NA AMRAT KOMBO, ZANZIBAR@@@@
SIKU zote baadhi ya watu wanaimani ya kuwa,
mwanamke bado ni mama wa nyumbani pekee.
Ambae anatakiwa kuchunga familia yake tu peke
yake, lakini bila ya kufikiri kuwa mwanamke anaweza kufanya mambo makubwa ya
kuwasaidia jamii na kuleta maendeleo katika nchi.
Ushahidi wa hili, sasa usiangalia tena Marekani na
kwengineko, njoo kwa Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania, alivokuwa jasiri
na mchapa kazi, katika nafasi yake ya uwongozi.
Hivyo inaonesha kuwa, mwanamke sio mdhaifu kama
watu wanavoona, hebu tuangalie baadhi ya viongozi mwanamke wanavyowajibika
katika nafasi zao.
Fatma Rashid
Juma ni diwani wa Chukwani Unguja, anasema
kabla ya kushika nafasi hiyo, alikuwa mfanya biashara mjasiria mali mdogo, huku akiwa mwanancha wa
chama cha mapinduzi CCM.
Anasema katika mwaka 2020, alijishirikisha katika
kugombea udiwani wakiwa na wagombea wenzake 11, wakiwa wanawake watatu na
wanaume nane, na kubahatika kutokea mshindi kwenye kinyanganyiro hicho kwa
kupata kura 49 katika watu 100.
Sababu iliyopelekea kuingia katika siasa, anasema
zipo nyingi ingawa moja ni kutetea haki za wanyonge, kuweza kupaza sauti zao.
Licha ya hayo anasema uongozi hauna umri kila mtu anahaki ya kusimamia na
kutetea, na hasa akishafikia ule umri wa kuanza kupiga kura.
Diwani Fatma amefanya mambo mbali mbali ambayo
yameweza kuwasaidia wananchi wake, ikiwemo kutengeneza barabara ya kijiji cha Shakani
na ya Chukwani, kutengenezea banda la wajasiria mali 20 katika
skuli ya Chukwani, lenye gharama ya shiling 5,700,000
na kwasasa anapambana kutengeneza kituo cha
daladala cha Chukwani.
Sambamba na hayo anatarajia kutengeneza kisima
katika wadi ya Chukwani na Buyu, ili kuona wananchi wake wanaendelea kuugawa
muda wao katika kazi nyingine.
Vikwanzo ambavyo amepitia wakati alipopata nafasi
ya uwongozi ikiwemo baadhi ya wagombea wenzake kuwepo kwa matabaka, lakini
alifanikiwa kukabiliana na vikwazo hivyo kwa kuamua kujishusha chini na kuanza
kuwasikiliza maoni yao.
" Wakati nilipopata hii nafasi, nikapelekea
kupata changamoto ya wagombea wenzangu, kuweka matabaka pamoja na maneno yasio
kwisha, ingawa niliamua kupambana na changamoto hiyo na kufanikiwa,’’anasema.
WANAOMFAHAMU DIWANI FATMA
Sheha wa Chukwani
Suleiman Mohamed Mwinyi, anasema kuna umuhimu wa kuwepo viongozi wanawake kama
Diwani Fatma, kwani wanakuwa na ushawishi mkubwa katika uwongozi wao.
" Haswa wanapopewa mafunzo, huwa mstari wa
mbele katika kufahamu mambo mengi, wanakuwa waaminifu katika uwongozi wao kama
alivyo Diwani wetu,’’anaeleza.
Anaona viongozi walio wengi wanawake, wamekuwa watetezi
wakubwa katika shughuli mbali mbali, ikiwemo katika sekta ya kupiga vita vitendo vya ukali na
udhalilishaji.
Sambamba na hayo alisema katika shehia yao wametoa
viongozi mbalimbali wanawake kwa lengo la kuwajengea uwezo na kusimamia
maendeleo ya shehia hiyo.
"Katika shehia yetu, tunao viongozi wanawake,
kwa mfano tumewahi kuwa na mbunge mwanamke, diwani mwanamke hadi kufikia
mwenyekiti wa halimashauri wa wilaya, na akanzisha vikundi tofauti vya maendeleo,’’anasifia.
"Kwasasa
tuna mkuu wa wilaya mwanamke ambae ni
mchakarikaji, mshumpavu, na mwenye
kuvumilia kero za wananchi, pamoja na kutatua changamoto zetu, akishirikiana
na Diwani Fatma,’’analeza.
