NA
HANIFA SALIM, PEMBA
WAANDISHI
wa habari ni watu muhimu katika jamii yoyote ile ulimwenguni.
Maana moja ya majumku yao ambayo sio rahisi kufanya na kundi jengine
la watu ni kule, kuelimisha, kuburudisha na kuhabarisha iwe kijamii, kisiasa,kiutamaduni
na kiuchumi.
Licha ya changamoto ambazo wanakumbana nazo katika utekelezaji wa
majukumu yao, bado wana dhima kubwa ya kuipatia jamii taarifa ambazo zinatokezea
kila siku.
Pamoja na kadhia hiyo taasisi kama hizo za vilabu vyao, ‘Press Club’
huwa zinasimama wima, kuwatetea waandishi hao wanaokumbwa na madhila kadha.
Mei 3 ya kila mwaka duniani kote, kunaadhishwa siku ya uhuru wa vyombo
vya habari, ni siku muhimu kwa waandishi wa habari.
Waandishi wa habari wamekuwa wakifanya kazi zao kwa mujibu wa katiba
zote mbili, ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Zanzibar ya
mwaka 1984 ambazo zinahimiza upatikanaji
wa habari na kutowa habari kwa wananchi.
Kwa kawaida kila jambo ambalo linamaslahi na watu ili liweze kuenda
sawa ni vyema kuwa na umoja wao kama vile vyama, jumuiya na vyenginevyo.
PPC
Klabu ya waandishi wa habari Pemba, ndio ndio kimbilio pekee kwa
waandishi wote wa habari na watangazaji kisiwani humo.
Kama ilivyo miunganiko yote, nao PPC waliamua kuanzisha umoja, wao kwa
malengo kadhaa moja wapo ni kuwa na suati moja.
Pemba Press Club (PPC) tokea kuanzishwa kwake mwaka 2002, imefanya
mambo kadhaa yenye kuwajengea uwezo waandishi wa habari, juu ya utendaji wa
kazi zao za kila siku yakiwemo mafunzo na ziara za kimasomo.
MWANZILISHI
WA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI (PPC)
Klabu ya waandishi wa habari wa Pemba (PPC) ilianzishwa mwezi Disemba mwaka 2002, ikiwa na wanachama 30
wakati huo, chini ya Mwenyekiti Azizi Simai Alawi.
Chimbuko la klabu hiyo, lilianzia mwaka 1986, wakati Mwenyekiti huyo alipopata
safari ya kwenda Ujerumani, katika matembezi ya kujifunza kitaaluma.
“Nilipata ushauri kutoka kwa uwongozi wa Ujerumani, tuanzishe Klabu na
watatusaidia, baada ya kurudi nilikaa na uongozi wa wizara ya habari, wakatupatia
ofisi tukaanza kufanya kazi,’’anaeleza.
Baada ya hapo waandishi wa habari wa Unguja, walikua na jumuiya ya
waandishi wa habari wa Zanzibar (JAZZ), ambayo ilimteua kuwa Mratibu wa jumuiya
hiyo Pemba.
Mwaka 2002, alichaguliwa kwenda mkoani Mwanza Tanzania bara, kuhudhuria
mafunzo na alitakiwa kuanzisha tena Klabu ya waandishi wa habari Pemba.
“Kwa mara ya pili tulipoanzisha (PPC) tulikuwa na ofisi katika eneo la
stendi kuu ya gari sokoni mjini Chake chake, tulipata misaada mbali mbali
kutoka kwa Umoja wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC),’’alieleza.
Walianza kwa kuandika miradi ya kuelimisha waandishi wa habari,
kuandika habari za uchunguzi kwa kushirikiana na uongozi wa klabu ya waandishi
wa habari wa Zanzibar ‘ZPC’.
Anasema PPC imesaidia waandishi, kwa kuwaelimisha maadili ya uwandishi
wa habari, kuandika habari za uchunguzi, habari za michezo, za vijijini, za
uchaguzi na makala za aina mbali mbali.
Kuwepo kwa PPC kumekuwa na faida kwa waandishi wa habari, kwani
wamepata fursa za kujifunza, sambamba na tasisi zao walizoajiriwa.
