Mkurugenzi wa Idara ya
Uendeshaji na Utumishi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na
Watoto Dkt. Salum Khamis Rashid amewataka maafisa ustawi kusimamia vyema kesi
za udhalilishwa na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia ili kuendelea kuimarisha
hali ya ustawi nchini.
Amesema hayo jana wakati
akifungua kungamano la maafisa ustawi kutoka wizara mbali mbali hapa nchini lilifanyika
katiak ukumbi wa Sebleni Unguja ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha siku ya ustawi.
Amesema dhamira ya serikali
ni kuondoa kabisa vitendo vya udhalilishaji na ukatili hivyo maafisa Ustawi wakifanya kazi kwa uweledi wa
hali juu na kuondoa muhali katika kusimamia kesi hizo vitendo hivyo vinaweza
kutokomezwa kabisa.
Aidha amesema kuendelea
kuachiwa na kuoneanaaibu na muhali kunapelekea kuongezeka kwa mmomonyoko wa
madili katika jamii na kuzoeleka vitendo hivyo kuwa vya kawaida.
Nao maafisa wa ustawi
wameiomba serikali kutoa mafunzo zaidi kwa wanaume kwani wao ndio wahusika
wakuu wa vitendo hivyo katika jamii.
Pia wamesema maafisa ustawi wanadharauliwa wakati
wanaposimamia majukumu yako hivyo waiomba idara ya ustawi kuwapati utambulisho
ili kuthaminika na kuaminika wakati wa wakiendelea na majukumu ya.
Pia wamesema endapo
mitaala ya skuli itaanzishwa na kuwekwa somo rasmi la udhalilisha na vitengo
ukati ili kuongeza wigo zaidinchinj.
Akifunga kungamano
hilo mratib wa Idara ya Ustawi Lahdad
Haji Chum amesema kitengo cha ustawi kinakabiliwa na changamoto
nyingi ikiwemo ukiukwaji wa sheria kwa wale wanaofanya viyendo vya ukatili na
kuwachia huru bila ya kuchukuli hatua za kisheri.
Nae mhadhiri wa kungamano
hilo kutoka chuo cha kikuu cha SUZA amesema kuachana kwa wzazi au migogoro
katika famili kunachangia watoto wengi kupata matatizo ya kudhalilisha na
kufanyiwa vitendo vya ukatili.
Comments
Post a Comment