NA AMRAT KOMBO, ZANZIBAR @@@@
Wapo wanawake ambao wanao uwezo mkubwa wa kuwa viongozi, lakini baadhi ya mitazamo katika jamii inawarudisha nyuma na kuamua kukaa pembeni.
Kwa bahati
mbaya mitazamo hii, inahusishwa na
maelekezo ya dini kutokana na tafsiri potofu inayotolewa na badhi ya watu juu
ya maelekezo ya dini na kuonekana kwa kiasi fulani.
Hata utekelezaji wa mikataba ya kikanda na
kimataifa juu ya haki na nafasi za wanawake, ikiwa pamoja na katika uongozi,
ambayo nchi yetu imeiridhia inatekelezwa kwa kuchechemea au kufumbiwa macho kwa
visingizio mbali mbali.
Miongoni mwa
mikataba inayohimiza kulindwa kwa haki za wanawake ni tamko la kimataifa kuhusu
haki za binadamu la 1948 ambao umelenga kutokomeza aina zote za kuwabagua wanawake.
Kifungu cha
pili cha Mkataba wa Afrika juu ya haki za binadamu,inajumuisha kanuni
yakutobagua kwa misingi ya rangi, kabila ,jinsia ,lugha,dini,siasa au maoni
mengine yoyote.
Zanzibar
inayo idadi kubwa ya waumini wa dini ya Kiislamu (zaidi ya asilimia 95),ambao
mwenendo wa maisha yao unaongozwa na melekezo ya dini yao na kila kukicha
viongozi wake wa dini ya Kiislamu huikanusha mitazamo ya watu wanaokataa
mwanamke kuwa kiongozi.
Miongoni mwa
maelezo yanayotolewa kuonyesha dini ya Kislamu haikatazi mwanamke kuongoza ni
nafasi walizopewa wanawake kuogoza katika enzi za mitume,ikiwa pamoja na wakati
wa vita.
Mwanazuoni
maarufu wa masuala ya dini ya Kiislamu, Profesa Issa Haji Zidi wa Zanzibar,
amekuwa akisisitiza mara kwa mara kwamba dini ya kiislamu haijakataza kuwepo
kwa kiongozi mwanamke, isipokuwa mwanamke anatakiwa kufuata,sheria na taratibu
na Kiiislamu juu ya mwanamke awe na mwenendo gani wa kimaisha ndani na nje ya
nyumba yake.
Alisema katika enzi za Mtume Muhammad (S .A.W )
mwanamke alikuwa kiongozi katika vita na mambo mengine na kote aliweza kuifanya
kazi hio kwa uweledi na uadilifu.
Mchungaji wa
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Shukuru Malonda, alisema
mwanamke ana nafasi mbalimbali za
uwongozi, ikiwemo ndani ya kanisa na
kijamii.
Alitoa mfano
wa viongozi wa kike waliongoza na kuwasimamia watu katika dini ya Kikirsto na
kutaja kwamba miongoni mwao Esta, ambae
alikuwa Malkia na Debora ( kiongozi na
hakimu wa wana wa Israeli) alikuwa nabii.
Anasema
katika kanisa hilo wamewapatia nafasi sawa wanawake na wanaume ya kuongoza
kanisa, ikiwemo nafasi ya wachungaji na nafasi ya wainjilist.
"Katika
kanisa letu, tumewachaguwa wanawake wawili na wanaume wanne ambao ni
wachungaji, pamoja na wainjilist 12 ikiwa wanawake watano na wanaume saba, wote
kazi yao moja ya kuongoza kanisa,"alisema.
Licha ya
serikali kusimamia maendeleo ya wanawake, lakini taasisi zisizoza
kiserikali wanaume na wanawake wanapata
nafasi sawa za uongozi na hapana tatizo lolote.
Mratibu wa
kuinua wanawake katika uongozi katika
Chama cha Waandishi wa Habari Wanwawe (TAMWA ZANZIBAR), Maryam Ame,alisema haielewi dini inayokataza mwanamke kuwa
kiongozi,ispokuwa jambo muhimu ni kuwa na uwezo na kuimudu nafasi hio.
"Tunatoa
elimu kwa wanawake ambao wanahitaji kuwa viongozi ili wajitambue na kutatua
changamoto zinazowakabili, vikiwemo vikwazo vya kusingizia dini,"
aleieleza.
Mapka hivi
karibuni wanawake 172, wamepatiwa mafunzo ya uongozi Unguja na Pemba na
kuwashauri wanaotaka kuingia kwenye uongozi wasiwe na hofu kwani katiba
inawahakikishia haki hio ambayo inasisitizwa katika mkataba mbali mbali ambayo
nchi yetu meiridhia.
Pamoja na
hamasa za serikali, asasi za kiraia na
viongozi wa dini, lakini mwanasiasa Hamisa Mmnanga alisema bado ipo haja ya
wakati wa uchaguzi kuwepo na utaratibu
bora utaowapa nafasi waliokuwa mahodari,
shupavu na jasiri kuwania nafasi hizo.
Diwani wa
zamani wa Bububu, Amina Ali Mohamed, alisema mitazamo ya kidini inayoshadidiwa
na baadhi ya watu imesababisha kuwepo mizozo na mara nyengine wanawake
kudharauliana.
"Baadhi
ya wananchi bado wapo nyuma katika kuhakikisha mwanamke anapewa nafasi ya
uongozi, iwe wa kijamii, kiuchumi au siasa," aliongeza.
Aliwataka
wanamke wenye nia ya kuoongoza kutosisikiliza maneno ya watu wenye mitazamo
isiokuwa na tija na badala yake waendelee kufanya kazi kwa bidi ili
kuwahakikishia wananchi kuwa mwanamke anaweza kuongoza.
Faki Ali ambae ni mkaazi wa meline
nne,alisema ni kweli baadhi ya watu
wanawakwamisha wanawake wasitake kuwa viongozi kutokana na kuwepo na mtazamo
hasi ya kidini.
Zaliha salum ambae ni kijana aliewahi kutaka
kuingia katika siasa lakini hofu ya dini yake imemsababishia kuachana na nafkra hizo.
Diwani wa Jitimai
Mwanakwerekwe Unguja, Asha Hassan
alisema ameingia katika nafasi za uwongozi kwasababu anaamini dini yake ya
Kiislamu inaruhusu mwanamke kuongoza, ijapokuwa baadhi ya masheikh wanarudisha
nyuma maendeleo ya wanawake.
Aliwataka
wanawake wenziwe kutokata tama na waendele kutekeleza ibada ya Mungu,huku
wakiwa wanaendelea kupambana katika harakati za kuwa kiongozi.
Kwa ujumla
yapo mabadiliko Zanzibar juu ya nafasi ya mwanamke katika uongizi, lakini bado
panahitajika elimu na juhudi ili mwanamke wa Visiwani ajione hanyimwi haki ya
kuongoza na anashirikiana na wanaume katika kuiletea jamii maenedeleo yenye
maisha mazuri, raha na furaha.
MWISHO
Comments
Post a Comment