Na Najjat Omar ā Unguja.
Chama cha Waandishi wa Habari wanawake Zanzibar āTAMWA, wamewakutanisha wadau mbalimbali katika kujadili masuala ya ukuaji wa teknolojia kwenye dhana ya kupunguza vitendo vya udhalilishaji.
Majadiliano hayo yalifanyika katika ukumbi wa Raha Leo ulipo kisiwani Unguja kwa
kuwakutanisha wadau wa masuala ya kijamii kama viongozi wa kisiasa,walimu,wanafunzi,
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wanawake TAMWA āZanzibar Asha Abdi amesema licha ya ukuaji wa teknolojia kurahisisha masuala ya ujifunzaji kwa watoto ila kwa upande mwengine unachochea udhalilishaji wa watoto kuiga hata kufanya na kujifunza mambo mabaya.
āUkuwaji wa teknolojia umekuwa mkubwa ambapo nao una changamoto zake ,watoto wanajifunza mambo huko kwenye mitandao na kujaribu kwa kufanya sasa hii teknolojia pia inachochea sana masuala ya udhalilishaji kwa watoto kama jamii tunatakiwa tujitahidi sana kuwalinda watoto na masuala haya kwa kuwa makini.ā Amesema Asha Abdi wakati akifungua majadiliano hayo.
Akiwasilisha hoja Mkufunzi kutoka Chuo kikuu cha Zanzibar ā SUZA Daktari Sikujua Omar amesema simu janja zimekuwa na msaada mkubwa kwa watoto kwenye ujifunzaji ila watoto pia wanapitia masuala ya udhalilishaji kwenye matumizi ya simu hizo ikiwemo kurusha au kurushiwa picha chafu.
āWengi wenu hapa mnatumia simu janja na mnajua hasa kutumia mambo mbalimbali kwenye mitandao ila muangalie pia suala la kujilinda na udhalilishaji nyinyi wenyewe kama watoto kwa sababu ulinzi unaanza na wewe kwanzaā Amemalizia kusema Daktari Sikujua.
Baadhi ya viongozi wa majukwaa ya vijana kutoka Shehia mbali mbali wamesema suala la udhalilishaji na teknolojia ni jambo ambalo linatakiwa kuangalia na familia pale inapotoa fursa ya kijana wao kutumia simu.
Talhiya Juma ni Mwenyekiti wa Baraza la Watoto shehia ya Kama amesema kuwa suala la wahanga wa udhalilishaji kufichwa au hata kutumia simu kuwatangaza au kuwarekodi bado linawaathiri watoto hivyo jamii iliangalie hili kwa umakini.
āSi vibaya sisi vijana kutumia simu ila hata watu wazima unaotumia simu kuwaposti watoto wao au pale vitendo vinapotokea vinazidisha sana suala la udhalilishaji kwa watotoā Amesema Talhiya.
Viongozi wa dini wanasababu lukuki za kuielemisha jamii kuhusu kupingana na masuala ya udhalilishaji kwa jamii hususan kuwasaidia wazazi kutambua athari za teknolojia kwa watoto.
Mchungaji wa Kanisa la KKKT Lidya Isaya amesema suala la udhalilishaji limechukua sura mpya kwa sababu ya ukuaji wa teknolojia kwenye ulimwengu hivyo kila mmoja aawajibu wa kuwaelimisha watoto juu ya matumizi sahihi ya simu.
āTunaona picha za utupu zinatumwa kwenye mitano na nyengine ni za watoto wadogo,kisha zinasambwaza huo pia ni udhalilishaji maana ikitokea hio itamuathiri zaidi mtoto hivyo jukumu la kuwalinda watoto ni la jamii mzimaā Amesema Lidya wakati wa majadiliano hayo.
Sophia Ngalaphi ni Afisa Mawasiliano kutoka TAMWA,amesema suala la udhalilishaji kwa watoto ni kilio kikubwa kwa jamii ila sasa linajihusisha moja kwa moja na matumizi mabaya ya mtandao.āWadau ambao wamekuja hapo wanakaa na jamii hivyo jukumu la kuwalinda watoto na matumizi mabaya ya teknolojia ni la mzazi,mtoto mwenyewe na jamii kwa ujumlaā Amesema Sophia.
Zaidi ya wenyeviti wa mabaraza ya watoto 50 ,viongozi wa dini,wawakilishi wa taasisi mbalimbali walikutana kwa pamoja kujadiliana kwa pamoja njia nzuri ya matumizi ya teknolojia kwa watoto ikiwa kama ni maadhimisho ya mtoto wa Afrika yaliyobebe kaulimbiu ya āMatumizi sahihi ya kidigitali kwa ustawi bora wa mtotoā.
Comments
Post a Comment