MALENGO
YA KUANZISHWA PPC
Ni kuibua vitu ambavyo vitapelekea klabu yao kukuwa na kujiimarisha na
kujitegemea wenyewe, katika kuwahudumia wanachama wao.
“Tulikuwa na lengo ni kuanzishwa ‘Pemba Gazeti’ ambalo waandishi wa
habari wangelazimika kuleta habari zao ambazo zitatolewa kupitia gazeti hilo
iwe kama ni ajira,” anasema.
Mwazo yake kabla ya kuundwa kwa (PPC) ni kuanzisha redio jamii ya
klabu hiyo, hivyo anawashauri viongozi wa (PPC) kutafakari namna ya kuwa na
chombo bora cha kisasa kitakacho habarisha wananchi.
Aidha anasema walianzisha PPC baada ya kuona kundi kubwa la waandishi
wamekuwa wakikosa eneo la kujifunza zaidi, kutokana na uhaba wa vyombo kwa
wakati huo.
MWENYEKITI
WA SASA WA PPC
Bakar Mussa Juma ambae ni Mwenyekiti wa nne wa PPC, anasema, klabu za aina
hiyo zipo kila mkoa wa Tanzania.
Lengo lake ni kuwaunganisha wanahabari na kuwa ni chombo cha kupeleka
malalamiko yao na kuwa ni chombo cha kuwatetea pale wanapokumbana na matatizo.
Klabu inatafuta miradi kupitia taasisi mbali mbali, ikiwemo shirika la
Internews, wizara ya Afya na badala yake kutoa taaluma juu ya miradi hiyo.
“PPC imeshatoa mafunzo juu ya maradhi yasiyoambukiza, mafunzo ya
uwandishi wa habari za biashara, uchunguzi na makala kadhaa, ambapo hivi
karibuni tumetoa mafunzo ya uwandishi wa habari na changamoto za kidigitali,”anasema.
WAANDISHI
WANAJIUNGAJE NA PPC?
Waandishi wa habari ‘wanachama’ wanapatikana kwa kupeleka maombi na
kulipia kiingilio na ada ya kila mwezi, ambayo inatumika kwa uwendeshaji wa
shughuli za ofisi.
Umoja wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) ni mlezi wa
klabu za waandishi wa habari zote Tanzania, ambayo husaidia kutoa kodi ya
ofisi, kumlipa mratibu wa klabu pamoja na kutoa vifaa vyengine vya kiutendaji.
PPC hutekeleza miradi ambayo hulenga zaidi kutoa taaluma kwa waandishi
wa habari, juu ya kutumia kalamu zao kuihabarisha jamii ambapo ndio jukumu lao
kubwa la kikatiba.
‘’Hata mafunzo kuhusu matumizi ya kanuni, miiko na maadili ya
uwandishi wa habari ili habari zao zisiende kinyume na kazi yao, ‘’anafafanua.
MIKAKATI
Moja ni kuwafanya waandishi wa habari waweze kutumia kalamu zao na
vyombo vyao ikiwemo televisheni, redio, mitandao na magezeti katika
kuuhabarisha umma kupitia mambo mbali mbali.
Jambo la kujivunia kupitia klabu ya waandishi wa habari wa Pemba ni
kutoa waandishi wa habari weledi, wenye taaluma za juu na uwezo mkubwa wa
kuandika mambo mbali mbali.
MRATIBU
WA PPC
Mratibu wa Klabu ya waandishi wa habari wa Pemba (PPC) Mgeni Kombo
Khamis anasema, wamekuwa wakitoa mafunzo ya kihabari, kukumbushana maadili na
miongozo ya kazi zao.
Pamoja na hilo wamekuwa wakiwapatia mafunzo ya uandishi wa habari za
afya, mazingira, mahakamani, uchunguzi, sera na utafiti na habari za vijijini
ambazo zinawalenga wananchi.
PPC imeshatekeleza miradi mingi ikiwemo mradi wa kuelimisha wanawake
kushiriki katika masuala ya usajiriamali kwa kutumia vyombo vya habari kupitia
mradi wa sauti yangu mtaji wangu uliofadhiliwa na Tanzania media Fund (TMF) uliotekelezwa
mwaka 2017/ 2018.
