NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
WANANCHI wa shehia ya Makombeni
wilaya ya Mkoani Pemba, wamesema bado wanahitaji elimu zaidi ya athari za
utiririshaji maji machafu katika makaazi yao, ili kujiepusha na magonjwa ya
kuharisha na kutapika.
Wakizungumza
na waandishi wa habari waliofika shehiani hapo, walisema bado wapo baadhi yao
wamekuwa wakitiririshaji maji hayo, bila ya kujalia afya za wenzao.
Walieleza
kuw, inawezekana wanaofanya jambo hilo ni kutokujua athari za maji hayo kwa
jamii na hasa watoto ambao tahadhari yao ni ndogo.
Mmoja kati
ya wananchi hao Ali Khamis Juma alisema, moja ya chanzo cha utirirshaji wa maji
hayo, ni magonjwa kama ya tumbo la kuharakisha na kutapika.
‘’Ni kweli
suala la uchafuzi wa mazingira hasa la utiririshaji maji machafu lipo kwenye
shehia yetu, na inawezekana wengi wao hawajui madhara,’’alieleza.
Nae Semeni
Juma Kheir, alisema hayo yanajitokeza kutokana na kutokuwepo kwa adhabu kali
kwa wananchi wanaodharau uchimbaji wa shimo la kuhifadhi maji ya machafu.
Kwa upande
wake Zuhura Faraji Kheir, alipendekeza kuwa kama atatokezea mwananchi ambae ni
msugu wa kuchimba shimo la kuhifadhia maji machafu, apigwe faini ya shilingi
50,000.
‘’Napendekeza
kwa mara kwanza faini iwe kima hicho, kama akiendelea kuwa msugu faini iwe
shilingi 100,000 na mpango huo uendelee hadi atapachimba shimo,’’alieleza.
Hata hivyo
Asha Nassor Makame na mwenzake Mpemba Ali Khamis, wamesema cha kufanya ili
kuhakikisha kero hiyo inaondoka, ni wataalamu wa afya kupita mara kwa mara.
Walieleza
kuwa, elimu ndio ambayo inahitajika zaidi kwa jamii, kwa kuelezwa athari za
utiririshaji maji machafu na faidi za kuyadhibiti maji hayo.
Sheha wa
shehia ya Mkombeni Mwashum Makame Haji, alisema kuwa elimu ya kuyadhibiti maji
hayo imeshatolewa mara kadhaa na wataalam kutoka Baraza la mji wa Mkoani.
Alifafanua
kuwa, wapo baadhi ya wananchi wamekuwa wasugu kuchimba mashimo waliyoelekezwa,
na juhudi za kuwaelimisha zimekuwa zikiendelea kila siku.
Sheha huyo
alisema, utiririshaji maji ya machafu yanapozagaa kwenye miji husababisha
usumbufu ikiwemo uchafuzi wa mazingira na kusambaa kwa kinyesi ovyo.
‘’Watoto na
wazee ndio waathiri wakubwa iwapo utiririshaji maji machafu utaendelea, hivyo
ni jukumu la wananchi kuliona hilo na kuacha utamaduni huo.
Mkuu wa
wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja, alisema kilichopo ni kuongeza kazi ya kutoa
elimu kwa jamii, ili ifike siku wananchi wote wamechimba mashimo.
Shehia ya Makombeni
wilaya ya Mkoani mkoa wa kusini Pemba, inawastani wa nyumba 507, zikiwa na
wananchi 2,154 huku wanawake 1,133 wakiwa na wanaume 10,212, wastani wa watu
wanne (4) kwa nyumba moja.
Mwisho
Comments
Post a Comment