NA
MARYAM NASSOR, ZANZIBAR
WATU
wamekuwa wakiamini kuwa talaka ndiyo kimbilio, la matatizo yote yanayowakumba katika
maisha ya ndoa.
Katika dini ya kiislamu, talaka iko kisheria, ingawa
maadiko matakatifu na yasio na shaka, ni haramu ambayo Muumba ameichukia.
Na
wapo wanaoamini hata wakati wa kutolewa kwake ama kuandika, Imani inakubali
kuwa, mbingu hutikisika, ishara kuwa si uamuzi sahihi sana.
Ijapo
kuwa, maana ya ndoa ni mkataba wa hiari
ambao hufungwa kwa makubaliana baina ya mume na mke, ingawa pale
inapofika kuwa ndoa hiyo haina misingi
ya kuendelea tena, basi hupelekea kutoka kwa talaka.
Mohamed
Issa Ali mwanaharakati wa haki za watoto kisiwani Pemba, anashangaa kuona
wanandoa hao kutowafikiria watoto ambao watawakosesha mapenzi na malezi ya
wazazi wawili.
Na
huwa hamufikirii hata kwa dakika chache tu, kuwa lile janga la vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia kwa
watoto hao.
Utakuwa
na uhakika gani kuwa, ule ulezi wa pande moja siku hizi unaitwaa ‘single mother’
utakavyooathiri malezi na makuzi ya watoto.
Asha
Fadhil (36) mkaazi wa Mahonda anasema
yeye ni shuhuda wa mateso ya Watoto wanne wa kiume, waliyoachwa na wazazi wao
baada ya kuachana na kupelekwa kwa bibi yao mzalia baba Mahonda.
Akizungumza
na mwandishi wa Makala haya, alisema Watoto hao mkubwa wao alikuwa ana umri wamiaka
16 na wapili alikuwa na miaka 13 na watatu alikuwa ana miaka 10 basi yule
watatu alikuwa akimlawiti yule ndugu yao wa mwisho aliyekuwa na umri wa miaka sita.
Alisema
kuwa, kila ikifika usiku alikuwa akimsikia akilia kwa uchungu, na yeye kama
mzazi alikuwa akijiuliza huyu mtoto ana shida gani usiku.
Anasema,
siku moja asubuhi aliamka na kuwasubiri wanaenda kucheza, akawaita na kuwauliza
kwanini ndugu yao huwa analia kila ikifika usiku ndipo wakasema kuwa,huwa
anavuliwa suruali na kaka ake anaelala nae na kumfanyia kitendo kibaya.
“Nilitokwa
na machozi, kuwaona Watoto wale wanavyomtesa ndugu yao, kumbe kaka zake walikuwa wanamlawiti’’
alisema kwa masikitiko.
Aidha,
alisema kuwa chakushangaza Watoto wale walikuwa wanaishi na bibi na babu yao,
lakini hakuna hata mmoja aliyekuwa anajali.
Ali
Issa Kinole, Sheha wa shehia ya Mahonda alisema kuwa, baada ya kupata habari za
manyanyaso ya Watoto hao, walitoa taarifa kwa watu wa ustawi wa jamii na kuja
kuzungumza nao, ili wawashuhulikie Watoto wale vizuri.
Mrajisi wa mahkama ya kadhi, Iddi Said Khamis anasema talaka za kiholela zinaweza kusababisha
vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa
kijinsia.
Alisema,
takribani kesi nyingi za watoto unao wasikia kufanyiwa vitendo vya
udhalilishaji basi,mara nyingi huwa wanaishi na mzazi mmoja inaweza kuwa
wanaishi na mama pekee au baba na mama wa kambo.
Alisema
kuwa, kwa sasa hali ni mbaya, talaka za kiholela zimekuwa ni
nyingi, wanandoa hushindwa kustahamiliana na kuona suluhu pekee ni
talaka.
Ingawa
kwenye dini ya kiislamu, talaka imeruhusiwa
lakini ni jambo ambalo linamchukiza sana Muumba.
Aidha
alisema kuwa,kitakwimu talaka zinazotolea kiholela zimekuwa zikiongezeka siku
hadi siku.
Alisema,
kwa mwaka 2023 jumla yakesi 909 zimeripotiwa katika mahkama ya kadhi wilaya ya Mwanakwerekwe
Unguja pekee.
Na
kesi 66 zimeripotiwa katika mahkama ya Mwera Unguja, huku kwa upande wa mahkama
ya kadhi ya wilaya ya Makunduchi zilikuwa 60.
Aidha
alisema kuwa, kwa upande wa Pemba kuliripotiwa kesi 119 kwa Mahkama ya kadhi ya
wilaya ya Wete na kesi 45 kwa mahkama ya Konde.
Mrajisi
huyo alisema kuwa, katika mahkama ya kadhi ya wilaya ya Chake chake ilionekana
kuongoza kwa upande wa Pemba, ikiwa na kesi 126 za talaka.