“Pia tulitekeleza miradi kupitia klabu yetu hata wa kudumisha amani
mradi ambao ulifadhiliwa na shirika la Internews katika kipindi cha mwaka 2020,”
anasema.
Mradi mwengine ni wa kuelimisha jamii juu ya maradhi ya kifua kikuu
ambao unatekelezwa kupitia kitengo shirikishi kifua kikuu, ukimwi na ukoma
kutoka wizara ya afya kwa ufadhili wa Global fund, ulioanza mwaka 2019 na
unaendelea hadi sasa.
PPC kwa sasa ina wanachama 54 wakiwemo wanawake 26 na wanaume 28, .
MWENYEKITI
MSAAFU WA PPC
Mwenyekiti mstaafu wa klabu ya waandishi wa habari wa Pemba ‘PPC’ Said
Mohamed Ali anasema, PPC iliundwa kwa kuwaunganisha waandishi kwani kwa wakati
huo hakukua na chombo kiichowaunganisha.
PPC ni miongoni mwa klabu kongwe za waandishi wa habari ambazo zinatoa
fursa za kuwapa mafunzo waandishi kupitia miradi mikubwa.
“Chanzo cha kuanzishwa kwa eneo la wafanyabiashara juakali mjini chake
chake ni ‘PPC ‘tuliwakusanya kutoka sehemu tofauti, kushirikiana na BBC
kuandika habari za vijijini ambazo ziliibua changamoto nyingi na kuwawezesha
wananchi kupaza sauti kueleza kero zao,” anaeleza.
PPC ilitoa mchango wake mkubwa wa kuwepo kwa chuo cha habari Pemba,
ambao walipata mafunzo ya ngazi ya cheti na diploma.
Aliwataka waandishi wa habari wafanye kazi kwa kujituma wao wenyewe na
waache tabia ya kusubiri kupangiwa kazi, wajiamini, waache kushabikia siasa na
pia wakumbuke wajibu wao kwa jamii.
Mjumbe wa kamati tendaji wa klabu ya waandishi wa habari Pemba (PPC) anaewakilisha
kundi la vijana Gasper Chales anasema, klabu hiyo ina faida nyingi ikiwemo
kujenga uwezo kwa wandishi kwa kutoa taaluma.
Kwa Pemba waandishi wa habari wengi ni vijana ukizingatia wana
mahitaji yao mengi ikiwemo muendelezo wa kukuzwa kielimu.
“Kama kijana kazi ambazo tunazifanya ni kupeleka mawazo na kushauri
kuwepo kwa miradi ambayo itatunufaisha sisi waandishi vijana kwani tunahitaji
kuendelea kujifunza hiyo ndio kazi yangu kubwa,” anasema.
WANACHAMA
Mwandishi wa habari wa shirika la Magazeti ya serikali Pemba, Habiba
Zarali Rukuni ni mwanachama wa Pemba Press klab anasema, klabu hiyo ina mchango
kumbwa kwa waandishi wa habari kutokana na fursa wanazozipata.
‘’PPC imetunufaisha sana, moja ni kutuunganisha waandishi wa habari
kuwa kitu kimoja pamoja kutupatia mafunzo ya ndani na nje ya Pemba,’’ anasema.
Meneja wa ZENJ FM Pemba Is-haka Mohamed Rubea anasema, PPC
imewanufaisha kupata mafunzo ambayo hawakuweza na hata kutarajia kuyapata
katika taasisi wanazozifanyia kazi.
‘’Klabu hii ni muhimu kwa waandishi wa habari, inatusaidia kuongeza
ujuzi na maslahi yetu waandishi wa habari, tumepata sehemu ya kuwasilisha
malalamiko yetu tunapopata changamoto,’’ anasema.
Mwandishi wa habari wa kituo cha Swahiba FM, Fatma Hamad Faki anasema,
klabu hiyo ni muhimu imewasaidia waandishi wa habari waliowengi wamepata fursa
za kuongeza taaluma za juu za kimasomo.
MWISHO.
Comments
Post a Comment