NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@
MJUMBE wa Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya CCM taifa Majaaliwa Kassim Majaaliwa, amewataka wanachi wa Jimbo la Kiwani, kuwachagua wagombea wote wa CCM kwenye uchaguzi wa mkuu mwaka huu.
Alisema, kama wananchi wanataka maendeleo ya kweli,
wagombea waliopitishwa ndani ya jimbo hilo wanatosha, kufikia maendeleo yao.
Majaaliwa aliyasema hayo leo Septemba 21, 2025, Kwareni Mwambe jimbo
la Kiwani wilaya ya Mkoani, alipokuwa akiwanadi wagombea ubunge, uwakilishi na
madiwani wa jimbo hilo, kuelekea uchaguzi mkuu, mwezi Oktoba mwaka huu.
Alieleza kuwa, tayari CCM imeshandaa mpango kazi wa miaka
mitano ijayo, ambapo ndani yake eneo la Jimbo la Kiwani, limeshaelezwa vya
kutosha.
Alieleza kuwa, huduma zote muhimu ikiwemo maji safi
na salama, afya, barabara na uwezeshaji wananchi kiuchumi, limetajwa ndani ya
mpango huo.
Alieleza kuwa, kila mmoja ajitokeze kupiga kura kwa
amani, ingawa kura zao wahakikishe wanawapigia kura mbunge, mwakilishi wa
madiwani wote wa Jimbo la Kiwani.
Aidha, Majaaliwa, aliwahakikisha wananchi wa Kiwani,
kama ikiwa watawachagua wagombea wote wa Jimbo hilo, wataendelea kushirikiano
nao kwa karibu.
Akimnadi mgombea Ubunge, wa Jimbo hilo Hija Hassan
Hija, alisema ni kinara wa maendeleo, kwa historia yake.
Katika hatua nyingine, Mjumbe huyo wa Kamati kuu ya
hamlashauri kuu ya CCM taifa Majaaliwa Kassim Majaaliwa, ambae pia ni Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Muungaano wa Tanzania, aliwahakikisha ulinzi na usalama wananchi
wote.
Alisema, serikali imeshajipanga kuhakikisha hakuna
uvunjifu wa amani, kuelekea uchaguzi mkuu, hivyo kila mmoja ashiriki bila ya
hofu.
Alieleza kuwa, Tanzania unaoutamaduni wake wa kufanya
shughuli zake kwa amani, kama ilivyo kwa chaguzi zilizopita.
‘’Niwahakikishe wananchi kuwa, ikifika siku ya
kupiga kura Oktoba 29, nendeni kwa kujiamini, maana ulinzi utaimarishwa,’’alifafanua.
Nae Mgombea uwakilishi wa Jimbo hilo Hemed Suleiman
Abdulla, amesema kama wakipata ridhaa, watakuwa watumishi wao na sio mabosi.
Alisema, Kiwani ijayo ndani ya miaka mitano, itakuwa
ya mfano, kama wakipata ridhaa kutoka kwa wananchi hao.
Alieleza kuwa, kila mmoja abakie na chama chake,
ingwa kura zao ikifika Oktoba 29, wahakikishe wanawapigia kura wagombea
wenzake.
Alifafanua kuwa, wanampango wa kuendeleza miundombini
ya elimu, ikiwemo ujenzi wa skuli ya sekondari nyingine, ili kuwapunguzia
mafasa wanaokwenda skuli nyingine.
Alifafanua hayo, anayowaahidi sio utani kwani tayari
wameshafanya utafiti wa kujua, changamoto zao za Jimbo la Kiwani.
‘’Kwa mfano wananchi wa wadi wa Kendwa wayanyohospitali
kwa ajili ya huduma za mama na mtoto, lakini na wale wa Mwambe watajengewa yao,’’alifafanua.
Aliahidi kuwa, kijana yeyote anayetoka jimbo la
Kiwani, kwenda kusoma elimu ya juu, watamfuatilia ili kumsaidia na asome kwa
utulivu.
