NA HAJI NASSOR, PEMBA
MKUU wa mradi jumuishi wa vyombo vya habari kanda ya Afrika kutoka shirika la kuwajengea uwezo waandishi wa habari Jacklie Jidubwi, amesema shirika hilo litaendelea kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili kuwa waledi kwa kuibua maumivu yanayowakumba watu wenye ulemavu chini.
Mkuu huyo wa mradi aliyasema hayo machi 8, mwaka 2022 mjini Zanzibar wakati akiyaghairisha mafunzo ya siku2 kwa wanahabari wa Zanzibar juu ya uandishi bora wa habari za watu wenye ulemavu kupitia mradi wa jumuishi wa vyombo vya habari.
Alisema Internews imevutiwa mno na kazi na mwamko walionao waandishi wa habari wa Tanzania wakiwemo wa Zanzibar kwa kuibua changamoto na madhila yanayowasakili watu wenye ulemavu.
Alieleza kuwa kwa juhudi hizo za wazi wazi ndio maana shirika hilo limevutiwa na kazi hizo na kuahidi kuendelea kufanyakazi na vyombo vya habari.
"Kwa hakika Internews tumevutiwa mno kuona mradi huu unatekelezwa katika nchi kadhaa lakini kwa Tanzania mmezalisha habari 376 kwa kipindi kifupi na baadhi yao kuzaa matunda kwa watu wenye ulemavu," alisema.
Katika hatua nyingine Jacklie amewataka waandishi waliopatiwa mafunzo hayo kuendelea kuyafanyiakazi na sio tu kwa kuandika mabaya pekee kwa kundi la watu wenye ulemavu.
Mkuu wa program kutoka Internews Tanzania Shaaban Maganga alisema moja ya jukumu la lazima kwa mwandishi wa habari ni kuyafikia makundi yote katika utendendaji wa kazi zao.
Alieleza kuwa Internews imeona umuhimu wa kuwaunga nguvu waandishi hao na vyombo vyao ili kujikwamua kwa pale wanapokwa kiutendaji.
"Wapo baadhi yenu wameshapata hata kuungwa mkono kifedha na wengine watapewa ili sasa kufika huko ambako hamfiki katika kuwaandikia watu wenye ulemavu" alifafanua.
Nae mtendaji Temigunga Mahondo alisema ni vyema waandishi wa habari wakazingatia maadili ya kazi zao ili habari na vipindi wanavyofanya visiwaumize watu wenye ulemavu .
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Baraza la taifa la watu wenye ulemavu Zanzibar Mwalimu Ussi Khamis amesema baada kubaini uwepo wa chagamoto wanadhamiria kuifanyia mapitio sheria ya watu wenye ulemavu haki na fura nambari 9 ya mwaka 2006
Alisema kwa mfano vipo vifungu havina maelezo ya kutosha na wala havitaji adhabu ikiwa tasisi ya umma imejenga jengo lisilorafiki kwa wa watu wenye ulemavu.
Mwandishi Rahma Suleiman wa gazeti la Nipashe alisema mafunzo hayo yamemzindua katika kazi zake.
Nae mwandishi wa redio jamii Mkoani Amina Massoud Jabir alisema mafunzo hayo yamemjenga zaidi hasa katika utengenezaji wa vipindi.
Fatma Hamad Faki wa pembayaleo blog na Amour Khamis wa Zanzibar cable walisema wamefanikiwa mno katika kazi zao baada ya kupata mafunzo ya awali.
Awali mafunzo hayo yalifunguliwa na aliyekuwa waziri katika ofisi ya Makamu wa kwanza za wa rais Zanzibar na sasa waziri wa fedha dk. Saada Mkuya Salum.
MWISHO
Comments
Post a Comment