NA HAJI NASSOR, PEMBA RAIS wa Baraza la Habari Tanzania MCT, Jaji Mstaafu Bernad Luanda, amewataka wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa wanachama wa baraza hilo, kutoa michango yao ya kina, ili kupata katiba mpya, ya baraza hilo. Aliyasema hayo leo Januari 8, 2026 wakati akifungua mkutano mkuu huo, kwa njia ya kielektroniki ya ‘ZOOM’, uliowanganisha wanachama kadhaa hai. Alisema MCT inawategemea mno wanachama hao, katika kulipeleka mbele baraza hilo, na kwa kuanzia ni lazima, kuwa na katiba inayokwenda na wakati. ‘’Niwaombe sana wanachama nyinyi hai wa MCT, leo kutoa maoni yenu, ambayo naamini, yatakuwa ndio dira ya kupata katiba mpya,’’alifafanua. Katika hatua nyingine, Rais huyo wa MCT aliwatakia kheir ya mwaka mpya wanachama wake wote, na kuwataka kuutumia vyema, katika kufanikisha malengo yao. Akiwasilisha uchakataji wa maoni kuelekea katiba mpya ya MCT, mjumbe wa sekretariet Mwanzo Lawrence Milinga, alisema moja ni kutaka kuipa hadhi ya kipekee ofisi ya MCT iliyo...