NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
KAMATI ya maadili na taaluma ya shehia za Wambaa na Chumbageni wilaya ya Mkoani Pemba, imepiga marufuku kufanyika vitendo viovu, vinavyofanywa na baadhi ya vijana, katika ya fukwe ya bandari ya Kwakitunga Wambaa.
Kamati hiyo imesema, wamebaini kuwa, kila ifikapo siku za sikukuu na mwishoni mwa wiki, wapo vijana, wengi wao kutoka nje ya shehia hizo, huitumia fukwe hiyo, kwa kufanya mambo machafu.
Akizungumza kwenye kongamano la malezi na maadili, lililofanyika Wambaa sokoni, Mjumbe wa kamati hiyo sheikhe Mahamoud Hussein, alisema hawakatai vijana kusherehekea sikukuu, bali wanachopiga marufuku ni uvunjifu wa maadili.
Alisema, suala la furaha ni jambo jema, baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhan, ingawa wanachokipinga ni kufanyikwa vitendo vya udhalilishaji.
Alieleza kuwa, uislamu haukatazi furaha kwa mtu yeyote, bali kinachotakiwa iwe ni kwa kufuata maadili na misingi ya dini ya kiislamu, ili furaha hiyo isigeuke nakama.
āāKamati ya maadili na taaluma, inapiga marufuku kwa vijana wanaozitumia vibaya neema za bahari na fukwe, kwani athari inapojitokeza humkubwa kila mmoja,āāalifafanua.
Katika hatua nyingine, aliwataka wazazi la walezi kuwaelimisha watoto wao, juu ya nidhamu nzuri za kusherehekea sikukuu, ili isigeuke adhabu.
Nae sheikh Hassan Khamis Othman, aliwataka waumini wa dini ya kiislamu, kushrikiana katika kudhibiti vitendo viovu katika fukweli hiyo, kwani athari yake inaweza kuwakumba walio wengi.
āāSualala la kuwaelimisha wenzetu juu ya matumizi sahihi na fukwe, sio la kamati ya maadili na taaluma pekee, bali kila mmoja kwa nafasi yake, anaowajibu huo,āāalifafanua.
Hata hivyo amewataka wazazi na walezi wa shehia jirani za Wambaa na Chumbageni, kuwazuia watoto wao kutoitumia vibaya neema ya ujio wa sikukuu.
Kwa upande wake ustadhi Mohamed Juma, amewakumbusha wananchi wa shehia za Wambaa na Chumbageni, kushirikiana katika kudhibiti vitendo viovu, hasa vinavyofanywa katika fukwe za Kwakitunga shehia ya Wambaa.
Baadhi ya wananchi wa shehia za Wambaa na Chumbageni, walisema ipo haja ya kuungana na kamati yao ya maadili na taaluma, ili kudhibi vitendo vya udhalilishaji.
Hivi karibuni akizungumza kwenye mashindani ya tano ya qur-an yaliofanyika Chumbageni, Mkuu wa wilaya Mkoani Dk. Hamad Omar Bakari, amewakumbusha waumini wa dini ya kiislamu, kuwa kila mmoja anawajibu wa kuzuia machafu katika jamii.
Hata hivyo, alisema yuko tayari kushirikiana na wananchi wa shehia za Wambaa na Chumbageni, katika kudhibiti vitendo viouvu kwa vijana.
Hata hivyo aliwataka wazazi na walezi, kuwabidiisha watoto wao, katika kukifuata kwa vitendo kitabu cha Muumba, ambacho kimetoa njia ya maisha yasiokuwa na shaka.
..mwishoā¦
Comments
Post a Comment