ASHA ABDALLA, PEMBA @@@@
WAKULIMA wa Mbogamboga na Matunda wameshauriwa kusindika Matunda na kuusarifu Mchicha lishe ili kuimarisha Afya na kujiongezea kipato katika soko na kuweza kuimarisha uchumi wa nchi .
Ushauri huo ulitolewa na Warld vegetable centre kwa kushirikiana na ZEA chini ya mradi wa AID-I unaofadhiliwa na USAID, wakati walipokua wakipewa Mafunzo ya nadharia na vitendo ,huko Pujini katika kiwanda cha usindikaji wilaya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba.
Mradi huo ulisema unalengo la kuhakikisha wanatoa Elimu kwa wakulima wadogowadogo kupitia katika mashambani mwao na darasani ili waweze kujua namana gani wanaweza kuusarifu mchicha lishe na kusindika matunda ili kuboresha na kuongeza thamani ya mazao ya siweze kupotea.
Munira Rashid khamis ambae nimsimamizi wa masuala ya lishe na afya kutoka katika Mradi wa Warld vegetable centre aliesema kuwa ipo haja kubwa kwa wakulima wa mbogamboga na matunda kupata uwelewa zaidi juu ya upotevu wa mazao na mbogamboga baada ya mavuno kua ni ukosefu wa Masoko ,miundombinu ya vitendea kazi, Majokofu ya asili ya kuhifadhia na vyungu vya udongo.
"Wakulima tunapovuna mboga zetu na matunda tujitahidi kuzifanyia maboresho ya kuzihifadhi katika sehemu salama ili yaweze kukaa kwa muda mrefu bila ya kuharibika na kupoteza thamani ya zao hilo" alifafanua.
Aidha alifafanua kuwa mbegu za mchicha lishe nimuhumi sana kuzisarifu kwa kuzichanganya na nafaka nyengine, zikiwemo mtama ,choroko,mbegu za mboga, kwa ajili ya kutengeneza unga wenye virutubisho sahihi vyenye
kujenga mwili na kuwapa watoto kuanzia6, wajawazito, na watuwazima pamoja na wagonjwa .
Hatahivyo aliwaomba wakulima hao kupitia Mafunzo hayo ya kusindika unga wa mchicha lishe na kusarifu mazao waliopewa wende wakawe walimu kwa kwa kuwafundisha wakulima wenzao ili Elimu hiyo ipate kuzidi kuendelea nakuimarika zaid Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
"Mradi wetu wa Warld vegetable centre kwa kushirikiana na ZEA tunalengo la kuwawezesha wakulima kwa kuwapa hii Teknolojia ya kisasa kwenye huu usindikaji wa Mchicha lishe pamoja na Mazao mengine zikiwemo tungule kwakutengeza Tomato past na viungo ili Wajasiriamali kuweza kukuwa kimaendeleo zaidi" alifafanua.
Kwaupande wake Muezeshaji food technolojikalis ambae ni Meneja Kituo cha kuleya na kukuza Wajasiriamali Zanzibar Ahmed Nasour Masoud aliwapa Elimu wakulima hao wanapovuna mazao yao wayafanyie usindikaji kwa yale ambayo yanahitaji kusindikwa ili mkulima apate kujiongezea kipato na kuongeza bidhaa kuwa bora na kuondoa upotevu wa Mazao.
" Tunapo weza kusindika mazao yetu ambayo yaliharibika kama tungule kuifanyia Tomato past au Nyanya paket au kusindika kwakuanika tukapata unga wa tungule tukatumia kwamatumizi mengine tuna weza kupunguza upotevu wa Mazao nakuweza kujiongezea soko na kupata kipato kizur." Alifafanua.
Hata hivyo aliwashauri wakulima hao kuandaa mazingira safi na salama wakati wanapotaka kufanya usindikaji na kuweka vifungashio ambavyo vinaweza kuendana na muda uliopo mfumo wa utamaduni na ukuwaji wa Teknolojia ya kisasa na pia kurahisisha kulinda bidhaa isiharibike kwa haraka.
Nae Nadra Suleiman Haji kutoka katika mradi wa Warld vegetable centre alisema kua mradi huu ni wa miaka miwili na madhumuni makubwa katika Mafunzo hayo nikufikia Wajasiriamali 120 katika vikundi kumi na mbili ambavyo wataweza kuunda viwanda tofauti kwa wale ambao wamepatiwa Mafunzo na kuwafundisha wengine .
Aidha alieleza kuwa Mradi huu kwa kushirikiana na ZEA kupitia mafunzo haya yaliotolewa kuhusiana na mchicha lishe hayataishia hapa bali yataendelea kwa usindikaji wa tungule, usindakaji wa viungo tofauti na kuviimarisha viwanda kwa kuwapatia vitendea kazi Wajasiriamali hao.
Hatahivyo aliwaomba wajasiriamali wayachukuwe Mafunzo hayo waliopewa nakwenda kuyafanyia kazi ,kwani hiyo nifursa pekee kwa akina mama ambayo itawasaidia kukuza bidhaa zao ambazo watazalisha hapa nakuondokana kutumia bidhaa zinazozalishwa nchi nyengine.
Nae Kaumu mkuu wa Idara ya Mafunzo na miradi ya uwezeshaji kutoka Wakala wa uwezeshaji Wananchi kiuchumi ZEA Ali MohamedAli amewaomaba wajasiriamali hao kuyachukuwa mafunzo hayo kwa umakini na iwe nimuendelezo mzuri kwawe gine ambao wanatamani kua wajasiriamali na kuzalisha bizaa kama hizo za kusindika unga wa mchicha lishe ambao una virutubisho na mazao ili kujipatia kipato kikubwa kwenye soko .
Nae Afisa Maendeleo ya kilimo Wilaya ya Mkoani Said Ali Hassan alisema kuwa Mradi wa Warld vegetable centre ni msaada mkubwa katika kisiwa cha Pemba kwa kupewa hii taaluma kwa wakulima hivyo aliwaomba wakulima hao wayatumie vizuri mafunzo waliopewa kwavitendo ili kulifikia lile lengo ambalo lilikusudiwa katika kuboresha bidhaa zenye ubora .
Nao baadhi ya washiriki wa Mafunzo hayo Rabiya Ali Hamim aliushukuru mradi wa Warld vegetable centre kwa kushirikiana na ZEA kwa kuwapa hii taaluma ambayo walikua hawana uwelewa nayo Ä·uhusu huo Mchicha lishe na upotevu wa mazao baada ya mavuno, hivyo mafunzo hayo yanaweza kuwapa fursa mbalimbali na kuweza kuzitatua changamoto za kimaisha.
Kwakupitia mradi huo wameahidi watakwenda kuyafanyia kazi nakuwapa ujuzi kwa wale wenzao ambao hawakubahatika kupata mafunzo hayo ili wajasiriamali waweze kuongezeka siku hadi siku.
Mafunzo yalioandaliwa na Warld vegetable centre kwa kushirikiana na ZEA chini ya mradi wa AID-I unaofadhiliwa na USAID ni ya miaka miwili kwa sasa yaliofanyika siku3 na yamejumuisha wakulima na wajasiriamali 220 kwamafunzo yana nadharia na wajasiriamali 30 kwa vitendo .
Mwisho
Comments
Post a Comment