NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
KUFUATA uzazi wa mpango, haihusiani
na kuzaa watoto kidogo.
Uislamu unafafanua kuwa, hakuna uhusiano wowote kati ya kuzaa
watoto kidogo, eti chanzo kikawa ni kufuata uzazi wa mpango.
Kumbe, kutajwa suala la uzazi wa mpango na Muumba, alishajua ili
mtoto aweze kupata virutubisho na mjengo wa mwili, kiakili, mifupa na ngozi, anyonye
maziwa ya mama yake.
Ndio maana Mhadhiri chuo Kikuu cha Zanzibar ‘SUZA’ Profesa Issa
Haji Zidi, anasema uzazi wa mpango, ambao uislamu unaukubali, sio jambo kubwa,
bali ni kumuacha mtoto kunyonya miaka miwili.
Kufanya hivyo, ndio hujenga huruma, mapenzi, udugu wa kiafya
kuanzia ya mama na mtoto mwenye, ijapokuwa pia humpa nafasi baba kujipanga
tena.
Kumbe, hata mwanamme anapata wasaa wa kucheza cheza na mke wake
vyema, iwapo uzazi wao, utakuwa ni wa mpango, kama ambavyo Muumba, ameagiza.
‘’Wapo wanaume hukesha kwenye vibanda vya starehe kwa usiku
mkubwa, akikumbuka kwenda kwake na idadi ya watoto wasiopishana, huona
karaha,’’anasema.
Hapa Sheikh Nurdeen Kishki, anasema unaweza kuzaa watoto hadi 10
au 15, ingawa suala la uzazi wa mpango, ndio msingi mkuu.
Uislamu, unawapendelea wema mno wanandoa, na unyonyeshaji wa
miaka miwili, ni kumrejeshea mama mazazi afya yake, ili kujipanga tena, kwa
kushika mimba nyingine.
‘’Uislamu unavyosisitiza uzazi wa mpango, hauna jambo kubwa la
kuibua mijadala, bali ni kule kutimiza haki ya mtoto, aliyezaliwa, ya kunyonya
kwa miaka mwili,’’anasema.
Sheikh Salum Msabaha, akizungumza kupitia tv za kislamu za
mitandaoni, anasema wala uzazi wa mpango, haujapingana na kauli ya kingozi wa
waislamu, anayetaka kujifaharisha siku ya malipo, kwa kuwa na idadi kubwa ya
watu.
‘’Uislamu unahimiza ya kuwa, ‘na wanawake walojifungua
wanyonyeshe watoto wao miaka miwili mfululizo, ikiwa wanataka kutimiza,’’ alinukuu
aya ya Qur-an.
Sheikh Abdalla Nassor Abdalla ‘Mauli’ wa Chake chake, anasisitiza
kuwa, uislamu unataka watu wenye afya bora na imara, ili kuyakabili vyema mazingiara
yao, ya kujitafutia chakula.
Akaenda mbali akasema, maziwa ya mama na hasa ya miaka miwili,
yana virutubisho, ambavyo havipatikani kwenye nyama, samaki wala tunda la aina
yoyote ulimwenguni.
Tena maziwa hayo, yanatofautiana, kati ya yale ya miezi miwili na
ya baada ya kujifungu na yale ya mwaka mmoja na miezi sita, jinsi yalivyobeba
virutubisho.
Kumbe maziwa ya mama, yalioingiliwa na mtoto mwengine, huzaa
homoni sugu, ambazo mtoto akiyanyonya huvuruga mfumo wake wa chakula.
‘’Ndio maana, mtoto anaenyonya maziwa ya mama mwenye ujauzito,
kwanza hupungua uzito, homa za mara kwa mara na baada ya wiki tatu, anaweza
kutapika,’’anaeleza.
Ilishaelezwa kwenye uislamu kuwa, waumini wa dini ya kiislamu
wasijiingize, wala wasiingizane kwenye madhara baina yao, ikiwemo kunyonyesha
maziwa mabovu mtoto.
IPI NJIA NZURI YA UZAZI WA MPANGO
ISIYO NA MADHARA?
Uislamu unaelewa kuwa, zipo njia kadhaa za uzazi wa mpango,
ingawa unazigawa katika makundi mawili makubwa, ikiwemo zinazokubalika na
zisizokubalika.
Sheikh
Nurdeen Kishki, anasema njia nzuri ambayo ilikuwa ikitumiwa na hata na Masahaba,
ni ile kwa mwanamme aliyekwenye ndoa, kukwepesha mbegu zake.
