JUKWAA LA PILI LA MSAADA WA KISHERIA ZANZIBAR
2022
Laibua maazimio 16 yenye shabaha ya
uimarishaji utoaji msaada wa kisheria
LSF yaahidi makubwa, Mkurugenzi
Hanifa aupiga mwingi
NA HAJI NASSOR, PEMBA::
DISEMBA 13 na 14 mwaka 2022, ilikuwa
ni siku adhimu na adimu, zilizofanyika jukwaa la pili la msaada wa kisheria Zanzibar.
NINI MAANA YA JUKWAA?
Ni mkutano,
mjadala, kongamano la wazi linalowakutanisha wadau wa haki jinai, kujadili,
kubadilishana uwezo na kukosoana, kwa njia amani.
Maana
kupitia jukwaa hilo, linalowakutanisha wadau zaidi ya 200 kutoka Unguja na
Pemba, huandaliwa na wizara ya Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, chini
ya Idara ya Katiba na Msaada wa kisheria.
Jukwaa hilo,
liliwakutanisha watoa msaada wa kisheria, wasaidizi wa sheria, mahakimu,
waendesha mashtaka, wanufaika wa msaada wa kisheria, Polisi, masheha na
wanaasasi za kiraia.
Kwa jicho la
kawaida utaona kuwa, jukwaa hilo linamtiki kwa wadau hao kukutana, na kujadili
changamoto, mafanikio, mwelekeo na dira ya baadae, ya utaoji wa msaada wa
kisheria.
LSF
Tasisi hii,
imekuwa ndio mdau mkuu wa Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria sio tu,
kufanikisha majukwaa kama hayo, lakini hata, kuiwezesha Idara, kufikia malengo
yake.
Ijapokuwa
Idara hiyo ni ya serikali, lakini kupitia sheria yake nambari 13 ya mwaka 2018
ya Msaada wa Kisheria na hata sera yake ya mwaka 2017, hazijakataa kushirikiana
na wadau.
Ndio maana,
katika jukwaa la mwaka huu, ambalo lilifanyika tena Chuo cha Utalii Maruhubi
mjini Unguja, na kufunguliwa na Makamu wa Pili wa rais Hemed Suleiman Abdulla,
mwakilishi wa LSF alitoa neno.
‘’Niiombe
sana serikli kuhakikisha, sheria ya Msaada wa Kisheria Zanzibar, nambari 13 ya
mwaka 2018, ifanyiwe marekebisho,’’anasema Lulu Mwanakilala.
Mwanakilala
hapa, kumbe hakulala alichoona ni kufuatia ushauri huo kwa serikali, kutaka kuwepo
kifungu kipya, kinachoruhusu uanzishwaji kwa Mfuko wa Msaada wa Kisheria
Zanzibar ‘MMSAKIZA’
Hapa
akisema, mfuko huo sasa unaweza kuchangiwa na serikali na watu wa asasi za
kiraia, au mtu mmoja mmoja, ili sasa kuwasaidia watoa msaada wa kisheria
Zanzibar.
Jengine
alilolishauri kwenye jukwaa hilo, Lulu anasema wakati umefika kwa wasaidizi wa
sheria, ambao hawana mishahara kupewa ofisi chini Idara ya serikali za Mitaa,
ili wapunguze gharama za kukodi ofisi.
IDARA YA KATIBA, MSAADA WA KISHERIA
ZANZIBAR
Ambapo Mkurugenzi wa Idara hii, Hanifa Ramadhan Said wakati
akisoma yataokanayo na jukwaa la mwaka 2021, anasema yapo mengi yaliotekelezwa,
baada ya kupendekezwa.
‘’Kwa sasa wasaidizi wa sheria wetu, wanavitumia vyombo vya
habari wanapokuwa na shughuli zao za kutoa elimu kwa wananchi,’’anasema.
Hata suala la ushirikiano, kati ya wasaidizi wa sheria na
watendaji wa serikali, unatia moyo, jambo ambalo limerahisisha utendaji wa kazi
zao.
Mkurugenzi Hanifa hakuacha kuipongeza tasisi ya LSF, kwa
kuendelea kuwaunga mkono, katika utekelezaji wa shughili zao hasa za kujengeana
uwezo.
Kisha kwenye siku ya pili, kabla ya jukwaa hilo kufunguwa
akasoma maazimioa 16 yalioibuliwa na kupitishwa na washiriki wa jukwaa hilo.
Yote ni mazuri
na moja wapo ni kwa LSF kuendelea kusadiana kuwajengea uwezo watendaji wa Idara
ya Katiba na Msaada wa Kisheria, pamoja na kufunguliwa kwa ofisi za wasaidizi
wa sheria katika ofisi ya wilaya.
