WANACHAMA 25 kutoka vikundi 16 vya kuweka na kukopa katika Wilaya ya Kusini Unguja wamepatiwa mafunzo ya siku mbili ya kuchagua, kupanga na kusimamia biashara.
Mafunzo hayo yalitolewa chini
ya Programu ya Mashirikiano ya pamoja
kwa ajili ya haki za Watu wenye Ulemavu
(CADiR) inayotekelezwa na Chama cha waandishi wa Habari wanawake Tanzania,
Zanzibar (TAMWA ZNZ), Shirikisho la Jumuiya za Watu wenye Ulemavu Zanzibar
(SHIJUWAZA) na Jumuiya ya wasioona Zanzibar (ZANAB) kwa ushirikiano mkubwa na
Shirika la Watu Wenye Ulemavu la Norway (NAD).
Amapo jumla ya washiriki 16 wa mafunzo hayo ni watu wenyeulemavu na 9 ni walezi na
wasimamizi wa Watoto wenyeulemavu,
ambapi wanatarajiwa
kuyafikisha maarifa haya kwa wanachama wenzao, ili kila kikundi kinufaike pamoja na kuimarisha biashara zake.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo,Aziza
Ismail ambae ni Mratibu wa program ya CADiR kutoka NAD, alisema taasisi zinazoshirikiana katika
programu hii zina matumaini makubwa kuwa mafunzo haya yatawawezesha wawakilishi
wa vikundi kupeleka elimu waliyoipata kwa wenzao,ili
kusaidia wanachama wote kuchagua biashara bora na zenye tija.
“Kwa vile miongoni mwa malengo
makuu ya program hii ni kuwawezesha watu wenyeulemavu kuinuka kiuchumi na kupata kipato rasmi,
tunaamini mafunzo haya yatasaidia kikamilifu kulifikialengo hili”, alisisitiza Mratibuhuyo.
Mkufunzi
wamafunzo hayo, Muhidini Ramadhan kutoka TAMWA ZNZ alisema, hali
ya umasikini inaweza kupungua kwa watu wenye ulemavu iwapo wataelimishwa juu ya
ujuzi na miradi ya kiuchumi yenye tija.
Nae
Meneja wa Programu kutoka TAMWA ZNZ Nairat Ali, aliongeza
kua mafunzo
haya ni muhimu kwa ajili ya kuwasaidia wanachama kupanga na kuchagua biashara
zenye tija ili vikundi viwe endelevu na viweze kujitegemea kiuchumi.
Kwa
upande wake ndugu Khamis Ali, Afisa Program kutoka ZANAB, amewataka washiriki wa
mafunzo hayo kujifunza kwa umakini mafunzo hayo ili waweze kuchagua biashara
sahihi zitakazowawezesha kupata mikopo na kuweza kurudisha kwa wakati.
Washiriki walijadili na kuandika mipango ya biashara,
baadhi wakieleza ndoto zao za kukuza biashara ndogo ndogo walizo nazo, ikiwemo kilimo,
ufugaji, kufungua maduka na ushonaji.
Akizungumza kwaniaba ya washiriki wenzake,
Yusra Ali Hassan ambaye ni Msaidizi Katibu wa kikundi cha "Mtu ni Utu"cha Kajengwa, ame wapongeza waandaaji wamafunzo hayo na kusema kwamba, yamewapa muongozo
mzuri wa namna ya kupanga biashara na kutumia vizuri fedha katika kukuza
biashara zao.
“Kupitia
mafunzo haya tumejifunza kupanga matumizi kwa uangalifu na kuweka mipango
thabiti ya biashara, binafsi
nimeona namna biashara ya ushonaji inavyoweza kukua zaidi nikiwa na maarifa
haya mapya,” amesema Yusra.
Mafunzo
hayo ya siku mbili yamefanyika katika ukumbi wa walimu Kitogani, ikiwa ni sehemu ya utekelezajiwa
program ya CADiR katika eneo la uwezeshaji kiuchumi,
ambalo linalenga kuanzisha na kuimarisha vikundi vya watu wenye ulemavu vya kuweka na kukopa katika wilaya
11 za Unguja na Pemba.
MWISHO
Comments
Post a Comment