NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
IMETAJWA kuwa, wanawake wanapohaingaikia
hudumza za kijamii kama vile maji safi na salama, huduma za afya ya uzazi,
elimu ya lazima hupoteza mwelekeo wa kudai haki zao za kisiasa, demokrasia na
uongozi.
Hivyo,
mamlaka husika zimeombwa kuimarisha huduma hizo kwa haraka, katika vijiji mbali
mbali kisiwani Pemba, ili kuhakikisha kundi la wanawake, linafikiwa na huduma
hizo kwa ukaribu.
Ushauri huo
umetolewa leo April 27, 2023 na wadau wa haki za wanawake, kwenye mkutano wa siku moja, wa
kusikiliza changamoto na ufumbuzi wake, zinazowakabili wanawake kutodai haki
zao, zilizoibuliwa na wahamasishaji jamii, waliomo kwenye Mradi wa
kuwahamasisha wanawake kudai haki zao, unaoendeshwa na TAMWA, PEGAO na ZAFELA
na kufanyika Chake chake.
Walisema, wanawake
wanayo haki ya kuwa viongozi katika maeneo kama ya jimbo, kwenye jamii,
serikali na hata kwenye asasi za kiraia, lakini kutokana na kukabiliwa na
changamoto za utafutaji wa huduma za kijamii, hukosa kutilia maani jambo hilo.
Mmoja kati
ya wadau hao, Mratibu wa TASAF Pemba Mussa Said Kisenge, alisema wanawake
wamekuwa wakikabiliwa na changamoto za ukosefu wa karibu wa huduma zao muhimu.
‘’Ijapokuwa,
kwa mfano kupitia TASAF serikali imeanzisha mpango wa kuziwezesha familia
maskini, ili wanawake wafikirie namna ya kudai haki zao, lakini bado wapo
wanaokabiliwa na changamoto,’’anasema.
Nae Afisa
Mipango wilaya ya Chake chake Kassim Ali Omar, alisema ikiwa huduma ya maji
safi na salama, huduma za afya ya mama na mtoto zitapatikana kwa urahisi,
wanawake wanaweza kuongezeka, katika kudai haki zao za uongozi.
Nae Mjumbe
kutoka chama cha siasa cha ACT-Wazalendo Saleh Nassor Juma, alisema wanawake
wanayohaki ya kuongoza, iwe kwenye siasa, serikalini au katika asasi za kiraia.
Akifungua
mkutano huo, Mratibu wa TAMWA-Zanzibar ofisi ya Pemba Fat-hya Mussa Said,
alisema huo ni mfululizo wa kukutana na wadau, ili kuibua changamoto
zinazowakabili wanawake katodai haki zao.
‘’Wanawake
wanayohaki ya kudai haki zao katika demokrasia, siasa na uongozi, na ndio maana
zaidi ya mikutano 70 kwenye shehia mbali mbali kisiwani Pemba, tumeshaifanya ya
kuihamasisha jamii, juu ya jambo hilo,’’alieleza.
Nae
Mkurugenzi wa PEGAO Hafidh Abdi Said, alisema suala la utetezi wa haki za
wanawake, sio jukumu la asasi za kiraia pekee, bali kila mmoja kwa nafasi yake.
Alisema, wizara
ya elimu ikiweka mazingira ya upatikanaji elimu bora na wizara ya afya
ikiimarisha huduma za afya, hapo mwanamke atakuwa na hamu ya kufikiria suala la
uongozi.
Nae Mratibu
wa mradi wa kuihamasisha jamii kudai haki zao za uongozi, siasa na demokrasia ‘SWIL’
kutoka PEGAO Dina Juma alisema, kila mmoja akitimiza wajibu wake, wanawake
wanaweza kuongezeka katika nafasi mbali mbali za uongozi.
‘’Kinachoonekana,
bado baadhi ya makundi ya watu hawajawaamini wanawake kuwa wanaweza kushika uongozi
na kuongoza, sasa dhana hii ikiondoka wengine zaidi wataonekana,’’anafafanua.
Akiwasilisha
changamoto na mafanikio, muhamasishaji jamii kutoka wilaya ya Chake chake
Hassain Omar Salim alisema, baada ya kukutana na wanawake kadhaa kisiwani
Pemba, wapo walioweka nia ya kuingia majimboni, katika uchaguzi mkuu ujao.
‘’Kwa mfano
wilaya ya Micheweni pekee tumepata wanawake 35, lakini karibu kila wilaya wapo
wanawake wasiopungua 25 walioweka nia, hii ni ishara nzuri na mafanikio ya
ziara zetu,’’alifafanua.
Kwa upande
mwengine, muhamasishaji jamii huyo, alisema baada ya kuibua changamoto kwa
jamii, zipo zilizofanyiwa kazi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa nyumba, vituo vya
afya, ujenzi wa daraja na kurejeshwa skuli kwa wanafunzi watoro.
Tayari wahamasishaji jamii kisiwani Pemba
ambao wanatekeleza mradi wa ‘SWIL’ unaoendeshwa na PEGAO, ZAFELA na
TAMWA-Zanzibar wameshazifikia shehia zaidi 70, kwa wastani wa wananchi 3,000
kuwapa elimu ya umuhimu wa wanawake kuwa viongozi.
Mwisho
Comments
Post a Comment