NA BAKAR MUSSA, PEMBA:: MARCH 2020 Tanzania, iligundua kesi ya mwanzo ya ugonjwa Corona baada ya dunia kugubikwa na janga kubwa la uwepo wa gonjwa huo, 'UVICO19' ambalo ulianza mwezi disemba 2019 nchini China. Licha ya Zanzibar kupoteza roho za watu wake kadhaa, lakini pia kwa kiasi fulani, iliathirika kiuchumi, ijapo kwa asilimia ndogo kutokana na watalii kutoingia kwa kasi kama ilivyozoeleka. Ikumbuke kuwa, ugonjwa huo unaelezwa unasambaa kwa kasi kutokana na kuwepo kwa makaazi ya watu karibu (msongomano) na hivyo kuwepo na hadhari ya kutokukaa karibu na kuvaa Mask (Barkoa). Kwa vile ugonjwa huo ulitawala dunia nzima, ni wazi kulitokea mtikisiko wa uchumi, ingawa waswahili husema ‘Mwenyeezi Mungu akikupa kilema hukupa na mwendo’. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ilipata mkopo wa fedha kutoka Umoja wa Mataifa, baada ya kuonekana nchi nyingi kukumbwa na ukosefu mkubwa rasilimali fedha za kujiletea maendeleo kutokana na kuwepo ugonjwa huo. Zanzibar...