‘’Kuhakikisha
kuandika ripoti za utendaji kazi, kwa kugusia malengo 17 endelevu ya dunia, ili
kuonesha muitikio wa jamii pamoja na kuimarisha mifumo, itayohakikisha taifa
linakuwa na raia wema,’’alifafanua.
Azimio
jengine ni kwa Idara hiyo, kuhakikisha inachukua juhudi za kuratibu na kufanya
marekesbisho ya sheria ya Msaada wa Kisheria, ili kuweka mfuko wa taifa wa
Msaada wa kisheria.
Mkurugenzi
huyo akasema azimio jingine ni kuongeza kasi ya mafunzo ya usuluhishi na
utatuzi wa migogoro kwa wasaidizi wa sheria.
Afisa sheria wa Idara hiyo Unguja Ali Haji Hassan, anasema
lazima wasaidizi wa sheria, wazidishe kasi ya kuwafikia wananchi kuwapa elimu,
ushauri na msaada wa kisheria.
SERIKALI KUU
Makamu wa
Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdullah, yeye ndie aliyekuwa mgeni rasmi,
katika jukwaa hilo, na kuelezea namna wasaidizi wa sheria, wanavyofanya kazi
zao.
Licha ya
kuvutiwa huko, amewakumbusha wasaidizi wa sheria na watoa msaada wa kisheria, kuendelea
kufanya kazi zao kwa uweledi.
Hapa, akasema
hasa nguvu zaidi kwao ni mapambano ya udhalilishaji, rushwa na dawa za kulevya,
ambazo zinaendelea kugharimu maisha ya vijana.
Maana anaona
kuwa, bado jamii inakabiliwa na changamoto hizo, hivyo ni wajibu wao kuendelea
kutumia weledi wao, ili wananchi waishi kwa salama, bila ya kuwa na changamoto
hizo.
Lakini hata
waziri wa Nchi Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora
Zanzibar, Haroun Ali Suleiman, yeye akasema, serikali, inajua kazi inayofanywa
na wasaidizi wa sheria.
Hapa nae
akawasisitiza wasaidizi wa sheria wazidishe kasi na juhudi za kuhakikisha, wanaifikisha
elimu husika kwa jamii.
Mwalimu
Haroun, kama wengi wanavyomuita, akaendelea kutoa darssa kwa wasaidizi hao wa
sheria kuwa, serikali itaendelea kuwa karibu mno, na Idara ya Katiba na Msaada
wa Kisheria.
Lengo
anasema kwanza kuwatia moyo watendaji hao wanaoongozwa na Mkurugenzi Hanifa,
ili kuona wanafanikisha malengo yao, ya kuifikia jamii.
‘’Muelewe
kuwa, kazi hii ya utoaji wa masaada wa kisheria ni kazi ya kujitolea zaidi, na
malipo yenu ni kwa Muumba zaidi, hivyo endeleeni kuwasaidia wananchi, ili wapate
haki zao kisheria,’’alieleza.
Lakini
Makamu wa Pili, alikumbushia ahadi yake kuwa, yuko tayari kuusaidia mfuko wa
msaada wa kisheria, mara utakapoanzishwa, ili kuhakikisha unasaidia kusukuma
mbele dhana ya utoaji wa msaada wa kisheria.
Jambo hili lilizua
shangwe, vifijo, furaha na kushangiliwa na kupigiwa makofi na wasaidizi wa
sheria, waliojazana kwenye jukwaa hilo la mwaka 2022.
‘’Mheshimiwa
Waziri, mimi naunga mkono uanzishwaji wa mfuko huo, na niko tayari hata
mshahara wangu mmoja kuuweka, na naamini na wengine watasaidia,’’aliweka bayana.
Zamu ikafika
ya Naibu Katibu Mkuu wizara ya Nchi Afisi ya Katiba, Sheria, Utumishi na
Utawala Bora Zanzibar Omar Haji Gora, amefurahishwa na uamuzi wa waziri Haroun,
pale alipoiagiza Tume ya Kurekebisha sheria Zanzibar, ili kuifanyia marekebisho
sheria ya msaada wa kisheria, Zanzibar no 13 ya mwaka 2018.
‘’Ushauri wa
wenzetu wa tasisi ya LSF, kuwa sasa sheria yetu tuifanyie marekebisho, ili
itambuwe uwepo wa mfuko wa maalum wa msaada wa kisheria, kama ilivyo kwa
wenzetu wa Tanzani bara,’’anafafanua.
Akafafanua
kuwa, jukwaa hilo ni utekelezaji wa sera ya mwaka 2017 na sheria ya msaada wa
kisheria no 13 ya mwaka 2018.
