WAZIRI SAADA MKUYA ALIA NA MIUNDOMBINU ISIYORAFIKI KWA WATU WENYE ULEMAVU BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR
NA HAJI NASSOR, PEMBA
WAZIRI wa nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar dk. Saada Mkuya Salim amesema bado watu wenye ulemavu wanaendelea kukabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo wanaofika baraza la wawakilishi kwa shughuli mbali mbali.
Dk. Saada Mkuya aliyasema hayo Machi 7 mwaka 2022 ukumbi wa hoteli ya Maru maru mjini Zanzibar alipokuwa akifungua mafunzo ya siku2 ya uandishi wa habari za watu wenye ulemavu yalioandaliwa na Shirika la Internews kupitia mradi wa vyombo vya habari jumuishi nchini. Internews in Tanzania
Alisema muhimili wa baraza la wawakilishi lilipaswa kuwa mfano mzuri wa kuweka miundombinu rafiki kwa kundi la watu wenye ulemavu ili iwe rahisi kwao wanapowagania haki zao.
Alieleza kuwa hivi karibuni alimshuhudia mwanamke aliyealikwa barazani hapo akibebwa na wanaume ili kufika juu sehemu ya wageni. Internews
Aidha Waziri huyo aliipongeza Internews Tanzania kwa kuwajengea uwezo waandishi wa habari katika kuibua changamoto za watu wenye ulemavu Zanzibar.
Hata hivyo amewataka waandishi hao kuendelea kulitetea kundi la watu wenye ulemavu ili wapate haki zao.
Mapema Mratibu wa progam kutoka Internews Tanzania Shaaban Maganga alisema mafunzo hayo ni muendelezo wa kuwajengea uwezo waandishi wa habari.
Alieleza kuwa kundi la watu wenye ulemavu linahitaji watetezi wakiwemo waandishi wa habari na hasa baada ya kujengewa uwezo.
Nae kiongozi wa mradi wa vyombo vya habari jumuishi kutoka Kenya Jackie Lidubwi alisema Tanzania ndio pekee iliozalisha habari 376 kwa nchi nyengine zinazotekeleza mradi huo.
Nae mwakilishi kutoka shirikisho la watu wenye ulemavu Zanzibar SHIJUWAZA Juma Salim Ali alisem watu wenye ulemavu wana haki sawa na wengine.
Alieleza kuwa vyombo vya habari ni muhimu katika kufanikisha upatikanaji wa haki zao.
Comments
Post a Comment