Skip to main content

Tukiwapa uongozi wanawake sio hidaya ni haki yao kikatiba

                                             


 NA HAJI NASSOR, PEMBA

INAWEZEKANA wapo wanaodhani kuwa suala la kumpa uongozi mwanamke, kuanzia shehia hadi taifa, ni kama hidaya kutokwa kwa wenye mamlaka.
Hidaya ni zawadi ambayo inawezekana mtu asipewe au pewe kwa mtoaji akiona ipo haja hiyo.
Na wale wenye mamlaka na uwezo wa kushawishi mwanamke kupata nafasi ya uongozi, hudhani kuwa hili ni hidaya.
Maana utasikia kauli kutoka kwa viongozi wanaume wakisema kuwa, kamati ya shehia fulani kama ina wajumbe 12, basi angalau wanawake wawe watatu.
HALI HALISI
Wanawake wanasema wamekuwa wakishuhudia kauli za kukatisha tama kuwa, hutumika maneno kama vile angalau wanawake wawili, lazima wanawake waepo.
Asha Hassan Omar wa mtandao wa wanawake Mkoani anasema, imekuwa kama zawadi kutokana kwa wanaume wanapotaka kupewa nafasi.
Anasema kwa karne hii tayari wameshapa uwelewa wa jinsi ya kuongoza, sasa hakuna majaribio tena kuwapa uongozi wanawake bali kama ni haki, itekelezwe.
Anabainisha kuwa sheria mama ambayo ni katiba, inavyo vifungu ambavyo vinaeleza kuwa, kila mmoja yuko sawa mbele ya sheria, hivyo hakuna zawadi katika hilo.
“Mwanamke na mwanamme wote wako sawa mbele ya sheria, sasa iweje sisi wanawake tuonekane kwenye masuala ya uongozi kama ni hidaya na wala sio haki,’’anasema.
Mwanajuma Hija Kombo wa Chake chake anasema, sasa wapewa haki zao uongozi, maana wameshakaa nje kwa karne kadhaa jambo ambalo liliwaacha nyuma.
Anasema zipo taasisi za watu binafsi kama vike TAMWA, wameshawawezesha kiuongozi, hivyo mamlaka husika zihakikishe kuna kuwa na usawa kwenye uongozi.
Hata mwanaharakati wa haki za wanawake na watoto wa mjini Wete Sahaba Mussa Said, katika moja ya mikutano yake, aliwahi kusema kuwa suala la uongozi kwa wanawake sio hidaya.
“Kama kundi la wanaume wanapewa nafasi za uongozi bila ya mwenye mamlaka kuhoji uwezo wake, hivyo na sisi kikatiba tuko sawa,’’anafafanua.
Katika eneo jengine mwanaharakati huyo, anasema kama kwenye suala la uchaguzi kwa maana ya kupiga kura wanawake huweko mbele, kampeni ni uwingi wa kwenye vyama na uongozi isiwe ajenda.
WANAWAKE WAHAKI YA KUWA VIONGOZI?
Kaimu Mwanasheria wa wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba, Mohamed Hassan Ali anasema jawabu ni kweli kuwa mwana haki sawa na wanaume kwenye uongozi.
Anasema sasa baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa vyama vingi ndani ya taifa la Tanzania bara na visiwani, ni wakati kwa wenye mamlaka kuona waliona kundi hilo.
“Wapo wanawake wa mfano mzuri hapa Zanzibar akina Amina Salum Ali, Salama Mbarouk Khatib ambae kwa sasa ni mkuu wa mkoa wa kaskazini Pemba na hata mawiziri wa sasa akina Riziki Pemba wamefanya vizuri,’’anasema.
Khadija Omar Hamza wa Pujini anasema sasa wapewa nafasi nao waongoze ndani ya Zanzibar na hata kule Tanzania bara, maana muda wa majaribio kwoa umekwisha.
‘’Kama mamlaka zilikuwa zikitujaribu kwa miaka 57 tokea tujitawale weyewe, sasa wameshatujua uwezo wetu, kilichobakia watupe nafasi hizo ili tuongoze,’’anabainisha.
Riziki Hamad Faki wa Mkoani anasema bado zipo nafasi kama za wakurugenzi, makatibu tawala mkoa, manaibu mawaziri, manaibu makatibu wakuu na hata masheha wanaweza kuongoza.
Anasemakwa usikivu na ahadi ya rais wa awamu ya nane ya Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi ya kuwapa kipaumbele, wanawake bado tama ya kushika maeneo kadhaa kiungozi tunayao,’’anasema.
Mjumbe wa baraza la vijana Chake chake Mwanakhamis Haja Khamis anasema wakati umefika sasa kupewa nafasi za uongozi maana asasi za kiraia kama TAMWA zimeshawawezeshwa.
Anasema kwa vile suala la uongozi kwa mwanamke sio hidaya kutoka kwa mtu mwengine, ndio maana lazima iwe 50 kwa 50 kati yao na kundi la wanaume.
“Hadi sasa kwenye vyombo vya maamuzi bado sisi tuko kidogo, hivyo inakuwa vigumu kutatua changamoto zetu hilo, lakini mwarubaini wa hili ni kupewa nafasi sisi,’’anasema.
Afisa Mipango wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba Siti Habib Mohamed, akizungumza kwenye moja ya mikutano, alisema hakuna katiba, sheria, wala mikataba inayomzuia mwanamke kuwa kiongozi.
