NA HABIBA ZARALI,
PEMBA@@@@
HAWAKUKOSEA
waliosema 'umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu'
Msemo huu umesadiki
katika utekelezaji wa mradi wa kuwawezesha wanawake kudai haki zao za uongozi ,
demokrasia na siasa 'SWIL' unaotekelezwa kwa mashirikiano kati ya TAMWA Zanzibar, ZAFELA na PEGAO.
Mradi huo ambao
ulizinduliwa mwaka 2020 na kutarajiwa kumalizika 2023 umeonekana na mafaniko
makubwa katika hatuwa mbalimbali za utekelezaji wake.
Utekelezaji wa
mradi huo ambao ulitarajiwa kuwafikia na kuwawezesha wanawake 6000 kwa zanzibar,
Unguja na Pemba katika kudai haki zao ili nao waweze kuwawezesha wengine tayari
umeonyesha njia katika kufikia hatuwa ya kudai haki zao za uongozi.
Mradi huo wa SWIL ambao
unafadhiliwa na ubalozi wa Norway umetekelezwa maeneo mbalimbali ambapo kwa
upande wa Pemba tayari umeshawafikia wastani wa wanawake 4000.
Katika hatuwa za
kufanikisha lengo la mradi la kuwawezesha wanawake kudai haki zao za uongozi
demokrasia na siasa kumeanzishwa kamati za Wilaya za kuhamasisha wanawake kudai
haki zao za uongozi.
Kamati hizo
zinajulikana kwa jina la kiutaalamu 'citizen brigged' asilimia 60 ni wanawake
na 40 ni wanaume ambao ndio walengwa wakuu wa kutowa ushirikiano kufikia
malengo ya mradi huo.
VIONGOZI WA MRADI
Mkurugenzi
mtendaji wa mradi wa Swill kutoka PEGAO Hafidh Abdi Said anasema kwa Wilaya za
Pemba mradi umevuuka lengo kwani wameshajengewa uwezo zaidi ya watu
waliokusudiwa.
Anasema
uhamasishaji huo haukulenga kuwajengea uwezo wanawake hao kuwa viongozi
serikalini wala vyama vya siasa pekee bali hadi ndani ya sekta iliyomo ndani ya
jamii.
"Wanawake
hawatakiwi tu kuingia ndani ya Serikali bali hadi ndani ya vyama, kamati
za maendeleo , jumuiya , nafasi za usheha na maeneo mengine",alisema.
Alifahamisha kuwa
idadi ya wanawake kwenye uongozi kwa sasa imezidi ukilinganisha na awamu
iliyopita Tanzania zanzibar na bara.
Mratibu wa mradi
huo kutoka TAMWA Zanzibar Fat-hiya Mussa
Saidi anasema tayari mradi umefikia hatuwa ya lengo lililokusudiwa ambapo ndio
tarajio lake kwani mradi huu unawawezesha
wanawake lakini na wanaume wanahusishwa.
Anaeleza kuwa
utekelezaji wao mkubwa ndani ya mradi huo wa swill umewawezsha waandishi wa habari wa Unguja na Pemba, ili
wapate uweledi wa masuala ya wanawake na uongozi.
“Tunaamini kama
tukiwawezesha vizuri waandishi wa habari
watakuwa na maono mapana na kuondokana na dhana zilizo ndani ya jamii juu ya
wanawake na uongozi.
Hata hivyo anasema
vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika kufikisha elimu hiyo kwa jamii
,kwani vimekuwa na sauti pana ambayo haifikiwi na taasisi nyengine.
Mapema Mratibu wa
mradi huo kutoka PEGAO, Dina Juma Makota anasema wanawake wanapaswa kujiongeza
kielimu, washiriki katika masuala ya kijamii, kutokata tamaa, waweze kupambana na kutokana tamaa ili waweze
kushinda vikwazo vinavyowekwa na kuwakosesha nafasi za uongozi.
Anasema kupitia
mradi huo tayari tayari wamewajengea uwezo wanawake ambao walikuwa hawawezi
hata kusimama mbele za watu lakini sasa wanaweza hata hivyo wako walioingia
kwenye chaguzi za ndani na kushinda.
Anasema kundi hilo
lina haki sawa na la wanaume ingawa wenye mamlaka ,wanaliona tofauti kundi la
wanawake ingawa mradi wa kuwawezesha
kudai haki zao ‘swill’ unaweza kusaidia kwani hata jamii imeweza kutatuliwa
kero ambazo zinawarejesha nyuma”anasema.
WAHAMASISHAJI
JAMII KUPITIA MRADI
Nachia Khamis
Mohamed wilaya ya Mkoani anasema katika kutembelea vijijini wamebaini
changamoto mbalimbali zinazosababisha wanawake wasifikie malengo ya kuwa viongozi
ingawa baada ya kugunduwa walilazimika kutowa elimu.
