NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
PAMOJA na kukua kwa uchumi, uimarishaji wa
miundombinu ya barabara na ongezeko kubwa la vyombo vya usafiri, imebainika kuwa,
kama Jeshi la Polisi na wananchi hawakushirikiana, vifo vitokanavyo na ajali za
Piki piki (boda boda) hazitopungua nchini.
Imeonywa kuwa, kwa
kuliachia jukumu la kupunguza ajali za piki piki Jeshi la Polisi pekee,
haitokuwa dawa ya kupunguza ajali hizo, ambazo pia husababisha vifo na vilema.
TAKWIMU ZA AJALI ZA PIKI PIKI
Uchunguuzi
uliofanywa na mwandishi wa habari hizi, umebaini kuwa, kwa mfano kwa mwaka 2019
hadi mwaka 2020 kwa Tanzania, kulikuwa na ajali za piki piki 1,133 zilizosababisha vifo 674, sawa na majeruhi 948.
Imebainika kuwa,
kati ya ajali hizo, Tanzania bara kuliripotiwa ajali 964, zilizosababisha vifo 573 na majeruhi 767 kwa miaka hiyo miwili.
Wakati kwa
Zanzibar, kuliripotiwa ajali 169 sawa
na vifo 101 huku idadi ya majeruhi
wakiwa ni 181.
Katika kipindi cha
Januari hadi Disemba pekee kwa mwaka 2020 kwa Tanzania, kulikuwa na matukio 505 ya ajali za pikipiki,
ikilinganishwa na matukio 628 katika
kipindi kama hicho mwaka 2019.
Kwa upande wa
Zanzibar, mikoa iliyoongoza kwa ajali za piki piki katika mwaka 2020, ni mkoa
wa Mjini magharibi ulioripoti ajali 1,774, ukihusisha vifo 25.
Ingawa kati ya hao,
wanaume waliongoza kwa kuwa 24, huku wanawake akiripotiwa mmoja aliyefariki,
kutokana na ajali za piki piki.
Mkoa mwengine ni wa
Kusini Unguja kwa ajali 469, sawa na vifo watu 10, huku wanaume wakiwa wanane
(8), na wanawake wawili.
Mkoa wa kusini
Pemba, uliripoti matukio 604, yakihusisha vifo 10, wakiwemo wanawake wawili (2)
na wanaume wanane (8).
Uchunguzi ukabaini
kuwa, kwa mwaka huo wa 2020, mkoa wa Kaskazini Unguja ulikuwa na ajali 311,
ambazo zilihusisha vifo vya wanaume wanane (8) na mwanamke mmoja, ambapo mkoa
wa Kaskazini Pemba, ulikuwa na ajali 858, sawa na vifo vya watu watano (5) wote
wakiwa wanaume.
VYANZO VYA AJALI
Jeshi la Polisi
Tanzania limesema, vyanzo hivyo vimegawaika katika makundi matatu makubwa,
ikiwa ni pamoja na sababu za kibinaadamu, ubovu wa vyombo vya usafiri na
uchakavu wa bara bara.
Imebainika kuwa,
kati ya ajali hizo 1,133, zilizoripotiwa
kwa kuanzia mwaka 2019 hadi 2020, na kusabisha vifo 674, ajali 508,
zilisabishwa uendeshaji hatari wa madereva wa piki piki.
Eneo jingine zipo
ajali 333, zilizosabishwa na madereva hao, kuipita gari ‘over take’ bila ya
uangalifu, huku ajali nyingine 239 zikisababishwa na watembea kwa miguu.
MADEREVA WA PIKI PIKI (BODA BODA)
Dereva wa piki piki
kijiji cha Wawi wilaya ya Chake chake Pemba, Khamis Nassor Kassim, anasema chanzoa
cha ajali hizo ni usimamizi hatarishi wa askari wa usalama barabarani.
‘’Wenyewe wamekuwa
wakitufukuza, kama hakutii amri ya kusimama, sasa inaweza kuzaa ajali na wakati
mwengine kusababisha vifo au vilema,’’anasema.
Kombo Himid Mkadamu
dereva wa piki piki, anasema mwendo kasi unachangiwa na vijiwe vingi vya boda
boda kutokuwa na zamu ya uchukuaji abiria.
‘’Tajiri anataka
shilingi 10,000 kila siku, na wewe uliyeajiriwa unataka fedha ya mafuta,
matengenezo madogo na kula ya kila siku, hivyo mwendo kasi lazima,’’anasema.
Nae dereva mwengine
wa Wete Pemba, anasema inawezekana kutokuwa na adhabu kali, huchangiwa na
baadhi yao kupuuza alama za barabarani.
