Na Mwandishi Wetu@@@@
Kuelekea wiki ya Mwananchi, Mashariki wa klabu ya Yanga wa Kijiji cha Buma kilichopo Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wamejitokeza kutoa misaada mbalimbali ya kijamii ikiwamo madawati.
Mashabiki hao walikabidhi madawati hayo katika shule ya Msingi Buma iliyopo kijijini hapo ikiwa ni mwendelezo wa kutoa misaada kwa jamii kuelekea siku ya Mwananchi inayotarajiwa kufanyika Agosti 4 Mwaka huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa maarufu 'Lupaso'.
Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mwenyekiti wa Klabu hiyo Tawi la Buma Ismail Omary amesema kuwa, wanachama wamekua na utaratibu wa kutoa misaada mbalimbali kwa jamii, lengo ni kurudisha hisani kwa wananchi wanaowazunguka kutokana na mwendelezo mzuri wa timu yao.
" Leo tumejitokeza kwenye viwanja vya shule ya msingi Buma lengo ni kutoa msaada wa madawati ili wanafunzi waweze kuyatumia wakati wa masomo, huu ni utaratibu wetu wa kurudisha fadhira kwa wananchi kutokana na hamasa tunqzozipata za timu yetu kuchukua makombe.
" Tumechukua kombe la klabu Bingwa na hivi karibuni tumechukua kombe la Toyota kutoka Afrika ya Kusini, kama mashabiki tunaona fahari kuishabikia timu yetu na kuwaunga mkono wachezaji ili waweze kufanya vizuri zaidi," amesema Omary.
Ameongeza kuwa, wanaona fahari kuona maboresho ya usajili yaliyofanywa na mwekezaji wa timu hiyo msimu huu Ili waweze kuwa na kikosi Bora ambacho kitatoa ushindani mkubwa mara baada ya msimu kuanza, jambo ambalo litawasaidia kuendelea kufanya vizuri Katika mechi zijjazo.
Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Shule ya Msingi Buma, Hawa Namalenga amewashukuru mashabiki wa timu hiyo na kuwaomba wadau wengine kujitokeza kutoa msaada kwa ajili ya wanafunzi.
" Tunawashukuru mashabiki wa timu ya Yanga kutupatia madawati haya kwa sababu yatawasaidia wanafunzi kukaa bila ya changamoto yoyote na kusoma katika mazingira salama," amesema Namalenga.
Ameongeza kuwa, ili kuhakikisha watoto wanafanya vizuri kwenye mitihani yao, wanapaswa kusoma katika mazingira mazuri na salama, jambo ambalo litasaidia kuongeza ufaulu.
Mwisho
Comments
Post a Comment