IJAPOKUWA kuanzia serikali za wilaya, mkoa hadi taifa zimeshapiga marufuku kwa wanawake, watoto na watu wengine kuacha kabisa kuokotoa karafuu zinazoanguka “ mpeta ” lakini bado wengine wanaendelea kupuuzia agizo hilo . Wapo wanaoendelea kuokota mpeta wakiwa na watoto wao, ingawa sababu za kuokota mpeta wenyewe huwa wanazo na pengine ukizisikiliza zinaweza kuingia akilini. Maana wengine husema kama ni vitendo vya udhalilishaji, basi vipo hata kabla ya ujio wa zao hili la karafuu, na ndio maana wanadai kuwa anaetaka kudhalilishwa hata kama hakuna karafuu. Lakini kubwa na lililonileta mbele yenu leo hii na kuutumia ukurasa huu, ni kuwauliza hawa wanaokwenda kuokota mpeta wakiwa wamejipamba wana ajenda gani huko? Maana utashangaa wakati ukipishana nao au kama utabahatika kupanda gari moja nao, jinsi walivyojipura kama sio kujiremba. Kiutamaduni kila mmoja anaekwenda kazini hukoga na kujipura jinsi awezavyo, ingawa kila ina mazingira yake, lakini sio kuokota mpeta na kujipambana mbon