‘’Tukifanikiwa, kuingia madarakani mimi, Mbunge na
madiwani tutahakikisha tunawafuatilia kihuduma na hatutombagua kijana kwa
sababu ya chama cha wazazi wake,’’alifafanua.
Aidha aliwaomba wagombea wenzake, kuhakikisha
wananadi sera za chama na sio matusi, na kuwataka wananchi wanaofanya kinyume
wawanyime kura wagombea hao.
‘’Sisi tumeshajipanga na kuendelea kunadi sera zilizomo
ndani ya Ilani ya CCM ya mwaka 2025/2030, na sio matusi wala viashiria ya
uvunjifu wa amani,’’alifafanua.
Mapema Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa Hamad Hassan
Chande, alisema sifa zote za kuwa Mwakilishi wa Jimbo la Kiwani, mgombea uwakilishi
huyo anazo.
‘’Maendeleo yaliopatikana katika taifa letu,
yamesimamiwa kwa kiasi kikubwa na Hemed Suleiman Abdulla, hivyo anafaa kwa nafasi
hiyo,’’alifafanua.
Nae mjumbe wa Halmshauri kuu ya CCM taifa Mohamed
Aboud Mohamed, wakati akiwanadi wagombea hao, alisema wana sifa za kuwa viongozi
ya kuwatumikia wananchi.
Alisema, mgombea uwakilishis Hemed Suleiman Abdulla,
akiwa Makamu wa Pili wa rais, amesimia umoja, mshikamano na kufanikiwa
kuwaunganisha wazanzibari.
Alieleza kuwa, Hemed ni hodari wa kazi zake,
mwamifu, mtiifu, machapa kazi na aliyetayari wakati wote kuwatumikia wananchi.
‘’Na ndio maana utekelezaji uliofanikiwa wa Ilani ya
ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025, unaoongozwa na Rais wa Zanzibar, hivyo
Hemed ameshusika kwenye eneo hilo,’’alifafanua.
Kwa upande wa mgombea ubunge wa jimbo hilo, Hija
Hassan Hija, alisema anamfahamu vyema, jinsi alivyokuwa akipigania maslahi ya
wananchi wa Kiwani, hata alipokuwa chama chake cha awali.
Nae kada wa Chama cha Mapinduzi Hamza Hassan Juma,
alisema Mgombea uwakilishi Hemed Suleiman Abdulla, anafaa kushika nafasi hiyo,
baada ya kuonekana utendaji wake kwa nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.
‘’Kwa hakika Mgombea uwakilishi wa Jimbo la Kiwani,
hakuna mbadala maana ni mpenda maendeleo na asiyependa majungu, katika kazi,’’alifafanua.
Kada wa chama hicho Machano Othman Said, alisema Mgombea
ubunge wa jimbo hilo la Kiwani Hija Hassan Hija, amekuwa king’ang’anizi mkubwa
kwa jambo lenye maslahi.
Alisema, anakumbuka vyema wakati akifanya nae kazi,
katika baraza la Wawakilishi, ambapo alikuwa hapindishi maneno, kwenye jambo
lenye maslahi ya umma.
Mabunge mstaafu wa Jimbo la Kiwani Rashid
Abdalla Rashid na Mwakilishi Mussa Foum Mussa, wamesema wananchi wa Kiwani
wanayosababu ya kuwachagua wagombea wa
chama hicho kwa makubwa waliyofanya.
Walisema, mgombea uwakilishi Hemed Suleiman Abdulla,
ndie aliyemshauri Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi, jimbo hilo kuwa
huduma zote za kibinaadamu.

Walisema wanalo tenki la kuhifadhia maji safi na
salama lenye ujazo wa lita milioni 1, vituo vya afya vyenye hadi ya huduma za
juu pamoja na ujenzi wa skuli tatu za ghorofa.
‘’Kwa mfano katika skuli hizo tatu za ghorofa, zimesababisha
kuwepo wa vyumba 103 vya kusomea na kuondoa mikondo mitatu, kwa wanafunzi,’’alifafanua.
mwisho
Comments
Post a Comment