NA NIHIFADHI ISSA, UNGUJA@@@@
NI kawaida kwa watoto wa kike wakifikia umri kuanzia miaka 10, kubaleghe na kutokanana na maumbile siku hizo huanzia tatu (3) hadi saba (7).
Kiutaratribu watoto hutakiwa kwenda skuli kuanzia siku 20 hadi 22 kwa mwezi mmoja lakini watoto wa kike hususan walioko vijijini, huenda skuli siku 15 hii hutokana na kuingia kwenye kawaida yaao na kukosa taulo za kujisitiri.
Zanzibar
yenye watu wapatao milioni 1.8 huku idadi ya vijana ikiwa ni Zaidi ya 600,000 inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa elimu ya afya na hedhi salama
kwa wanawake
Sharon Robert
akiwa Mkurugenzi wa taasisi ya 'holding hands
foundation' alifanya utafiti mwaka 2019 na kugundua kuwa, watoto wakike wanaoishi
nje ya mji wanakosa kwenda skuli siku 84 kwa mwaka, katika ya siku 180
wanazotakiwa.
Akiwa
mwanamke na kiongozi kwenye taasisi yake Hii ilimfanya Sharon kuanzisha kampeni
ya kukusanya taulo za kike na kuwapa wasichana bure maskulini.
Sharon
alianza ugawaji wa taulo za kike mwaka
2020 ambazo anazipata taulo hizo kupitia watatii wanaokuja visiwani Zanzibar
pamoja na wadau wengine.
Licha ya
kuwa mama, mke yeye pia ni Meneja wa
hoteli ya Shangani kupitia nafasi hiyo humkutanisha na wageni kupata taulo za
kike ambazo huzisambaza katika skuli za msingi na sekondari mjini na vijijini
lengo kumsaidia mtoto wa kike kupata haki yake ya elimu bila ya ikwazo
chochote.
Sharon anasema kuwa mwanamke ni kiongozi, mzazi na mlezi na ni vyema kuwasaidia wanawake wengine na anaamini ikiwa wasichana watapata taulo za kike watahudhuria masomo yao kwa siku 230 ndani ya mwaka.
''Nafanya hivi nikiwa chini ya taasisi lakini pia nikiwa
mwanamke kwasababu utafiti tulioufanya wasichana wengi hawana uwezo wa kupata
taulo, kwa kila mwezi kwa hiyo natumia nafasi yangu wakija watalii
nawaeleza hali iliyopo na wao hutoa mchango wao,”alisema Sharon.
Hadi kufikia Disemba 2023 mwanamke huyu ameshawafikia wasichana 8,000 kwa Unguja huku mlengo ni kuwafikia
wasichana 23,000 hadi kufikia mwaka 2025 kwa miaka minne.
''Iili msichana afikie ndoto zake za kuwa kiongozi bora ni lazima aandaliwe mazingira mazuri ya kujifunza na ili ajifunze vyema ni lazima ahudhurie skuli kama ambavyo wavulana wanahudhuria,''anasema.
Utafiti kutoka taasisi ya haki ya elimu nchini Tanzania unaonesha wasichana hukosa siku nne hadi saba za masomo kutokana na kuwa kwenye siku zao za hedhi
Hali hii
inapelekea wanafunzi wanawake kukosa fursa ya kufanya baadhi ya mitihani na hivyo ufaulu wao
kushuka kutokana na kukosa cha kujihifadhia wakati wa kupata siku zao
Mradi huo wa
kugawa taulo za kike kwa wasichana kwa skuli za msingi na sekondari umewafikia wanafunzi wa skuli ya Machui,
Jendele, Eden kwa upande wa Unguja
Tatu Shaban ni Mwalimu mkuu skuli ya msingi Jendele, Mkoa wa kusini Unguja wilaya kati, amesema bado kuna changamoto ya wasichana kutokuhudhuria masomoni wakiwa na sababu mbalimbali ikiwemo ya kukosa taulo zao.
''Wasichana hulazimika
kubaki nyumbani mpaka siku zake za hedhi zimalizike, ndio arudi skuli kutokana
na kukosa cha kujihifadhia, hivyo hukosa masomo kwa kipindi karibia siku saba, lakini wakipatiwa misaada hiyo ya taulo hawana sababu ya kubaki
nyumbani,’’amesema.
Anaeleza kuwa, hii ni mara ya pili kupata
msaada wa taulo za kike, kwa wasichana
wa skuli ya Jendele, ambapo mara kwanza walipata kwa mwaka mzima na mara pili kwa miezi sita.
Ashura Said ni mwanafunzi wa darasa la saba katika skuli hiyo, amesema hii ni mara ya pili kupata taulo za kike, japo kuwa alikuwa hakosi vipindi vya masomo, lakini hakuwa na amani wala haimpi uhuru akiwepo darasani.
’’Nashukuru kwa msaada huu mara hii, nakaa kambi kwa ajili mya mitihani zitanisaidia sana kujihifadhi, kwani
nimefahamishwa pia jinsi ya kuzitumia,’’amesema Ashura.
Wanafunzi wengine waliofikiwa na huduma ambayo imetokana na jitihada za kiongozi mwanamke ni skuli ya Machui msaada wa taulo hizo za kike imekuwa ni mkombozi kwao, kwani awali wakipata siku zao, wakiwa mazingira ya skuli huona aibu kwa vile hutokea ghafla na hulazimika kuazima nguo za kujihifadhia kwa majirani.
‘‘Tumefurahi mno kupata taulo hizi, ilikuwa tukipata siku zangu tukiwa skuli tunachafuka na
kupata aibu sasa inatubidi tuwagongee majirani watusaidie tujisitiri ndio hapo tunarudi nyumbani masomo yanatupita,’’anakumbuka Mwanafunzi huyo wa skuli ya Machui.
Suala la
uongozi kwa mwanamke sio tu la kuteuliwa au kuchaguliwa kiuchaguzi bali hata
kujitoa katika jamii na kuonesha uwezo wa kusaidia wengine kwa kutatua
changamoto zilizopo.
Kwa mujibu
wa waliofikiwa na msaada huo maono ya mwanamke kiongozi Sharon kuwasadia watoto wa kike taulo kumewajenga kujiamini wakiwa skuli pamoja na uhakika wa kutokukusa
vipindi vya masomo tofauti na awali.
MWISHO
Comments
Post a Comment