‘Ni kweli sisi
tukishapakia abiria, hutaka tumfikishe na kurudi kijiweni kuchukua mwengine,
lakini hata ikitokezea, ajali ni kuwekwa ndani siku mbili, adhabu
imekwisha,’’anasema.
Abiria wa piki piki
Asha Kassim Khelef wa Micheweni anasema, wakati mwengine hata wao abiria, kwa
haraka zao, huwa ni sababu ya kutokezea ajali.
Abiri mwengine
aliyepata ajali ya kukatika mkono eneo la Chamanangwe, anasema chanzo ni
kufukuzana baina ya dereva wake na mwengine.
‘’Mimi kwa vile
nilikuwa nakimbilia uwanja wa ndege wala sikuwa na maneno ya kumzuia, lakini
ghafla walikwaruzana na kuanguka chini, ikawa ndio mwisho wa
safari,’’anaelezea.
Mkuu wa mkoa wa
kusini Pemba, Mattar Zahor Massoud, anasema uzuiaji wa ajali ya piki piki,
unaweza kufanikiwa kwa Jeshi la Polisi, abiria na madereva kushirikiana.
‘’Ajali za piki
piki haziwezi kupungua, maana askari na dereva wa piki piki hakuna kitu
kinachowaunganisha, ila kuna kitu kinachowakimbiza ambacho ni
ukaguzi,’’anasema.
Mwanaharakati wa
utii wa sheria bila ya shuruti Khalfn Amour Mohamed, anasema mifumo ya ukaguzi
wa piki piki barabarani, ni chanzo cha kutokezea ajali.
‘’Wakati mwengine
askari wanakaa kwenye mipindo, au kwenye taa za kuongezea vyombo vya usafiri,
au kwenye mikusanyiko mfano mikutanoni, ndio anafanya ukaguzi,’’anasema.
Mwenyekiti wa
Jumuia ya waendesha boda boda mkoa wa kusini Pemba Kassim Khamis Juma, anasema
bado waendesha piki piki na askari, wamekuwa wanakimbiana.
‘’Elimu ya
kujikinga na ajali tunawapa kila muda, lakini wapo wengine sio wanachama na
ndio wachafuzi wa amani na utulivu kwenye barabara,’’anasema.
Mmilikiwa boda boda
Juma Shaame Issa na mwenzake Mwanakhamis Juma Mohamed, wanasema moja ya sharti
wanalowapa waliowaajiri, ni kutokuwa chanzo cha ajali barabarani.
‘’Ajali za piki
piki zinaweza kupungua, ikiwa sheria zitakuwa kali kwa dereva anayesababisha
ajali, na moja wapo iwe ni kuny’ang’anywa leseni yake kwa kipindi,’’anasema
Juma.
Asha Mussa Mjaka
ambae alipata ulemavu kwa ajali ya piki piki mwaka 2020, anasema ilisababishwa
na honi ya ghafla iliyopigwa na gari ya Polisi, ikiashiria dereva huyo asimame.
‘’Mimi sikuwa
nimevaa kofia ngumu ‘helment’ sasa wao waliokuwa kwenye msako, tena eneo lenye
mpindo, basi baada ya honi dereva alishtuka na kuingia msingini na kukatika
mguu,’’anasema.
JESHI LA POLISI
Mkuu wa kikosi cha
usalama barabarani mkoa wa Mjini magharibi Unguja Khamis Mwakanolo, anasema
chanzo cha ajali ni madereva wa piki piki, kutokujua athari za ajali.
‘’Hawajui kuwa kila
ajali inapotokezea, athari ya mwanzao huwa ni mwili wa dereva, ndio kisha
chombo ama mtu mwengine, sasa haya kwa vile hayajulikana ndio maana ajali
zinatoezea,’anasema.
Anaeleza kuwa, sio
sahihi kwa askari wa usalama barabarani kukaa kwenye taa za kuongezea gari,
kuwa wanakuwa chanzo cha ajali.
Maana anssema wapo
baadhi ya waendesha vyombo hasa wa piki piki, huondoka kukatisha barabara hata
kama taa hazimruhusu kufanya hivyo.
‘’Kuwepo kwa askari
kila eneo ni chanzo cha kuzuia ajali, ingawa kutokana na changamoto za kuongoza
misafara, kushiriki kwenye shughuli nyingine za kitaifa, madereva hutumiya
vibaya fursa hiyo,’’anasema.
Mkuu wa usalama barabarani Mkoa wa kusini
Pemba Shawal Abdalla, anasema wapo baadhi ya wazazi wanawanunulia piki piki
watoto wao bila ya kujali kwanza umri, pili leseni na ruhusa ya njia, ili
ikifika wakati wa ukaguzi isiwe kukimbiana baina.