Anasema wamebaini wanawake
wengi wanakuwa na lengo la kugombea nafasi za uongozi lakini wanakwazwa ikiwemo
ndoa kwani hupambana na wivu kwa wanaume zao, dhana potofu kwa kisingizio cha
kuwabadilikia.
Umbali wa skuli kwa
baadhi ya maeneo nao unawasababisha kutofika malengo kwani vijana wa kike wengi
huishia darasa la tisa na kukatisha masomo jambo ambalo huvisa malengo yao
yakiwemo ya kugombea nafasi za uongozi.
“Tunapozikuta
chanagamoto zinazowakwaza wanawake kufikia uongozi tunakaa pamoja na kutowa
elimu kati ya wanawake na wanaume na kuwaelekeza umuhimu wa mwanamke kuwa
kiongozi yote inatokana na dhamira ya
mradi wa swil”,anasema.
Ali Abdalla Juma wa wilaya ya Chake chake anasema kutokujiamini
,jamii kuwa na uwelewa mdogo unaohusiana na wanawake na uongozi kwani wengi
hawakusoma, wanaume kutowaruhusu wake zao kugombea, mitaji hasa katika nafasi
za juu kama ubunge na uwakilishi, ukandamizaji kwa baadhi ya vyama ni mambo
yanayofanya wanawake kuwa nyuma katika kugombea nafasi za uongozi.
Baada ya kuona hizo
changamoto chini ya mradi huu wa SWIL kwa vile na sisi tumesha wezeshwa basi tuliweza kutowa elimu kwa jamii kwa mifano hai ya
kidini na kiulimwengu tukiwahusisha viongozi wa kike akiwemo mama Samia Raisi wa Tanzania pamoja na bi
Khadija Binti Khuwailid ambae alikuwa mke wa kiongozi wa kiislamu Mtume
Muhammad (S.A.W).
Saada Saleh Ali Wilaya
ya Wete anasema kwa upande wao wamegunduwa baadhi ya maeneo wanawake wengi
hawajui kusoma na kuandika na tayari wamefanikiwa kuanzishwa kwa darasa la watu
wazima katika kijiji cha Kiuyu Minungwini.
“Pamoja na mambo
mengine kama vile umbali wa skuli matatizo ya maji ,vituo vya afya vya
kujifungulia,ukandamizaji kwa baadhi ya vyama, jamii kutopendana lakini
tumefikia hatuwa nzuri ya kuelimisha na ni ukweli usiopingika kuwa kwa sasa kupitia
mradi w swill wanawake wameamka”,alisema.
WANAUME
Ali Makame Juma
(57) wa Mkoani anasema kabla ya kuja
mradi huu wanawake hawakujuwa haki zao na ndio maana ikawa nafasi nyingi
zinachukuliwa na wanaume jambo ambalo halikuwa sahihi.
Anasema hatuwa
inayochukuliwa na mradi ya kupita katika jamii na kuweza kutowa elimu hiyo ni
ya mfano kwa vile wanawake wengi walikuwa wamelala katika suala la kudai haki
zao hasa za uongozi na kuwaachia wanaume peke yao.
“Mimi mwenyewe
nilikuwa naona kama hakuna umuhimu wa wanawake kuwa viongozi lakini kumbe ni
bora tukiwapa wanawake kuongoza kuna neema kubwa kupitia wao kwa vile ni
waaminifu kuliko ata sie wanaum
e,”anasema.
Zuhura Juma Khamis
(42) wa Chake chake anasema bado wenye mamlaka ambao wengi wao ni wanaume
wanawabania kuwapa nafasi wanawake jambo
amabalo kwa sasa wanatakiwa kuachana nalo na kuwatizama wanawake kwani nao
wanaweza kushika nafasi zaidi ya wanaume.
Salma Suleiman wa
Mkanyageni anasema elimu inayotolewa na
mradi wa Swill imeweza kuwafunuwa macho wanawake wengi na wameelewa kuwa kumbe
kuna fursa mbalimbali wanazikosa kutokana na nafasi nyingi kuchukuliwa na
wanaume.
“Sisi huku vijijini
ndio ambao tuko nyuma sana hasa katika masuala ya uongozi kwani imezoeleka kuwa
mwanamke si wa kuwa kiongozi na badala yake akae nyumbani na kulea watoto basi
jambo ambalo limeturejesha nyuma kwa muda mrefu sana.
WANAHARAKATI
Wanaharakati
wanaopinga haki za wanawake kisiwani Pemba wanasema wanawake wengi wamekuwa na
uthubutu wa kuweza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na kuweza kuzikamata.
Tatu Abdalla Msellem
anasema hata nafasi za usheha ,udiwani na nyengine katika jumuiya mbalimbali
zinaonekana kukamatwa na wanawake jambo ambalo hapo zamani halikuwepo.
