NA HAJI
NASSOR, PEMBA@@@@
KATIBU
Mkuu wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar Mattar Zahor Massoud,
alisema changamoto zinazowakabili wafanyakazi wa wizara hiyo Pemba, zitatatuliwa
hatua kwa hatua, ili wafanye kazi kwenye mazingira rafiki.
Alisema, anayaelewa
vyema mazingira wa tumishi walioko Pemba kwa kule kukaa kwa muda mrefu, akiwa
kwenye nyadhifa tofauti, hivyo wizara itahakikisha inazitatua changamoto hizo.
Katibu Mkuu
huyo, aliyasema hayo hivi karibuni, wakati akijitambulisha kwake na kuzungumza
na watumishi hao, na kusema anachoomba ni umoja na mshikamano miongoni mwao.
Alieleza
kuwa, baada ya kukutana na waratibu alielezwa changamoto kadhaa, ikiwemo suala
la usafiri, kutoshirikishwa baadhi ya waratibu hasa uandaaji wa bajeti kuu, na
kuahidi kuyafanyia kazi.
Alisema,
suala la usafiri wa vyombo vya maringi mawili, wizara yenyewe itanunua kwa aina
ya vipaumbele vyake, ili kuhakikisha zile Idara zinazohitaji, zinafanikiwa.
‘’Kwa upande
wa vyombo vya maringi mawili hivi, wizara yetu itajitutumua na kununua taratibu,
kila bajeti inapokuwepo, maana naelewa changamoto hizo,’’alifafanua.
Akizungumzia
usafiri wa vyombo vya maringi manne, alisema tayari yapo mazungumzo na wenzao
wa wizara ya Fedha, ili kuona wanawapatia usafiri huo.
‘’Unajua
wenzetu wa wizara wa Fedha ni wasikivu, ikiwa utawaendea na maelezo mazuri
yenye mchanganuo, twarajia kufanikiwa katika hili,’’alifafanua.
Kuhusu umoja
na mshikamano, aliwakumbusha watumishi hao kujenga tabia ya kushirikiana katika
kazi zao, ili kuwapa nafasi pana wananchi, wanapohitaji huduma.
‘’Isiwezekane
ndani ya wizara moja, kunataasisi inahitaji vifaa ili kufanikisha, lakini
isiazimwe na idara nyingine, jambo hilo ni baya na lisiwepo,’’alieleza.
Akizungumzia
namna ya watendaji hao kuongeza elimu, aliitaka Idara ya Utumishi, kuwa na
mpango madhubuti na endelevu, ambao utawahakikisha wafanyakazi wanasoma.
Alifafanua
kuwa, kwenye kutafuta elimu hakuna kikomo wa umri, bali ikiwa kunamfanyakazi
anataka kujisomea, ashauriane na Idara ya Utumishi na kukamilisha, ndoto yake.
‘’Niwahimize
watendaji wa wizara hii, kujiandalia mazingira rafiki ya kuongeza elimu, tena
sio tu kwa ajili ya kuongeza mshahara, bali kuongeza ujuzi wa kazi,’’alisema.
Mapema Afisa
Mdhamini wa wizara hiyo Pemba, Mfamau Lali Mfamau, aliwasisitiza wafanyakazi,
kufika na kurudi kazi kwa wakati, ili kutoa huduma bora kwa wananchi.
Alieleza
kuwa, wapo baadhi ya wafanyakazi wamekuwa na tabia ya kuchelewa kazini na kuondoka
kabla ya wakati, jambo linalotoa tafsiri mbaya, kwa jamii.
Wakati huo
huo Ofisa Mdhamini huyo, aliwakumbusha wafanyakazi hao, wanapokuwa na
changamoto za kiofisi kufuata ngazi moja baada ya nyingine, ili kulalamika.
Wafanyakazi
hao, wameahidi kuyafanyiakazi, walioelezwa, kwani yanatoa viashirio vya
utendaji kazi bora kwao.
Mwisho
Comments
Post a Comment