NA KHAULAT SULEIMAN ,PEMBA
WAZIRI wa Kilimo Mali Asili na Mifugo Zanzibar Shamata Shaame Khamis amesema Wizara imeandaa maonyesho nane nane kwa dhamira ya kuimarisha kilimo kwa dhana za kisasa pamoja na kuimarisha kilimo hai kwa manufaa ya bidha katika jamii ili kutoa fursa kwa tasisi za kiserikali na hata binafsi na wajasirimali na wananchi wote kwa ujumla.
Serikali kupitia wizara ya kilimo mali asili na mifugo imekamilisha matayarisho yote ikiwa lengo ni kuhamasisha wakulima kutumia njia bunifu za kilimo cha kisasa na kuongeza uzalishaji na mbinu bora za kisasa katika kukuza pato la taifa kwa ujumla.
Aliyasema hayo kwa wandishi wa habari huko katika ofisi za Wizara ya Kilimo Wete Jodari mkoa wa kaskazini Pemba wakati wa ghafla ya ufunguzi wa maonyesho ya kilimo ya nane nane ambayo yanafanyika Dole Kizimbani wilaya ya Magharibi A Unguja.
Wizara ya Kilimo Mali asili na Mifugo inaendeleza mipango na mikakati iliyoanzishwa na serekali katika kuendeleza sekta ya kilimo ili kuona nchi imepunguza utegemezi wa mahitaji ya chakula na kuendeleza kilimo cha biashara katika uzalishaji wa chakula na kuwawezesha vijana katika kilimo cha umwagiliaji
"Jitihada zinaendelea kuimarisha kilimo cha umwagiliaji na uzalishaji ikiwemo viungo na uzalishaji wa nazi na karafu kwa lengo la kuhifadhi rasilimali zetu zilizopo kupitia maonyesho hayo zipo fursa mbali mbali ,wananchi watakapo tembelea katika maonyesho hayo watapata kujua mbinu za kisasa za ulimaji na uzalishaji,"alieleza.
Serikali ya mapinduzi ya zanzibar imeendelea kujitahidi sana kuhakikisha vilio vya wakulima wa zanzibar vimeondoka kutokana na uwepo wa huduma za pembejeo za kilimo,mbolea pamoja na mbegu na dawa za kulia magugu zimepatikana kwa wakati na mavuno yote kwa wakati katika uzalishaji kwa mwaka huu yameongezeka tani 1.5 kwenye zao la mpunga kwa hekta 1.
"Jitihada hizo zimeendelea kuweka utulivu juu ya serikali yao kwa rais wa zanzibar kwa kuwaondoshea changamoto zilizokuwa zikiwakabili kwa mda mrefu kwa kuzipatia maji"alifafanua.
Mapema Afisa Mkuu idara ya kilimo na uhakika wa chakula Pemba Asha Omar Fakih aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika maonyesho hayo kwa lengo la kujipatia ujuzi na ufanisi katika uzalishaji wa bidha zao mbali mbali za kilimo kwa njia za kisasa zaidi
Maonyesho hayo ya kilimo nane nane ni tisa kuendelea kufanyika zanzibar kila ifikapo mwezi wa 8 ambayo ni siku ya wakulima ambayo hufanyika viwanja vya Dole Kizimbani wilaya ya Magharibi A Unguja kwa lengo la kuimarisha kilimo na dhana za kisasa yenye kauli mbinu isemayo kilimo na utajiri tunza amani kukuza ubunifu.
MWISHO.
Comments
Post a Comment