‘Njia
ya kukwepesha, inahitaji ujasiri hasa kwa mwanamme na hasa mwenye umri wa rika
la kati, ambapo njia hii, shahawa hutakiwa kutegeshewa kabla ya kuingia kwenye
mji wa uzazi, ni kuzitolea nje,’’anasema.
Njia
hii, inahitaji mwanamme na mwanamke jasiri, maana wapo wanaojaribu, ingawa
wakati mwengine hushindwa njiani.
Sheikha
Salum Msabaha, anasema njia hii haina madhara, hata chembe kwa wanandoa, na
uislamu inaikubali, kwani ilishatumiwa na waliotangulia kabla.
‘’Njia
ya kukwepesha bunduki (uume) ili
risasi (mbegu za kiume) zisiingie
ilipokusudiwa, ni nzuri ingawa mwanamke, hutakiwa
kuzichuma dalili za muume wake mapema,’’anafafanua.
DALILI ZA MATAYARISHO YA KUKWEPESHA
Moja,
inatajwa kuwa mwanamme kuongezeka joto la mwili, kuliko lile alilonalo kawaida,
kwa mfano mwili huunguza mithili ya mpishi wa mikate ya bekari.
Nyingine
ni kuongezeka kwa mvuto wa pumzi, kutoka nje ya tundu za pua kwenda ndani,
mithili ya mtu anayefukuzwa na mnyama mkali.
Mwaname
ambaye anakaribia kutoa mbegu, huanza kupoteza nguvu ghafla, na hapo mwanamke
hutakiwa kumsukuma kwa mpangilio muume wake, ili kuepusha mbegu kuingia ndani
ya uke.
‘’Dalili
nyingine kwa mwanamme ambaye anakaribi kutaka kutoa mbegu zake za uzazi ‘sparm’
hufumba macho japo kwa sekunde tatu hadi nne, hivyo mwanamke kama yuko makini,
na kuzitambua dalili hizi, anaweza kumkwepesha muume wake,’’anasema sheikh
Mohamed Makame Ali.
Wanaume
wamekumbushwa kuwa, nao lazima wazijue dalili ambazo, zitawaweke tayari, ili
kabla ya asali ‘manii’ kutoja kwenye
mji wa uzazi, waweze kukwepesha.
Moja
inayotajwa, ni kujihisi kupungua uzito hasa kwenye viungo vya mwili, mithili ya
kutaka kupoteza fahamu, pamoja na kupungua kasi ya awali ya kutikisika katika tendo
la ndoa.
Dalili
nyingine, ambayo wanawaume inawatokezea ni kumuona mwenza wake, kama anasinzia
au wakati mwengine kuongeza kasi ya uvutaji pumzi tena usio wa kawaida.
UPI WAKATI MWAFAKA KUTUMIA NJIA YA KUKWEPESHA?
Viongozi
wa dini ya kiislamu, wanashauri kuwa, wanandoa inapendeza zaidi, wafuatilie
mpangilio wao wa tarehe husika, kabla ya kuingia kwenye tendo la ndoa.
Mtaalamu
wa afya ya uzazi kutoka hospitali ya Chake chake Dk. Rahila Salim Omar, anasema
kama wanandoa, wameamua kuifuata njia hiyo, ni vyema wakawa bega kwa bega na
tarehe zao.
‘’Zipo
tarehe, mwanamke baada ya kumaliza hedhi, hawezi
kupata ujauzito, sasa siku hizo inashauriwa iwe ndio siku za kukutana na muume
wake,’’anafafanua.
Mkufunzi
wa afya ya jamii, Ali Mbarouk Omar kutoka Tume ya Ukimwi Zanzibar, anasema
uzazi wa mpango kwa njia ya kukwepesha, ni moja wapo ya uhakika.
Zipo
kadhaa, lakini kwenye dini ya kiislamu ambazo zimekubaliwa ikiwemo ya
kukwepesha na kufuata tarehe ni nzuri na hazina madhara kiafya.
Sheikh
Abdalla Nassor Abdalla ‘Mauli’ anasema kujikadiria watoto hasa kwa dhana kuwa,
huna uwezo wa kuwahudumia haifai, katika uislamu.
‘’Chakufanya
ni kufuata uzazi wa mpango, unaoambatana na mwanamke kunyonyesha miaka mwili
mfululizo, ikiwa hakuna kikwazo cha daktari,’’anasema.
