NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
SHAHIDI nambari 14 kwenye kesi ya
mauwaji, ambae ni Daktari wa hospitali ya Vitongoji Chake chake Pemba Ali Juma
Ali, amedai mahakamani kuwa, baada ya uchunguzi alibaini kuwa, mjeruhiwa
alishambuliwa kwa vitu vyenye cha kali na silaha mfano wa marungu.
Alidai
kuwa, wakati akiwa kazini kwake hospitalini hapo, Septemba 21, mwaka 2021,
alimpokea mjeruhumiwa Suleiman Said Saleh (55) akiwa katika hali mbaya.
Shahidi
huyo akiongozwa na Wakili wa serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka
Ali Amour Makame, mbele ya Jaji wa mahakama kuu Zanzibar Ibrahim Mzee Ibrahimu,
alidai kuwa uchunguuzi ukabini kuwa kina cha jeraha la kichwani ni nchi nne kwa
upana na urefu nchi mbili.
Alidai
kuwa, jeraha jingine ambalo lilikuwa bega la mkono wa kushoto, lilikuwa na nchi
tatu kwa urefu na kina cha kwenda chini likuwa nchi mbili.
Akiendelea
kuongozwa na Wakili wake, shahidi huyo alidai kuwa, wakati anamfanyia
uchunguuzi, alibaini pia mkoja wake wakati ukitoka ulikuwa umechanganyika na
damu na huku mjeruhiwa kabla ya kufariki alikuwa akililia maumivu.
‘’Kwa
kushirikiana na wataalamu wenzangu, pamoja na majeraha ambayo marehemu yalikuwa
yakionekana wazi wazi, pia uchunguuzi tukabaini alikuwa na mititigiko ambayo
yanaashirikia alishambuliwa na vitu bapa,’’alidai.
Aidha
shahidi huyo nambari 14, alidai vitu kitaalamu vinaweza kuwa mithili ya marungu
ya miti, ambayo yalionesha dhahiri alipigwa na watu.
‘’Hata
wakati tunamuhoji mjeruhiwa huyo, pamoja na ndugu na jamaa zake waliomleta,
walidai kuwa alishambuliwa na watu kadhaa na kusababisha kuvuja damu na kulia
maumivu,’’alidai.
Katika
hatua nyingine shahidi huyo ambae ni daktari, aliimbia mahakama hiyo kuu kuwa,
baada ya siku mbili na kumuona mgojwa wao hali imezidi kuwa mbaya, walimpatia
rufaa kwenda hospitali nyingine kwa matibabu.
‘’Ni
kweli tulimpokea mjeruhiwa akiwa katika hali mbaya mno, na siku mbili baadae
kutokana na ukosfu wa baadhi vya vifaa, tulilazimika kumpa rufaa,’’alidai.
Mara
baada ya shahidi huyo kumaliza kutoa ushahidi wake na kuiwasilisha fomu maalum
ya matibabu kutoka kituo cha Polisi ‘PF3’mahakamani, Jaji Ibrahim Mzee
Ibrahimu, aliupa nafasi upande wa utetezi, ili kuulizwa maswali.
Wakili msomi wa watuhumiwa hao wanne, akiwemo mwanamke mmoja, Zahran Mohamed Yussf, alitaka kujua ikiwa mgonjwa aliyempokea alikua na jalada ‘file’ lake na kujua alikuwa nambari ngapi.
Aidha
wakili huyo alitaka kujua ikiwa Daktari huyo hakumfanyia uchunguuzi yeye peke
yake, ingawa alidai kuwa alifanya na wenzake kwa amri yake.
Wakili
huyo pia alitaka kujua, ikiwa bado hadi sasa Daktari huyo anawakumbuka ndugu na
jamaa waliomlete mjeruhiwa huyo, siku alipokuwa kazini na kudai hawakumbuki
tena.
‘’Nini
nani aliyekwambia kuwa, majeraha aliyokuwa nayo mgonjwa uliyempokea, yalitokana
na ugomvi wa ndugu na jamaa zake, kama ambavyo uliieleza mahakama,’’alihoji
Wakili huyo.
Mara
baada ya kumalizika kwa ushahidi huo na maswali ya kinzani kwa pande zote,
Mwanasheria wa serikali Ali Amour Makame, aliimbia mahakama kuu kuwa,
wamebakisha na mashahidi wawili.
‘Mheshimiwa
Jaji, kwa sasa bado mashahidi wawili akiwemo Askari mpelelezi, na hivyo
tukimaliziana na hao wawili, itakuwa tumekamilisha mashahidi wetu 16, na
tunaweza kufunga ushahidi,’’alidai.
Hivyo
aliiomba mahakama hiyo, kuliahirisha shauri hilo na kulipangia tarehe nyingine,
kwa ajili ya kujakuendelea kuwasikiliza mashahidi waliobakia.
Jaji
Ibrahim, aliuuliza upande wa utetezi, ikiwa umekubaliana na ombi la upande wa
mashataka, na kupitia wakili wa watuhumiwa hao Zahran Mohamed Yussuf,
ulikubali.
Hivyo
Jaji huyo nae, alikubaliana na mawazo ya pande zote mbili, na kulipangia shauri
hilo, kurudi tena Febuari 20, mwakani, huku watuhumiwa wakiendelea na dhamana
zao.
Watuhumiwa
wanaodai kuumua Suleiman Said Saleh (55) wa Vitongoji ni Said Nassor Khalfan
(60), Khadija Said Saleh (52), Nassor Said Nassor (29) na Mohamed Said Nassor
(23) wote wakaazi wa Vitongoji.
Mwisho
Comments
Post a Comment