Licha ya
yote hayo alisema diwani Fatma amefanya jitihada mbalimbali za kimaendeleo,
ikiwemo kuhamasisha masuala ya afya, kiuchumi pamoja na kufanya ubunifu wa
kueka banda la ujasiria mali kwa lengo la kuweza kujikwamua na umaskini.
Mwananchi Aziza Ali, anasema wamepata kiongozi
imara mwenye utu, ambae anasidia kutatua changamoto zinazowakabili kwenye wadi
yao.
Nae Hamadi Makame, anasema wamepata kiongozi
anaewajibika katika majukumu yake, na ataendelea kumuunga mkono, ili aweze
kufanya kazi kwa wepesi.
Asha Hassan Juma ambae ni Diwani
ya Jitimai Mwanakwerekwe, anasema kabla ya kugombea
nafasi ya udiwani, alikuwa anafasi mbalimbali, ikiwemo mjumbe wa sheha, Mwenyekiti
wa umoja wa wanawake tanzania (UWT)
katika tawi na kuamua kugombea nafasi ya diwani tangu 2015 .
"Nimegombea udiwani katika awamu mbili, tangu
mwaka 2015 hadi 2020, na nikagombea tena 2020, hivyo uwongozi huu natumikia
hadi 2025," anasema.
Wengi wao wanasema msemo unaosema mwanamke bila ya
kuwezeshwa anaweza, ni sahihi kutokana na mapambano na jitihada wanazozifanya
mwanamke katika kuhakikisha analeta maendeleo katika uwongozi wake.
Mkurugezi wa Jumuiya ya wanasheria wanawake (ZAFELA)
Jamila Mahmoud, anasema wanatoa elimu ya kuhamasisha wanawake katika kugombea
nafasi mbali mbali za uongozi.
Anasema, kwani wanawake ilionekana wapo kidogo
mno, kwenye nafasi kuanzia udiwani, uwakilishi, ubunge, na hata kwenye nafasi
za uteuzi kama za uwaziri, katibu mkuu, mkuu wa wilaya, usheha pamoja na
wakurugenzi.
Sambamba hayo anasema kuna umuhimu wa kuwepo
sheria ambazo zinatoa nafasi, mfano watu walivopendekeza kuwepo kwa 50 kwa 50
kwa hiyo itasaidia wanawake kupata nafasi nyingi za uongozi.
"Mwanamke anapotaka kusimama katika kugombea jimboni, anaweza kupata vitisho, kutengenezewa
kashfa, pamoja na kuamini tamaduni kuwa
mwanamke hafai kuwa kiongozi, hizi huwavunja moyo,’’anaeleza.
Mratibu wa kuinua wanawake katika uongozi kutoka
chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA Zanzibar), Maryam Ame,
anasema wanatoa elimu mbalimbali, kwa wanawake ambao wanahitaji kuwa kiongozi,
ili wajitambue na kutatua changamoto za kiuongozi.
"Na hii inawapa hamasa na kuweza kutambua
haki zao za kidemokrasia, siasa, mil ana utamaduni ikiwemo haki ya kupata
elimu, afya pamoja na miundombinu,’’anasema.
Maryam anasema hadi sasa zaidi ya wanawake 172
wamepatiwa mafunzo ya uwongozi kutoka Unguja na Pemba, pamoja na kutambua
vikwazo na namna ya kukabiliana navyo.
Aidha aliwanasihi wanawake wanaotaka kuingia
kwenye uongozi kutokuwa na hofu, kama Katiba inavyosema katika serikali zote
mbili inavyoelezea pamoja na mikataba mbalimbali ya kitaifa na kikanda.
Mkurugezi wa Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Thabit
Idarous Faina, anasema hali halisi ya viongozi wanawake Zanzibar, kupitia
nafasi ya uwakilishi kwenye majimbo 50, ya Zanzibar wanawake ni wanane pekee.
Anasema wabunge wanaowakilisha Zanzibar wanawake
ni wanne tu sawa na asilimia nane, huku mawaziri wakiwa sita sawa na asilimia
33 na makatibu wakuu ni saba sawa na asilimia 39.
Kwa upande wa wakuu wa mikoa, mwanamke ni moja tu
sawa na asilimia 20,wakuu wa wilaya ni wanane sawa na asilimia 36 na masheha
wanawake ni 68 sawa na asilimia 17 kwa masheha wote ambao ni 389.
Sambamba na hayo anasema miongoni mwa vikwanzo vya
wanawake kutoingia kwenye uwongozi, ikiwemo majukwaa ya kisiasa yanatajwa kuwa
ni moja wapo ya vikwanzo vinavyosababisha wanawake wasifikie malengo yao.
Mwisho
Comments
Post a Comment