Ajali zilizonyingi
huwa zinazuilika, na hasa ikiwa dereva amekizi vigezo vya kuingia barabarani,
maana kwanza hatokuwa na hofu ya ukaguzi kutoka mamlaka yoyote.
MITANDAO YA KIJAMII IMERIPOTI NINI?
Ajali za barabarani zinatajwa
kuwa ndio zinasababisha vifo vingi vya watu duniani kulimo magonjwa yoyote, Shirika
la Afya Duniani WHO. linasema.
WHO kwenye ripoti yake ya mwaka 2018, limeanisha licha ya
bara la Afrika kuwa na idadi ndogo ya vyombo vya usafiri, lakini ndilo lenye ajali
nyingi za barabarani duniani, kuliko mataifa ya Ulaya.
Katika ripoti hiyo ‘WHO’ linasema kuwa kuna vifo 27 kwa
kila watu 1000, huku likifafanua kuwa, kuna vifo vya barabarani katika nchi za
Afrika ni mara tatu zaidi ya ajali zinazotokea Ulaya.
Ripoti ikafafanua kuwa, karibu nusu ya mataifa 54 ya
Afrika hayana sheria za mwendo kasi katika nchi zao, huku nchi kama Botswana,
Ivory Coast na Cameroon, ni miongoni mwa nchi ambazo zimeona kiwango cha vifo
vikiongezeka.
Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni , zinasema kuwa
watu milioni 1.35 waliuwawa katika ajali za barabarani duniani kwa mwaka 2016,
kiwango ambacho kiko tofauti kidogo na mwaka uliopita.
Upande mwengine katika ripoti iliyotolewa na Benki ya Dunia, imeelezwa kuwa hadi
kufikia mwaka 2020, idadi ya vifo vinavyosababishwa na ajali za barabarani
katika nchi za Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara, itaongezeka kwa asilimia 80.
ATHARI ZA AJALI ZA PIKI PIKI
Kassim Haji Ali
abiria ambae kwa sasa ana mkono mmoja, anasema kwanza ni kupata ulemavu wa
kudumu ambao haukutarajiwa.
Mayasa Hassan Hemed
ambae mume wake alipoteza maisha mwaka 2022 kwa ajili ya pili pili, anasema ni
vifo na kuwaacha watoto wakiwa na mlezi mmoja.
Baba ambae mtoto
wake alifariki kwa ajili, anasema ni kukosa nguvu kazi ya familia, kwani kila
familia inawategemea wengine kwenya kazi.
Mkuu wa kikosi cha
usalama barabarani mkoa wa Mjini magharibi Unguja Khamis Mwakanolo, athari ni
kuongeza umaskini ndani ya familia, kwa matibabu makubwa.
Mmiliki wa piki
piki (boda boda) Michakaini Chake chake Pemba Kombo Haji Kombo, anasema kwanza
ni kuwarejesha nyuma wao walioekeza kwenye vyombo hivyo.
Doktari Khamis Haji
Khamis anasema, ni matumizi ya dawa yasiyotarajiwa, kwa waendesha piki piki,
ambao kwa mwezi hujitokeza katia ya watatu hadi watano.
NINI KIFANYIKE KUPUNGUZA AJALI?
Kamisha wa Polisi
Zanzibar Hamad Khamis Hamad, anasema kwanza ni elimu kwa waendesha piki piki,
juu ya matumizi sahihi ya barabara.
Mwenyekiti wa
Jumuiya ya boda boda mkoa wa kusini Pemba, Kassim Khamis Juma, anasema
kuimarishwa kwa miundo mbinu ya barabara, hasa kutokana na ongezeko la vyombo
vya moto.
Dereva wa piki piki
Othman Issa Yakoub anasema utaratibu wa kukagua piki piki kila wakati uondoke,
na badala yake kuwe na mifupo ya kisasa.
Mwananchi Zuhra
Juma Mmanga wa Ngwachani Mkoani anasema, ni uwepo wa adhabu kali kwa dereva wa
piki piki, atakaetiwa hatiani kwa kosa hilo.
Jaji mkuu wa Zanzibar,
Khamis Ramadhan Abdalla, anasema mifumo ya sheria ikirekebishwa na kutiwa
hatiani kwa wakosaji, inaweza kuwa dawa.
Afisa Sheria kutoka
Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar Bakar Omar Ali, anasema kamera
zilizopo mjini zitumike kuwatia hatiani wanaokiuka sheria.
Mwisho
Comments
Post a Comment