“Hivyo mamlaka na tasisi zenye uwezo kuwanzia vyamani na serikali kuu, watupe nafasi za uongozi iwe uwaziri, katib mkuu, wakuu wa wilaya, mikoa, wakurugenzi na wenyeviti wa bodi,’’anasema.
TAMWA WANASEMAJE
Afisa Mawasiliano wa Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA- Zanzibar ofisi ya Pemba Gasper Charles anasema, wanawake sasa wako ‘fit’ kushina nafasi yoyote.
Anabainisha kuwa, baada ya kundi la wanawake kuishi kizani kwa zaidi ya miaka 100, sasa wakati umefika nao kuweka kwenye mwagaza kwa kupewa nafasi ya uongozi.
Anasema, wanawake kama walivyo wanaume hakuna hata mmoja aliyetajwa kwenye Katiba wala sheria na mikataba mbali mbali, juu ya suala la uongozi.
“Kama katiba imetaja sifa za mkuu wa wilaya, mkoa, mbunge, mkurugenzi na nafasi nyingine bila ya kuhusisha jinsi, hivyo hakuna kutengwa kwa wanawake,’’anaeleza.
Anasema walishawawezesha wanawake kushika nafasi ya uongozi tokea miaka ya 2008, kupitia miradi yao kadhaa ukiwemo wa WEZA I, WEZA II na WEZA IIII, pamoja na kuwajengea uwezo kimitaji.
“Sasa wanawake wa Unguja na Pemba, wako tayari kushika nafsi za uongozi, maana wamewiva kitaaluma, wanajiamini hivyo mamlaka ziwakumbuke kiuongozi,’’anasema.
Hata Mkurugenzi wa TAMWA Zanzibar Dk. Mzuri Issa Ali akizungumza kwenye uzinduzi wa muongozi wa mwanamke na uongozi hivi karibuni, alisema bado kiu ya wanawake kushika nafasi ya uongozoi haijazimwa.
“Lakini hatuna budi kumpongeza rais wa Zanzibar wa awamu ya nane Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kuwaona wanawake kuanzia wakuu wa wilaya, mkoa, mawaziri, makatibu wakuu na hata Katibu mkuu kiongozi,’’anasema.
WANAWAKE VIONGOZI
Mkuu wa Mkoa wa kaskazini Pemba Salama Mbarouk, amekuwa akirejea kauli yake, ya mara kwa mara kuwa, wanawake ni viongozi madhubuti na imara wanapopewa nafasi.
Anasema ingawa kwa serikali ya awamu ya nane, imejitahidi kuwakumbuka, lakini bado jitihada za kweli zinahitajika kumpa nafasi mwanamke katika uongozi.
Mwakilishi wa Jimbo la Chambani wilaya ya Mkoani Bahati Khamis Kombo, baada ya kutangaazwa kushika nafasi hiyo, alisema anataka kuuoneshwa ulimwengu kuwa wanawake wanaaminika.
Alisema, kwa miaka mitani iliyopita aliwafanyia mengine na maana wananchi wake, ni miaka mengine mitano ijayo 2020/2025, anatarajia kuitekeleza vyema Ilani ya chama chake.
“Mimi sioni sababu ya kuibua mijadala na vikao visivyo na Mwenyekiti kufikiria sana mamlaka zinapotaka kumpa nafasi ya uongozi mwanamke, kwani kila kundi lipo sawa mbele ya sheria,’’anasema.
Mwakilishi wa Jimbo la Gando Maryam Thani Juma, anasema kama sio hila na baadhi ya wanaume kuanzia kwenye vyama hadi siku ya kupiga kura, na wanawake kupata mwamko tokea zamani kuingia majimboni, sasa mambo yengekuwa mazuri.
Mkuu wa wilaya ya Magharibi ‘A’ Unguja Suzan Peter Kunambi akizungumza kwenye mikutano ya kusikiliza kero za wananchi, alisema anataka kuhakikisha hakuna udhalilishaji wilayani mwake.
“Mkombozi wa wanawake na watoto sasa kaja ndani ya wilaya yenu, ninachohitaji kwenu ni ushirikiano ili kufikia ndoto zangu za uongozi, maana huwa tunaambiwa mwanamke hawezi,’’anasema.
WENGINE WANASEMAJE MWANAMKE KUPEWA UONGOZI
Mwanidishi wa ITV/Redio One Pemba Suleiman Rashid Omar anasema, wana haki kikatiba, na wapo waliofanya vizuri kwenye nafasi zao akiwemo Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, alisema anawaamini sana wanawake katika uongozi, kutokana na ukweli, subra, uvumilivu na uweledi wanapopewa nafasi.
Mwanaharakati wa haki wanawake na watoto Tatu Abdalla Msellem anasema uongozi kwao sio hidaya ni haki yao kikatiba, hivyo hakuna mjadala wa kupewa nafasi hizo.
Msaidizi Katibu ofisi ya Mufti Pemba sheikh Said Ahmad Mohamed, anasema hakuna kizuio kikubwa katika dini suala la kumpa uongozi mwanamke wa kiislamu.
“Kinachoshauriwa tu, iwe kupewa kwake huko huo uongozi, hayapi kisogo majukumu na wajibu wa familia yake akiwemo mume wake kwa aliye kwenye ndoa,’’anasema.
Kijana Khadija Omar Mohamed wa Wawi anasema, kama sheria haikumbagua mwanamke wala mwanamme, hivyo hata suala la uongozi liwe pasu kwa pasu.
Mwanasiasa Juma Ali Khatib ambae kwa sasa ni mjumbe wa baraza la wawakilishi, anasema wanawake ndio nguzo kuu katika familia hivyo, suala la nafasi za uongozi wa kisasa halina shaka kwao.
Mwisho