Akafurahishwa
na tasisi ya LSF kuwa, imekuwa karibu mno na Idara ya Katiba, Msaada wa
Kisheria, katika kufanikisha majukumu yake, hasa ya kuhakikisha, wananchi
wanapata haki zao na ufumbuzi wa mambo ya kisheria.
WADAU WA SHERIA
Kwenye
jukwaa hilo, wapo waliopata nafasi ya kusema jambo, akiwemo mwakilishi kutoka
Umoja wa watu wenye Ulemavu Zanzibar ‘UWZ’ Shaibu Abdalla Mohamed, akasema kuna
ahuweni kwa watu wenye ulemavu, juu upatikanaji wa msaada wa kisheria.
‘’Jukwaa
hili la pili na sisi kushirikishwa kikamilifu hadi kutoa mada ni hatua moja,
maana kwa jukwaa la kwanza hatukushirikishwa kikamilifu,’’anasema.
Kwenye hili,
mwakilishi kutoka LSF Said Chitung, akasema kundi la watu wenye ulemavu, lazima
liangaliwe kwa macho manne, katika kuwafikia kielimu.
Akichangia
kwenye jukwa hilo, Said Rashid Hassan wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’
tawi la Pemba, akasema lazima suala la utoaji wa msaada wa kisheria, liendelee
kwa kasi.
Akitoa mada ya
saikolojia ya jamii na upatikanaji wa msaada wa kisheria kwa wahanga na
waathirika wa udhalilishaji katika mfumo wa haki jinai, wakili wa serikali Ali
Rajab, anasema ni jambo la kuzingatiwa mno.
‘’Hata
matumizi ya maneno wakati wa kumuuliza, kumtaka akuelezea nini alichofanyiwa,
usipokuwa makini unaweza kumzidishia maumivu,’’anafafanua.
Anasema
saikolojia kwa jamii wakati mwengine, mfano mdhalilishaji haonekani kama ni
mtenda kosa kubwa kama kisheria, hivyo lazima kwa watoa msaada wa kisheria
walijue hilo.
‘’Ndio maana
wapo wanaodhalilishwa, wamekuwa wakikataa kutoa ushahidi makahamani, kwani
saikolojia yao kwao hilo sio kosa kubwa,’’alifafanua.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’ Harusi Miraji Mpatani, yeye
akavishauri vyama vya wanasheria, lazima viongeze nguvu, ili jamii ipate msaada
wa kisheria.
Hoja yake ni
kuwa, msaada wa kisheria umewalenga wale watu maskini zaidi, hivyo lazima
viongozi wa vyama na wale wanasheria, wawasaidie wananchi.
WASAIDIZI/WADAU SHERIA WANASEMAJE
Mkurugenzi
wa Jumuia ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake ‘CHAPO’ Nassor Bilali
Ali, anasema kazi inayofanywa na Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria ni
nzuri.
‘’Hata sisi
jumuia za wasaidizi wa sheria, inafaa kwa kila aliyepata mafunzo kuwapa wenzake,
maana wakati mwengine inakuwa ngumu wasaidizi wote kufikiwa,’’anasema.
Mkuugezi wa
Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Kaskazini ‘A’ Asiya Fadhil Makame, anasema
moja ya changamoto wanayokumbana nayoni kukosa elimu ya saikolojia.
‘’Elimu ya
mapambano dhidi ya ukatili na udhalilishaji, tunayo ingawa sasa elimu ya
saikolojia ndio shida, na wakati mwengine tunawakosa kuongozana na waathirika
kwenye mahojiano,’’alisema.
Lakini hata
Mkurugenzi wa wasaidizi wa sheria wa sheria wilaya ya Mkoani Nassor Hakim,
anasema kupitia jukwaa hilo, linawapa mwanga kwa kule kubadilishana uzoefu na
wengine.
Kumbe hili
la uwepo wa jukwaa, hata profesa Mohamed Makame kutoka Chuo Kikuu cha Taifa cha
Zanzibar ‘SUZA’ anasema, suala la usaidizi wa sheria, linafaa kuungwa mkono na
jamii.
‘’Chimbuko
la msaada wa kisheria ni la kujitolea zaidi, kwa ajili ya kuwafikishia huduma
za msaada wa kisheria, tena bila ya malipo,’’anasema.
Jukwaa hilo
lilifungwa Disemba 14, 2022 na Waziri Haroun, ambae aliwataka wasaidizi wa
sheria, kuyafanyiakazi, yale waliyoyapata kwenye jukwaa hilo.
Ambapo ujumbe wa mwaka huu ni ’Uimarishaji
wa Huduma Bora na endelevu za utoaji wa msaada wa kisheria Zanzibar ‘’.
Mwisho
Comments
Post a Comment