Maana
wapo wanawake baada ya kuzaa, kwa kuhofia matiti yao kuanguka, hushindwa
kuwanyonyesha watoto wao, jambo amblo halikubalika katika uislamu.
Uislamu unawataka watu kuoana na kuzaana kwa utaratibu na mfumo mzuri,
ili kutunza na kulea maadili ya familia, kwani umeweka utaratibu wa umri wa
kuzaa kati ya mtoto mmoja na mwengine (2:233).
WANAUME WANASEMA JUU YA NJIA YA KUKWEPESHA
Issa Othman Haji
(55) mwenye watoto sita, anasema njia hiyo anaiona nzuri, ingawa kwa wanaume,
wenye mke zaidi ya mmoja.
‘Kwa mfano nina wake
wawili, sasa njia ya kukwepesha hainipi dhiki, tena ni mzuri na haina madhara,
lakini sina hakika kwa wenye mke mmoja,’’anasema.
Adnani Ali Khamis
(30) anasema yeye anatumia njia hiyo, ingawa anakwenda sambamba na kuzijua
tarehe za kubeba na kutobeba ujauzito kwa mke wake.
Mwanamme ambae
hakupenda jina lake lichapishwe, anasema njia hiyo ya kukwepesha ni nzuri,
lakini inahitaji umakini mkubwa kwa wanandoa.
‘’Mimi mke wangu
anatumia ya sindano, na hadi sasa haijamletea madhara, lakini hata hivyo mtoto
wangu akiwa na mwaka mmoja na mizei sita, najaribu kukwepesha na nafanikiwa,’’anasema.
Othman Khamis
Mmanga wa Chanjamjawiri, anasema mara kadhaa alijaribu njia hiyo, ingawa
humshinda njiani.
WANAWAKE WANASEMAJE
Maryam Himid
Mjaka (19) wa Wawi anasema haijaingia kwenye ndoa, lakini njia mwafaka ya kuwa
na uzazi wa mpango ni kukwepesha na kutumia tarehe.
Aisha Mkadamu
Nassor (50) wa Kengeja anasema, njia aliyokuwa akiitumia ni tarehe na
kukwepesha, wakati wote wa tendo la ndoa.
Maimuna Ali
Mohamed (22) ambae sio jina lake, anasema alijaribu kumataka muume wake
akwepeshe, ingawa alishindwa na sasa anaujauzito wa miezi sita na mtoto wa
mwaka mmoja.
‘’Baada ya kumzaa
mtoto wa kwanza, nilimuuliza muume wangu, tunafanya nini, kuhakikisha namnyonyesha
miaka mwili, akataka tukwepeshe, ingawa alinyonya mwaka mmoja tu,’’anafafanua.
TAMWA INAFANYA NINI?
Chama cha Waandishi
wa Habari Wanawake Tanzania –TAMWA Zanzibar na Tanzania bara, wanaendelea
kutekeleza mradi wa majaribio wa mwaka mmoja, wa haki ya afya ya uzazi.
Mratibu wa mradi
huo Zanzibar, Zaina Abdalla Mzee, anasema lengo ni kuwajenge uwezo waandishi wa
habari, ili waweze kutoa elimu kwa wanawake, wasichana na jamii, juu ya faida
za uzazi wa mpango.
Maradi huo, unaendeshwa katika wilaya za
Magharibi ‘B’ Kati kwa Unguja na Chake chake kwa Pemba, ambapo ulikuja baada ya
utafiti kugundua, elimu ya haki ya afya ya uzazi, iko chini kwa jamii.
Unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya
TAMWA-Zanzibar na wenzao wa Tanzania bara, unafadhiliwa na Shirika la
Wellspring Philonthropic fund la Marekani.
Shabaha kuu ya mradi huo ni kuwajengea uwezo
waandishi wahabari, ili kuripoti kwa ufanisi, juu ya haki ya afya ya uzazi kwa
wanawake na wasichana walioko mjini na vijijini.
WIZARA
YA AFYA
Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahme Mazurui,
anasema watumiaji wa njia za kisasa za uzazi wa mpango wamepungua kutoka mama
63,261 kwa kipindi cha Julai, 2020 hadi Machi, 2021 na kufikia 61,379 kwa
kipindi kama cha mwaka 2021/2022.
Shirika la Afya Ulimwenguni, kwenye taafita yake
ya mwaka 2022, limethibitisha kuwa matumizi ya njia za uzazi wa mpangilio,
yanaweza kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi 30, kila wajawazito 100.
Mwisho
Comments
Post a Comment