WAZIRI wa Nchi, Afisi ya Rais- Katiba, Sheria
na Utawala Bora Zanzibar Mwalimu: Haroun Ali Suleiman, anatarajiwa kuwa mgeni
rasmi, katika jukwaa la nne la msaada wa kisheria, linalotarajiwa kufanyika
Zanzibar mwaka huu.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu,
Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar hajjat: Hanifa
Ramadhan Said, alisema maandalizi yote ya jukwaa hilo, yameshakamilika.
Alisema, miongoni mwa mwaandalizi hayo ni kupatikana kwa
mgeni rasmi, ukumbi, mialiko kwa washiriki 140 kutoka Tanzania bara, Kenya,
Pemba na wenyeji kisiwani Unguja.
Mkurugenzi huyo alieleza kuwa, kwa upande wa washiriki kutoka Kenya, Tanzania bara na hata Zanzibar ni watoa mada, ingawa kwa upande wa Pemba na Unguja washiriki, ni makundi mbali mbali.
‘’Kwa mfano katika jukwaa hili la nne, linalotarajiwa
kufanyika kuanzia Novemba 20 hadi 21 mwaka huu, miongoni mwa waalikwa ni
wasaidizi wa sheria na wanaasasi za kiraia,’’alifafanua.
Waalikwa wingine ni masheha, watoa msaada wa kisheria, mawakili,
jeshi la Polisi, wanaharakati wa haki za binaadamu, waendesha mashtaka, ofisi ya Mwanasheria mkuu na watendaji
wa mahkama.
Aidha Mkurugenzi huyo wa Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria
Zanzibar, aliwataka waalikwa wote, wawe tayari wameshakaa kwenye maeneo
waliopangiwa sio zaidi ya saa 2:30 asubuhibi.
‘’Kwa mara hii jukwaa hili la nne la mwaka la msaada wa kisheria,
tunatarajia kufanyika ukumbi wa Michezani Mall, na mgeni rasmi ameshatbitisha
ushiriki wake,’’alifafanua.
Hata hivyo, aliwataka wakurugenzi kuwasimamia watu wao waliobahatika
kushiriki, ili kuhakikisha wanajali muda wa kufika, ili kufanikisha jukwaa
hilo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mkurugenzi wa Jumuiya ya Wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba ‘CHAPO’ Mohamed Hassan Abdalla, alisema, tayari watendaji watatu wakaokwenda wameshajulishwa.
Alieleza kuwa, majukwaa kama hayo yamekuwa na msaada mkubwa kupitia jumuiya zao, kwani huwapa mbinu, elimu wanapokutana na wananchi.
‘’Kwa mfano, katika jukwaa la tatu lililopita, sisi ‘CHAPO’
tiliporudi tulikwenda kwa wananchi, tukiwa na mbinu tofauti za utoaji wa elimu,
ushauri na masaada wa kisheria, tuliovuna kwenye jukwaa hilo,’’alieleza.
Nae Mkurugenzi wa Jumuiya ya wasadizi wa sheria wilaya ya
Mkoani ‘MIDAPAO’ Nassor Hakim Haji, alisema majukwaa hayo, huwapa fursa ya
kukutana na wadau kadhaa, wa haki jinai.
‘’Tunapokutana na magwiji wa kisheria kama mawakili huwa
tunaongeza uwezo, ujuzi na maarifa mapya, kwa ajili ya kazi zetu nyingine,’’alieleza.
Akizugumza hivi karibuni, Mkuu wa Diveshini ya Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Pemba Bakar Omar Ali, alisema, majukwaa hayo yana maana pana kwa wasaidizi wa sheria.
‘’Ukiwa makini kusikiliza mada zinazowasilisha pamoja na
zile ripoti, unaweza kuondoka na hata wazo la kulifanyia kazi, nadani ya
jumuiya,’’alieleza.
Akizungumza
kwenye jukwaa la mwaka jana, aliyekuwa mwakilishi wa taasisi ya ‘LSF Wakili
Alphonce Gura, alisema Zanzibar, imekuwa sehemu ya kujifunzia, katika utoaji wa
msaada wa kisheria, kwa nchi za Afrika Mashariki.
Alieleza kuwa, hayo
yamejitokeza tokea lilipomalizika jukwaa la pili la msaada wa kisheria la mwaka
2022, lililofanyika Zanzibar, na kuibuliwa maazimio 13, yaliyotekelezwa.
Wakili huyo, alifafanua
kuwa, kwa nchi za Ruwanda, Burundi, Uganda, Kenya na hata Tanzania bara,
Zanzibar imekuwa kinara na sehemu ya kujifunzia, utoaji wa msaada wa kisheria.
‘’LSF,
tunaridhishwa na tunapongeza mno, kazi zinayofanywa Idara ya Katiba na Msaada
wa Kisheria Zanzibar, kwa kuongeza wigo na kusababisha kuchukua nafasi ya
kwanza, kwa utoaji wa msaada wa kisheria,’’alifafanua.
Akizungumzia kanzidata,
ambayo imeanzishwa na LSF mwaka 2013, inayoangalia na kuzichakata kazi,
zinazofanywa na wasaidizi wa sheria, mmoja mmoja kwa Tanzania.
Kupitia kanzidata
hiyo, imedhihirisha uhitaji mkubwa wa msaada wa kisheria na kufikia watu
200,000 kila mwaka na kufikia watu milioni 7 kwa mwaka, wanaohitaji elimu ya
sheria Tanzania.
Ujumbe wa mwaka huu, wa jukwaa la nne la mwaka la msaada
wa kisheria ni ‘ushawishi wa upatikanaji wa rasilamali za kuendeleza
huduma za msaada wa kisheria Zanzibar’ .
Mwisho
Comments
Post a Comment