NA
HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
MAKAMU
Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake wa CCM Tanzania ‘UWT’ Zainab Khamis Shomar,
amesema CCM, itaendelea kuhubiri amani na utulivu, maana ndio mwalimu wa vyama
vingine vya siasa nchini.
Alisema, CCM baada ya kuwahudumia wananchi
wote wa Tanzania bila ya ubagauzi, msingi wake mwingine ni kuhubiri umoja,
mshikamano, amani na utulivu kwa nia ya kuwaunganisha watu wote.
Makamu huyo Mwenyekiti
ameyasema hayo jana, uwanja wa Umoja ni Nguvu wilaya ya Mkoani Pemba, kwenye
mkutano wa hadhara uliowajumuisha wana ‘UWT’ wa wilaya za Mkoani na Chake
chake, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuimarisha chama kisiwani humo.
Aliwataka viongozi wa
UWT, kuanzia ngazi ya shina hadi taifa kuendelea kuhubiri jambo hilo, kwani
ndio msingi mkuu wa kwa chama hicho na vyama vingi vingine.
Alieleza kuwa, hata
chama kinachopanga kufanya machafuko, kamwe hakiwezi kufanikisha lengo lao,
kama nchi hii haina amani na utulivu.
‘’Sisi UWT na jumuia
nyingine za chama, tumekuwa tukihimiza kila siku, kuwa ajenda yetu ya kwanza
iwe ni kuhubiri amani na utulivu, kisha kuleta maendeleo kwa kila
mtu,’’alifafanua.
Aidha Makamu Mwenyekiti
huyo wa UWT taifa Zainab Khamis Shomar, aliwapongeza rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan na Dk. Hussein Ali Mwinyi wa
Zanzibar, kwa kuchapuza miradi ya maendeleo.
Alieleza kuwa, tayari
Dk. Mwinyi kwa upande wa Zanzibar ameshavuuka lengo la utekelezaji wa Ilani ya
CCM ya mwaka 2020/2025, katika miradi kadhaa, aliyowaahidi wananchi wakati
akiomba raidhaa.
‘’Kwa mfano, aliahidi
ujenzi wa vyumba 1,500 vya madarasa, wakati wa kampeni ingawa ndani ya miaka
yake mitatu ya utawala ameshajenga vyumba 2,273 hapa ameshavuuka lengo kwa
asilimia 150,’’alifafanua.
Katika hatua nyingine,
Makamu huyo Mwenyekiti wa UWT Taifa Zainab Khamis Shomari, aliwataka vijana
ambao hawajasajili vikundi vyao vya ushiriki, kufanya hivyo haraka.
Alisema, tayari UWT
imeshafanya mazungumzo na wahusika, moja wapo ni kulegeza mashrti ili
kuhakikisha kila mwenye sifa anapata mkopo.
‘’Wakati nazungumza na
baadhi ya wajasiriamali hapa Pemba, nimegundua kuwa uhitaji ni mkubwa, lakini
masharti yanawarejesha nyuma waombaji,’’alifafanua.
Hata hivyo,
amewagauikia wanaume, wenye sifa kufunga ndoa na kuacha udhalilishaji kwa
watoto, kwani kufanya hivyo ni kuwazimia ndozo zao.
Mapema Waziri wa Elimu
na Mafunzo ya Amali Zanzibar Leila Mohamed Mussa, alisema kasi ya Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, imekuwa kubwa katika sekta mbali
mbali.
Alifamisha kuwa, Dk.
Mwinyi ameridhia kuwa shilingi bilioni 550, kati ya shilingi bilioni 830,
zitumike katika miundombinu ya elimu.
‘’Ndani ya fedha hizo
zinatumika ujenzi wa skuli za ghorofa, ukarabati na ununuzi wa samani, ili
kuhakikisha watoto wa Zanzibar wanasoma kwenye mazingira rafiki,’’alifafanua.
Akitoa taarifa za
utekelezaji wa Ilani kwa mkoa wa kusini Pemba, Mkuu wa wilaya ya Mkoani Khatib
Juma Mjaja, alisema kasi ya Dk. Mwinyi imekuwa kubwa ikilinginishwa na watu
wanavyoizungumza.
Katib wa CCM mkoa wa
kusini Pemba Ramadhan Kapeto, alisema CCM Mkoani humo, inathamini kwa vitendo
juhudi za Dk. Mwinyi ambazo zimewafikia, watu wote bila ya ubaguzi.
Akimkaribisha Makamu
Mwenyekiti huyo, Mwenyekiti wa UWT mkoa wa kusini Pemba Zuwena Khamis Abdalla,
alisema kwa utekelezaji imara wa Ilani ya CCM uchaguzi wa mwaka 2025, unaweza
kuwa mwepesi.
Makamu Mwenyekiti wa
UWT taifa akiwa na ujumbe wake alitembelea soko la Machomane, kuzungumza na
wajasiriamali juu ya namna ya kupata mikopo hiyo.
Mwisho
Comments
Post a Comment