NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
MGOMBEA Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dk. Hussein
Ali Mwinyi, amesema kuelekea uchaguzi mkuu wa vyama vingi, Oktoba mwaka huu,
suala la kuhubiri amani na utulivu liwe ndio ajenda.
Mgombea
huyo wa urais aliyasema hayo jana, uwanja wa mpira wa Makombeni wilaya ya
Mkoani Pemba, kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni kwa chama hicho, kuelekea
uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu.
Alisema,
haiwezekana kutekeleza jambo lolote pasi na kuhubiri amani na utulivu, maana
ndio msingi wa kila jambo.
Alieleza
kuwa, kama kuna mtu anadhani hilo sio jambo la msingi, sio vyema kuungwa mkono,
kwani hakuna jambo ambalo linaweza kutekelezeka pasi na amani na utulivu.
‘’Kwanza
niwambie kuwa tutaendelea, kuhubiri amani, mshikamano na umoja maa andio msingi
mkuu wa kila kitu,’’alifafanua.
Aidha,
Dk. Mwinyi alisema anakusudia kuwa Zanzibar kusiweko na skuli hata moja, ambayo
wanafunzi wanaingia mikondo miwili, bali ni mkondo mmoja, ili wapate muda kwa
kwenda madrassa.
Alisema,
tayari hilo kwa mkoa wa kusini Unguja, limeshafanikiwa na kutamani kwa miaka
mitano ijayo, iwe ni kwa Zanzibar nzima.
‘’Suala
la mikondo miwili sitaki kulisikia, maana wanafunzi wamekuwa wakipata
changamoto ya kuhudhuria madrasaa, ambapo miaka mitano ijayo hilo litafondoka,’’alisema.
Katika
hatua nyingine Mgombea huyo wa urais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi,
alisema anakusudia kuendelea kuifungua Pemba, kwa ujenzi wa barabara wa Chake
chake-Mkoani itakayokuwa na njia nne.
Alisema,
hakuna haja kwa wananchi wanapotaka kusafiri, kutoka mji mmoja kwenda mwingine,
kutumia muda mrefu jambo, ambalo ambalo ni kupoteza muda wa uzalishaji.
Alisema,
hakuna shaka kuwa muda mfupi ujao, hakutakuwa na barabara ya ndani ya Pemba,
ambayo haitokuwa ya kiwango cha lami.
‘’Ili
kuimarisha maisha ya wananchi, yapo mingi hutakiwa kufanywa, ikiwemo
miundombinu ya usafiri wa anga, nchi kavu na baharini,’’alisema.
Aidha
Dk. Mwinyi ambae ni Rais wa Zanzibar, aliwataka wananchi kuwapuuza wanaodai
kuwa, serikali ya awamu ya nane haijafanya jambo, kwani wana ajenda yao
binfasi.
Kuhusu
ajira 300,000 alizoziahidia kwa miaka mitano iliyopita, alisema walifanikiwa kuzipata
217,500, ingawa kwa awamu ya nyingine ijayo, itakuwa ndio kipaumbele chake.
‘’Vijana
msiwe na wasi wasi, nikipata ridhaa ya kuiongoza nchi, suala la ajira na
kupanda kwa gharama za maisha, itakuwa ndio kipaumbele changu cha kwanza,’’alisisitiza.
Kuhusu,
namna ambavyo atapambana na gharama za maisha, alisema kwa kuanzia, ni ujenzi
wa matenki ya mafuta katika eneo la Wesha kwa Pemba na Mangwapwani kwa Unguja.
‘’Hiawezekani,
mafuta yakiadimika siku moja, iwe ni changamoto kwa wananchi, tutakuwa na matenki
ya kuhifadhia mafuta pamoja na maghala ya kuhifadhia chakula,’’alisema.
Wakati
huo huo Mgombea huyo wa urais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi, alisema zao
la karafuu linaendelea kuwanufaisha wakulima, kwa kupata asilimia 80, baada ya serikali
kuliuza.
‘’Bado
zao la karafuu tunaendelea kulienzi, na miaka mitano ijayo, litaendelea kunusuriwa
kwa kuwepo la umwagiliaji na mikopo kwa wakulima,’’alifafanua.