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

…….SUZA WATOA USHAURI WA ADHABU YA KUNYONGWA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAFUNZI wanaosomea uwalimu Chuo cha taifa cha Zanzibar ‘SUZA’ kampasi ya Benjamin Wiliam Mkapa Wete Pemba, wamependekeza adhabu ya kunyongwa hadi kufa, kwa mtu atakaetiwa hatiani, kwa kosa la dawa za kulevya. Walisema, haiingii akili kuona, mahkama imeshamtia hatiani mtu kwa kukutwa na dawa za kulevya, ambazo huathiri nguvu kazi ya taifa na kisha, kupewa hukumu ya kifungo pekee. Wakizungumza leo Juni 26, 2024 kwenye kongamano la vyuo vikuu, juu ya masuala ya msaada wa kisheria, kuelekea wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar, lililofanyika Chuoni hapo, walisema wakati umefika sasa kutolewa kwa hukumu hiyo. Walipendekeza kuwa, ni vyema kwa mtu anayetiwa hatiani asibakie chuo cha Mafunzo pekee kuitia tena hasara serikali kwa chakula na wakati mwingine matibabu, wakati tayari ameshasababisha madhara, kwa vijana. Mshiriki Juma Nafasi Juma, alifafanua kuwa kama mtu ameamua kuliumiza taifa kwa kuingiza, kusafirisha, kusambaaza dawa za kulevya, hivyo n...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...