Alieleza
kuwa, kwa upande wa wilaya ya Mkoani , ziliripotiwa jumla ya kesi 64 na katika mahkama ya kadhi ya Kengeja
zilifikishwa kesi 10.
Aidha,
alisema kwa mwaka 2022 kulikuwa na kesi 416 zilizoripotiwa katika mahkama ya
kadhi za wilaya Unguja na Pemba.
Alisema
kuwa, ‘’utaona jinsi gani talaka zinavyotolewa kiholela, na kusahau kuwa
zimeruhusiwa lakini kwa utaratibu maalum uliyowekwa’’,alisema.
Mratibu
wa chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania, TAMWA Zanzibar Dk. Mzuri
Issa Ali alisema, talaka siku zote sio nzuri kwa wanandoa, wanapaswa kukaa
pamoja na kutafuta suluhu ya matatizo yao, mbali ya talaka.
Alisema
kuwa, wazazi wanapotengana kwa sababu zozote zile, basi wanao umia zaidi ni
watoto, kwani huwa ni wadogo na wanahitaji malezi na mapenzi ya wazazi wawili.
Aidha
alisema kuwa, watoto hupitia kipindi kigumu katika maisha yao, pale ambapo
wazazi hupeaana talaka.
Alisema
kuwa, watoto waliyopitia vipindi vigumu vya kutengana kwa baba na mama, haawezi
kusahau katika maisha yao yote, shida na
mateso waliyapata.
“Hivyo,
tunashauri wazazi wakae pamoja kuzungumza tofauti zao, lakini si kuona suluhu
pekee ni kupeana talaka,”alishauri.
Alifafanua
kuwa, wao TAMWA- Zanzibar wataendelea kutoa elimu juu ya madhara yatokanayo na
talaka, kupitia vyombo vya habari, ili kuwe na jamii bora ,ambayo inajikinga na
vitendo vya udhalilishaji.
Fatma
Ali Bakar, Mwanasheria kutoka chama cha
wanasheria wanawake Zanzibar ‘ZAFELA’ alisema
kuwa wanawake wanatakiwa kusoma ili kutimiza ndoto zao za kielimu.
Alisema
kuwa, sababu moja wapo ya talaka ni kuwa wanawake wengi hukatishwa masomo na
kupewa mume, hivyo bado wanakuwa hawajaandaliwa kisaikolojia kuingia kwenye ndoa.
Nae,
Mratibu wa maswala ya udhalilishaji shehia ya Mahonda Semeni Bundala, alisema
kuwa kwa upande wa shehia hiyo, huwa wana toa ushauri kwa wana ndoa kuwa, wakae
na kuzungumza tofauti zao.
Alisema
kuwa, wanapo achana baba na mama basi watoto ndiyo, wanaoteseka na kupelekea
kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji.
Sheikh
Nahoda Haji wa msikiti wa Mahonda,
alisema kuwa talaka ni jambo baya linalomchukiza mungu, hivyo ni bora wazazi kuacha jazba kwa kutaka
kuoneshana nani bora kuliko mwenzake.
Aidha
alisema kuwa, talaka huchangia vitendo
vya udhalilishaji kwa watoto kwani, wazazi wakiwa mbali mbali kila mmoja huwa
hana muda na watoto wao.
Nae,
Askofu Stephen Aron wa kanisa la Mahonda, alisema kuwa katika dini yao talaka
hairuhusiwi kutokana na kuwa wanaamini atakae muunganisha mungu, basi hakuna
atakae mtenganisha.
Hivyo,
jambo la talaka limekemewa vikali na dini yao, na hivyo wao hawaruhusu litokee,
mpaka mmoja wao atakapo fariki.
Nao,
baadhi ya wazazi waliyo wahi kuachwa na kuwaachia ulezi wa pekee yao, Bifarida
Sudi wa Chuini mkoa wa mjini wa Magharibi alisema, kuwa talaka ni jambo baya
sana, kwani watoto hukosa malezi ya pamoja ya baba na mama.
Alisema
kuwa, yeye alipoachwa alikuwa anashinda ndani na kulia, alikuwa hajui la
kufanya na watoto wadogo akiangalia hana kazi wala ndugu wa kumsaidia.
“Wazazi
tunatakiwa kuzungumzia tofauti zao ili tupate suluhu, kwani watoto huteseka
sana wakiishii na mzazi mmoja kwani hatuwezi kuwamalizia shida zao, hata kama
mzazi atakuwa na kipato kizuri,’’ alisema.
Nae,
Mzee Ali Faki Sungura alisema yeye alimuacha mkewe tu, kwasababu alikuwa haoni
njia nyengine ya kupita zaidi ya talaka.
Alisema,
baada ya kumuacha talaka zote tatu ndipo
alipokuja kutoka kwenye usingizi mzito aliyokuwa nao,na kukumbuuka ule msemo
usemao” amekumbuka shuka kumesha kucha.
MWISHO
Comments
Post a Comment