NA SHAIB KIFAYA, PEMBA@@@@
MAAFISA
habari Kisiwani Pemba, wametakiwa kuwa wabunifu zaidi kutokana na kukuwa kwa teknologia ya habari, ili
kuifikishia jamii taarifa sahihi, kwa maendeleo ya taifa .
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar
Hassan Khatib Hassan, alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili, kwa maafisa
habari, uhusino wa Wizara na tasisi za serikali na waandishi wa habari,
uliofanyika Gombani Chake chake.
Alisema licha ya kuwa na ukosefu mdogo wa utendaji na vitendea
kazi, bado kuna umuhimu wa kupambana na kuisaidia jamii, juu ya kupata taarifa
bora na za uhakika.
Alifahamisha, kwa sasa taarifa nyingi zisizokuwa sahihi zitawa katika
mitando ya kijamii, hivyo ni vyema kwa maafisa hao na vyombo vya vijana wengi
wasiokuwa na taaluma kuwa wepesi na
haraka kuilezea jamii juu ya usahihi na taarifa husika.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mtendaji Idara ya Program, Tume ya Taifa
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ‘UNESCO’Aboud Iddi Khamis, alisema lengo ya
mafunzo hayo, ni kuwajengea uwezo maafisa habari wa taasisi za Serikali
kufahamu majukumu yao.
Aidha alifahamisha kuwa, maafisa hao ni wasaidizi wa wananchi, kwa
kuwasemea kero zao ambazo zinazopaswa kufanyiwa kazi, na taa sisi husika
kutokna na jambo linalolalamikiwa.
Nae Mkufunzi wa mafunzo hayo Imane Duwe alisema, mwandishi ni mtu
muhimu wa tasisi, hivyo ni lazima kuhakikisha kuwa karibu na vyomba vya habari.
Alieleza kuwa, hilo ni kuhakikisha kazi zake zinafanyika kwa
wakati na haraka kwa kuu habarisha umma kwa jambo lilofanyika.
Sambamba na hayo, alisema ni lazima mwandishi kuangalia mipaka ya
utaji taarifa, ambazo zitaweza kuhatarisha usalama wa nchi, ili kuepusha
taharuki inayoweza kutokea katika nchi.
Mkuu wa Mawasiliano na habari kutoka Tume ya Taifa UNESCO Christina
Musaroche alisema, ipo haja ya kuwandaa
mpango maalum kwa maafisa habari wa Wizara, kuwapatia mafunzo ya kuwakumbusha
wajibu wao.
Alifahamisha kuwa, kwani bado wako nyuma kiutendaji ili kufikia
mbele na kuwaboresha kazi zao, ambazo pia wananchi wanazisubiri kwa ajili ya
kujua yanayofanywa na serikali.
‘’Tume ta taifa ya UNESCO ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
itaendelea kukutana na maafisa habari na wale wa uhusiano, ili kuwambusha
wajibu katika taasisi zao,’’alieleza.
Hata hivyo alieleza kuwa, ipo haja sasa kwa mafunzo mengine,
kuwakutanisha wakuu wa taasisi za serikali na maafisa hao, ili kujua changamoto
na namna ya kuzitatua.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo, walisema bado baadhi ya wakuu
wa taasisi hawajui umuhimu wa kuwepo kwa maafisa wa habari katika taasisi zao.
Mwisho
Comments
Post a Comment