Kuhusu
mashamba ya mikarafuu, ambayo yalikua ya eka, sasa serikali imeshatangaaza,
kuwapatia hati maalum ambazo zitakuwa na uwezo wa kuyarithi.
Kada
wa chama cha mapinduzi Khamis Hamza Chilo, aliwataka wanaccm, kuachana na sera
za maji taka, zinazotolewa na baadhi ya wagombea.
Alisema,
wapo baadhi yao, wanapitapita, na kuwaeleza wananchi, kwamba serikali ya awamu ya
nane haijafanya maendeleo, jambo ambalo sio sahihi.
‘’Kwa
mfano ukifika hospitali ya Mkoani, unaona nyumba za kisasa 74 za madaktari, achia
mbali upanuzi wa bandari, na ujenzi wa barabara za ndani kwa kiwango cha lami,’’alisema.
Mapema
Katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM Zanzibar Khamis Mbeto Khamis, alisema kama
kuna mtu analamikia kuwa serikali iliyopo madarakani sio halali, alishindwaje kukata
rufaa.
Mapema
Naibu Katibu mkuu wa CCM Zanzibar, Dimwa aliwaombea kura wabunge, wawakilishi
na madiwani wa CCM, waliomo wilaya ya Mkoani.
Alisema,
wagombea wote walioteuliwa na vikao vya juu vya chama, wanazosifa za utumishi
na kuwaletea maendeleo wananchi.
‘’Niwaombee
kura wagombea wote kuanzia, mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dk. Samia Suluhu Hassan, na mwenzake wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi, maana
ukiichagua CCM, umechagua maendeleo,’’alisisitiza.
Kwa
upande wake mgombea ubunge wa jimbo la Mkoani Prof: Makame Mnyaa Mbarawa, alimuahidi
Dk. Mwinyi kumpa kumpa kura za ndio, kwa maendeleo ndani ya Mkoani.
Alisema
tayari meli 24 kubwa zimeshafunga nanga bandarini hapo, pamoja na kushusha makontena
1,214 yenye bidhaa mbali mbali, tokea bandari hiyo ilipopanuliwa.
Aidha
alisema, sababu nyingine wananachi kuwapa kura ni kutokana na ujenzi wa banda maalum,
la kukaa abiria 1000 kwa wakati mmoja, ambapo ujenzi wake, unaendelea kwa kasi.
Jingine
alisema ni ujenzi wa barabara ya Mbuguwani- Tironi, yenye urefu kilomita 3, na
shilingi bilioni 6.31 zinaendelea kutumika, kwa ajili ya ujenzi wa barabara
hiyo.
‘’Kwa
hakika Dk. Mwinyi umetufanyia mingi ndani ya Jimbo la Mkoani, maana na sasa
ujenzi wa barabara ya Mkoani- Chake chake, utaanza wakati wowote, hongera sana
kwa hili,’’alifafanua.
Nae
Mgombea Uwakilishi wa Jimbio hilo, Khamis Hijazi, alisema tayari Dk. Mwinyi
anaendelea na ujenzi wa soko la kisasa eneo la Mbuyuni, jambo ambalo, lilikuwa
changamoto hapo awali.
Hivyo,
amewakumbusha wananchi wa wilaya ya Mkoani, kutomnyima kura Dk. Mwinyi, ili
aendeleze maendeleo anayoyakusudia.
Mgombea
ubunge wa Jimbo la Kiwani Hija Hassan Hija, alimuahidi Dk. Mwinyi, asiwe na
wasi wasi, kura za wananchi wa jimbo hilo, ni zake.
Hivyo
aliwaomba wananchi wa Zanzibar, kuwachagua wagombea wote wa CCM, kwani wana
uchu wa maendeleo.
Nae
mgombea uwakilishi wa jimbo hilo Hemed Suleiman Abdulla, amewataka wanaccm
kuwajibu wapinzani, kwa kuwapigia kura, wagombea wote wa CCM.
‘’Haipendezi
kuona mwanaccm, anaingia kwenye malumbano yanayoashiria uvunjifu wa amani, bali
wajibuni kwa kisanduku cha kura,’’alifafanua.
Mapema
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa kusini Pemba Yussuf Ali Juma, alisema kwa kuvuuka lengo
la utekelezaji Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025, ushindi wake utakuwa mapema mwaka
huu .
Mwisho
Comments
Post a Comment