NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
SHEHA wa shehia ya Wawi wilaya ya
Chake chake Sharifa Wazir Abdalla, amewataka wananchi kuendelea kuziripoti kesi
za udhalilishaji katika vyombo husika, na kutojihusisha na vikao vya kuzifanyia
sulhu.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi, alisema kisheria kesi za udhalilishaji na za jinai
kwa ujumla, hutakiwa kuripotiwa moja kwa moja, katika vyombo vya sheria.
Alisema, ni
kosa kwa jamii kuitisha vikao vya sulhu, kwani husababisha kuwapa nguvu
wadhalilishaji, kwa vile wanakosa hukumu.
Sheha huyo
alieleza kuwa, kuwaripoti katika vyombo vya sheria, kutochechea makosa hayo
kupungua katika jamii, ambayo huwaathiri wanawake na watoto.
‘’Kila mmoja
awe mlinzi kwa mwenzake, na asikubali kushiriki katika vikao vya sulhu, iwe kwa
ajili ya kuchukua fedha ama kumkimbiza mtuhumiwa,’’alieleza.
Katika hatua
nyingine, sheha huyo wa shehia ya Wawi Sharifa Waziri Abdalla, alisema
wataendelea kutoa elimu kwa jamii, juu ya madhara ya matendo hayo.
‘’Sisi
kupitia shehia yetu, tumekuwa tukiwatumia wasaidizi wa sheria, askari wa shehia
na kamati yangu ya maadili kutoa elimu kila kijiji, ili wananchi wapate
uwelewa,’’alieleza.
Kwa upande
wake, Katibu wa sheha wa shehia hiyo Shem Haroub Said, alisema bado jamii
imekuwa ikiendeleza kuzifanyia sulhu, kesi hizo.
Alisema,
pamoja na elimu wanayoitoa, lakini wapo baadhi wamekuwa wakipuuzia hilo, na
kusababisha watoto wa kike kukosa haki zao.
‘’Elimu
tumekuwa tukiitoa kila muda, juu ya athari ya matendo hayo hasa kuyafanyia
sulhu, kwani watoto wanaweza kukosa haki zao,’’alifafanua.
Nae Mratibu
wa wanawake na watoto shehiani humo, Fatma Kassim Mohamed, aliziomba mamlaka ya
vyombo vya sheria, kutozifumbia macho kesi za aina hiyo.
‘’Wakati
mwengine, mtoto anapelekwa mbele ya vyombo vya sheria ameshaharibiwa, ingawa
mwisho anaambiwa ushahidi haujakamilika,’’alilalamika.
Mama mmoja
ambae mtoto wake ameshabakwa mara mbili, ameziomba mmalaka, kumkamata kijana
aliyetajwa na mtoto wake, kuwa ndio muhusika wa tukio hilo.
‘’Pamoja na
kuripoti tukio hilo kwa vyombo husika, lakini bado muhsika anaendelea na
shughuli zake kama kawaida, jambo ambalo linatuumiza sisi familia,’’alieleza.
Nae mwananchi
Khamis Haji Seif, alisema bado baadhi ya wananchi wenzao, wamekuwa wakizifanyia
sulhu kesi hizo, na wakati mwengine kusababisha kuzorotesha kesi hizo.
Hivi
karibuni akifungua mafunzo ya siku 10 kwa wananchi wa Wawi juu ya kuzitambua
sheria mbali mbali, Afisa Mdhamini wizara ya nchi, afisi, rais, Katiba, sheria
na utawala bora Halim Khamis Ali, aliutaka uongozi wa shehia ya hiyo, kuendelea
kushirikiana, ili kuondoa majanga hayo.
Mkurugenzi
wa Juamuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake ‘CHAPO’ Nassor Bilali
Ali, amesema moja ya njia ya kuondoa matendo hayo, ni jamii kushirikiana kwa
karibu na vyombo husika.
Mwisho.
Comments
Post a Comment