani nao wanayo haki ya kupata elimu bora, kupatiwa matibabu pamoja na mahitaji mengine kama watoto wengine.
Vile vile alisema kuwa, ni vyema jamii iondoshe itikadi mbaya ya kuwa mtoto mwenye ulemavu hawezi kufanya chochote bali wajelewe kwamba wanao uwezo wa kusoma na kufanya viziri kama watoto wengine, kwani ulemavu haumzuii mtu kushiriki katika shuhuli za kimaendeleo.
Aidha sheha huo alisema kuwa, wamefanikiwa kuwarudisha skuli watoto wenye mahitaji maalum katika shehia ya Chambani na kuweza kufanya viziri katika masomo yao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuia ya Elimu Kwanza Development Organization (EKWADEO) Khalfan Ali Faki alisema kuwa, wanafanya juhudi ya kupita kila hehia na kuhakikisha kuwa, kila mtoto ambae ana ulemavu na ana uwezo wa kupata kusoma basi wanajitahidi kumsaidia kumpeleka skuli.
Alisema kuwa, ni jukumu la wazazi kuwapatia watoto mahitaji yao ya kila siku ikiwemo elimu, lakini wakishindwa kufanya hivyo watawasaidia.
"Tunafanya kazi ya kupitia katika shehia moja baada ya nyengine kutafuta watoto wenye ulemavu na kuwasaidia katika maeneo ambayo kuna mapungufu hasa hasa maeneo ya elimu, kwani ndio msingi bora wa maisha," alifafanua.
Aidha aliwataka wazazi kuwa karibu na viongozi wa Jumuia hiyo kuwasaidia wakati wanapokumbwa na changamoto ili kuweza kuwalea watoto wao katika mazingira yaliyo bora.
MWISHO.
Comments
Post a Comment