'Anasema mwaka huu ndio aliopangiwa na Mungu kuingia jimboni kugombea, ...awaomba wananchi kumchagua' IMEANDIKWA NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ "Alienipita kwa kura moja 2020, nimempita kwa kura 62 kwenye kura za maoni mwaka huu 2025, hivyo nimeshinda kwa kishindo," Maneno hayo ya furaha yalimtoka mgombea uwakilishi Jimbo la Tumbe kupitia chama cha Mapinduzi CCM Salma Khamis Tumu wakati akizungumza na mwandishi wa makala hii huko kijiji kwao. Salma mwenye umri wa miaka 53 mkaazi wa shehia ya Tumbe Magharibi anasema, ameamini kwamba riziki ya mtu haiendi kwa mwengine bali siku ikifika, itamfika tu mwenyewe. Pamoja na kushindwa kwenye kura za maoni kwenye uchaguzi uliopita wa mwaka 2020, lakini hakukata tamaa bali ajijipanga kugombea tena 2025, ambapo alipitishwa kwa kura 134 huku mpinzani wake ambae ni mwanamme akijipatia kura 72. Mgombea huyo anasema, hizo ni baraka za Mungu kumjaalia kupita kwenye nafasi hiy...
NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ ILE dhamira ya Dk. Hussein Ali Mwinyi kuifungua Pemba kiuchumi kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa, sasa imefana. Kwani uzinduzi wa ujenzi wa uwanja huo na barabara ya Chake Chake- Mkoani, umezinduliwa rasmi Septemba25, mwaka huu, katika uwanja wa ndege uliopo Furaha Pemba. Ni furaha kubwa kwa wananchi wa kisiwa cha Pemba, kuona kwamba kitu ambacho wamekisubiri kwa muda mrefu, sasa kinakwenda kufungua uchumi wao. Maana serikali ya awamu ya nane, imedhamiria kufanya mageuzi ya makubwa katika sekta ya usafiri wa anga Zanzibar, kwa lengo la kuimarisha miundombinu ya utoaji wa huduma katika uwanja wa ndege wa Pemba. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla amezindua ujenzi huo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, jemedari wa uchumi. Makamu huyo anasema, ujenzi wa miradi hiyo ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025 ambapo malengo ya se...