NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@
WATUMISHI wapya wa wizara ya elimu na mafunzo ya
Amali Pemba, wametakiwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya sheria na kanuni za
utumishi wa Umma ili kuongeza uwajibikaji katika utendaji wao.
Kauli
hiyo imetolewa na Mratibu Idara ya uratibu na Utumishi kutoka wizra ya elimu na
mafunzo ya Amali Zanzibar Harith Bakari Ali, wakati akifungua mafunzo ya
kuthibitishwa kazi kwa waajiriwa wapya yaliofanyika katika ukumbi wa Skuli ya
Michakaini Chake chake Pemba.
Alisema
ufanisi wa kazi hutokana na kufuatwa ipasavyo kwa Sheria, miiko na maadili ya
kazi ambayo humtengeneza mtumishi kua muawajibikaji katika utendaji wake wa
kila siku ndani na nje ya eneo la kazi.
"Sheria, maadili,
kanuni na miiko ya kazi ndio kichocheo muhimu cha uwajibikaji kwa
mtumishi wa Umma, hivyo ni muhimu kuyazingatia yote haya ili kufanya kazi zenu
vizuri na si katikamaeneoyakazi tu bali hata nje ya kazi, alieleza.
Alisema
kua kipengele chengine muhimu ni
uzalendo katika kazi, ambayo ni nyenzo
muhimu katika utekelezaji wa majukumu ya msingi ya mfanya kazi, na elimu pekee
si kigezo cha ufanyaji kazi bora wa mtu, bali uzalendo ndio msingi mkuu wa kufikia
uwajibikaji.
Alieleza
kua uzalendo humjenga mtumishi kuwepo kazini mda wote wa kazi pamoja na
kufanya kazi kulingana taratibu zilizopo, jambo
linalochochea upatikanaji wa huduma bora kwa jamii.
Alisema
maendeleo ya elimu nchini yamefikiwa kutokana na uzalendo na uwajibikaji wa
wafanya kazi wa wizara wakiwemo waalimu, ambao wanafanya kazi kubwa katika
kutekeleza majukumu yao ya kila siku katika kuwasimamia vyema wanafunzi wao.
Aidha
alitoa wito kwa watumishi hao kujiepusha na vitendo viovu ikiwemo uvunjifu wa
kanuni na sheria za utumishi wa Umma, kwa kufanyia kazi yale yote waliosomeshwa
ili lengo la utoaji huduma bora kwa jamii liweze kufanikiwa.
"Mafanikio
ya elimu tulionayo Zanzibar yamechochewa
na uzalendo walionao wafanyakazi wa wizara wakiwemo waalimu, hivyo ni muhimu na nyinyi kuyafanyia kazi kwa
vitendo mafunzo haya kwa kujiepusha na uvunjifu wa kanuni na sheria za utumishi
wa Umma", alieleza.
Kwa
upande wake Msaidizi Mkuu wa Chuo Cha Utawala wa Umma IPA tawi la Pemba Nuhu
Abuubakar Ali lengo la kuwepo kwa watumishi wa Umma katika serikali ni
kupambana na kuleta maendeleo endelevu kwa kutatua changamoto zilizomo katika
jamii, hivyo aliwasihi watumishi hao kua ni sehemu ya mapambano hayo.
Aidha
aliwataka watumishi hao watekeleze majukumu yao kama sheria kanuni
zinavyoelekeza bila kujali ubaguzi ili kukuza ustawi wa jamii na taifa kwa
ujumla.
Nae
Afisa elimu kutoka Mamlaka ya kuzuia rushwa na uhujumu uchumi (ZAECA)Mkoa wa
Kusini Pemba Badria Salim Ali aliwataka watumishi hao kutoa huduma kwa misingi
ya haki na usawa pamoja na kujiepusha na vitendo vya rushwa na uhujumu
uchumi, kwani kufanya hivyo ni kosa
kisheria.
Nao
washiriki wa mafunzo hayo walisema mafunzo hayo yanawasaidia katika utendaji
wao wa kazi wa kila siku na kuahidi kufanyia kazi kwa maslahi mapana ya jamii na taifa.
Mafunzo
hayo ya siku mbili yanayoyotewa kwa wafanyakazi wapya wa wizara ya elimu
yameandaliwa na Wizara ya Elimu na mafunzo ya Amali Pemba kwa kushirikiana na
Chuo Cha Utawala wa Umma IPA, ikiwa ni
sehemu ya kuwaongezea uwezo waajiriwa wapya katika kutekeleza majukumu yao ya
kila siku.
MWISHO




Comments
Post a Comment