Uthibitisho wa hilo
ni pale tunapoona kuongezeka idadi ya masheha katika wilaya zilizopo kisiwa cha
Pemba, kwa upande wa wilaya ya wete inayo masheha wanawake 14 kati ya shehia 36
jambo ambalo hapo nyuma hawakuwepo.
Wilaya ya chake
ambayo ilikuwa na sheha mmoja tu mwanamke sasa imepiga hatuwa hadi kufikia
watano ambapo wilaya ya Mkoani nayo imefikia masheha kumi, pamoja na ile ya
micheweni iliyofikia masheha nane.
Asha Muhsin Ali
anasema lazima wenye mamlaka waone aibu pale wanapowaacha wanawake katika
nafasi za uongozi kwa vile wanapopewa nafasi hizo wanaweza kuongoza na kuwashinda
hata wanaume.
“Mbona sasa tunaona
mabadiliko ya uongozi si haba katika mawilaya ,vyama na hata kamati za
maendeleo zilizomo kwenye jamii pakiwa na kiongozi mwanamke hakuharibiki na
mambo yote huenda sawasawa”alisema.
VIONGOZI WANAWAKE
Mwakilishi wa jimbo
la Chambani Bahati Khamis Kombo anasema mwanamke kushika uongozi ni jambo la
neema maana amekuwa mwarubaini wa kumaliza kero.
“Inashangaza na
haipendezi hata kidogo kuona kuwa bado wapo wanaume wenye mamlaka hawataki
kuwapa wanawake nafasi za uongozi na kuendelea kudidimiza maendeleo yao nay a
nchi kwa ujumla”,alisema.
Katibu Tawala
Wilaya ya Mkoani Miza Hassan Faki anasema licha ya wanawake kuonekana
kuongezeka katika ngazi za maamuzi
lakini bado haijaridhisha na inahitaji kuongezeka.
“Mradi huu wa swil
una shabaha nzuri kwa jamii na imeonekana kwenye mabadiliko ya wanawake
walivyohamasika na kudai haki zao za kuwa viongozi katika sekta mbalimbali na
juhudi za mradi huu huenda kwenye uchaguzi 2025 idadi ya wanawake majimboni na
kwenye wadi itaongezeka”,alisema.
Mkuu wa Mkoa wa
Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib anasema ili wanawake wasiweze kuachwa nyuma kwenye nafasi za uongozi
jamii itilie nguvu kuwasomesha watoto wa
kike ili mwisho wa siku kusiwe na kikwazo cha kielimu ambacho wanakitumia katika
kugombea nafasi.
Mkuu wa wilaya ya
Micheweni Mgeni Khatib Yahya anasema hakuna tatizo lolote mwanamke kuwa
kiongozi ikiwa atajiamini , kufanya kazi zake kwa uweledi na kukusimamia
maamuzi aliyoyatowa .
“Mimi apa mwenyewe
ni mwanamke na ni kiongozi lakini nafanya kazi zangu bila matatizo yoyote wala
siyumbi na napata kuwasemea wanawake wenzangu matatizo yao.
Sheha wa shehia ya
madungu Mafunda Hamad Rubea anasema hajaona chanagamoto yoyote ya utendaji kwa
kisingizio cha kuwa ni mwanamke kwani muongozo na taratibu za nafasi yake zipo
na zimeeleza wazi tena kwa ufasaha.
VIONGOZI WA DINI
Sheikh Said Ahmad Mohamed
kutoka ofisi ya Mufti anasema mwanamke hajakatazwa kuwa kiongozi na hasa akiwa
atazingatia maadili ,mila na desturi za dini na jamii yake.
“Yapo mambo hupaswa
wanawake wajiamulie wenyewe na sio busara kuona mifumo dume inatawala hadi kwa
mambo ambayo ni ya pamoja au yanawahusu wanawake pekee,”alisema.
Father Zero Marandu
kutoka kanisa katoliki Chakechake anasema hajakatazwa mwanamke kuongoza kwani anasema hakuna kondoo mwanamke kuchungwa
na mwanamme , hivyo lazima na wanawake nao wafike kwenye zizi ili kuangalia
kondoo wao .
Akimaanisha kuwa
mwanamke kuwa kiongozi sio jambo la mjadala maana wenyewe wana ajenda zao
wanapaswa wazishughulikie wenyewe.
Ni wakati sasa
jamii inapaswa kubadilika na kuacha tabia ya kumuona mwanamke hawezi kuwa
kiongozi kwani fikra hizo zinaporomosha
maendeleo ya wanawake na jamii nzima hasa ukizingatia wanawake nao wana masuala
yao mengi ambayo yanawahusu na yanahitaji kusemewa.
mwisho.
Comments
Post a Comment