Skip to main content

Posts

''TUNATAKA KUONA WANAWAKE WANAJITEGEMEA' WAZIRI PEMBE

  Salha ZJMMC@@@@ Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mh e . Riziki Pembe Juma amesema S erikali imeamua kuwawezesha wanawake jasiri ili kuwawezesha kiuchumi na kuweza kujitegemea weneyewe ili kuondokana na hali ya utegemezi katika jamii. Ame yasema hayo wakati akifungua mafunzo ya wanawake shupavu wa amali ya Zanzibar yaliyofanyika B weni katika Chuo cha Ufundi Karume Wilaya ya Magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi , Unguja. Amesema kutoa mafunzo kwa wanawake wenye ujasiri kunaongeza uwezo zaidi wa kuweza kuzalisha bidhaa zao zenye ubora. Pia ametoa wito kwa wataalamu jasiri wanaopatiwa mafunzo ya kuwa walimu kwa wanawake wengine ambao hawajapata fursa ili kuwawezesha wanawake wengi kuweza kujiajiri na kuondokana na utegemezi katika familia zao. Hata hivyo ametoa wito kwa wanawake kuwapenda, kuwaongoza, na kuwalinda watoto wote ili kuwasaidia kuepukana na vitengo vya   ukatili wa kijinsia na udhalilishaji . Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Ra...

TAMWA YALIPONGEZA JESHI LA POLISI KUKEMEA UVUNJIFU WA MAADILI ZAZNAIBAR

  Chama cha waandishi wahabari wanawake Tanzania Zanzibar TAMWA,ZNZ kinalipongeza jeshi la Polisi kwa kuchukuwa hatua za haraka kushughulikia suala la uvunjaji wa maadili lililofanywa hivi karibuni na kusambaa katika mitandao ya kijamii. Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Mkurugenzi wa chama cha waandishi wahabari wanawake Tanzania Zanzibar, TAMWA ZNZ Dk Mzuri Issa amesema kutokana na tukio lilotokea hivi karibuni na kutoa taswira mbaya ya kimaadili, kinidhamu na Udhalilishaji nchini, hivyo TAMWA imeliomba Jeshi la Polisi kuwakamata wote waliohusika na Sheria kuchukuwa mkondo wake. Amesema TAMWA ZNZ inaomba hatua kali zichukuliwe dhidi ya wahusika kwa mujibu wa sheria zilizopo ili kuwa funzo kwa wengine wanaotaka kujaribu na hivyo kulinda mila, silka na maadili ambazo ni moja kati ya tunu muhimu za Zanzibar. “Ni dhahiri kwamba vitendo hivyo kamwe havikubaliki na vinaweza kuleta athari na madhara makubwa ya hivi sasa na baadae katika kuimarisha yetu na   vizazi vya le...

PEMBA SASA KUEKEZA NI DOLA MILIONI 10 KUTOKA 100 ZA AWALI

                                     NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ SERIKALI ya awamu ya nane inayoongozwa na Dk. Hussein Ali Mwinyi imedhamiria kwa vitendo kukiinua kisiwa cha Pemba kiuchumi. Hii imekuja, baada ya kuonekana kisiwa cha Pemba kwa miaka mingi, kimeachwa nyuma, katika masuala ya ukuaji wa uchumi. Lakini Dk. Mwinyi, hakuwa nyuma katika kuhakikisha wananchi wa Pemba wanapata maendeleo kama wenzao wa Unguja, na ndio maana akatenga maeneo maalum, kwa ajili ya uwekezaji mkakati. Na miongoni mwa mambo, ambayo ameyafanya ili kuvutia wawekezaji ni kuimarisha miundombinu mbali mbali, pamoja na kuweka punguzo la bei kwa mwekezaji atakaeekeza. Kuna mpango wa kujengwa uwanja wa ndege wa kimataifa, bandari ya kisasa pamoja na kuimarisha miundombinu ya barabara, umeme na maji katika maeneo yaliyotengwa kwa uwekezaji, ili uwekezaji uwe wa kiwango kizuri. Kutokana na punguzo la bei lililo...

HIZI HAPA CHANAGAMOTO ZINAZOWAKWAZA WANAWAKE KUTOKUWA VIONGOZI MAJIMBONI

  NA AMRAT KOMBO, ZANZIBAR Hali ya wanawake, ikiwa pamoja na kushika nafasi za uongozi zinatafuatiana duniani kutokana na sababu nyingi. Miongoni mwa hizi sababu ni sera za nchi hizo, sheria, mila, tamaduni na dhana potofu ya kumchukilia mwanamke kama mtu ambaye haki zake kama binaadamu hazistahili kuwa sawa na zile za mwanamume. Matokeo yake ni kuona wanawake wengi wanakosa haki zao nyingi, ikiwa pamoja na za elimu, urithi , kushika nafasi za uongozi na kuwa na sauti inayosikika na kuheshimika katka kufanya maamuzi. Ripoti ya mwaka 2018 inayohusu uwiano wa kijinsia ulimwenguni imeweka picha halisi ya haki za wanawake katika siasa, uchumi na elimu ili kuutanabahisha ulimwengu kasoro ziliopo na kuelezea umuhimu wa kufanyika marekebisho. Hivi sasa ziaonekana zinafanyika jitihada mbalimbali kurekebisha dosari hizi ili kuhakikisha mwanamke, anakuwa ni sehemu ya uongozi, ikiwemo kwenye mambo ya kisiasa kwa vile huko ndiko anapofanyika maamuzi muhimu ya kimaisha, kisiasa na k...

SMZ yakumbushwa kuzifanyia marekebisho Sheria zinazominya uhuru wa habari Zanzibar

NA NAFDA HINDI, ZANZIBAR Mkurugenzi wa Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania Znz Dk Mzuri Issa amesema kuwepo kwa uhuru wa habari na kujieleza ni haki ya msingi ya binadamu ambayo itachochea kuleta maendeleo. Dk Mzuri ameyasema hayo wakati akifunguwa mkutano wa uchambuzi wa sheria zinazokwaza uhuru wa habari Zanzibar uliowashirikisha wadau wa masuala ya habari na waandishi wahabari uliofanyika katika Ofisi za Tamwa Tunguu, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja. Amesema suala la kupata habari kwa Zanzibar limeanzia tokea enzi za karne zilizopita, kinachorudisha nyuma kwa sasa kutopata habari ni kuwepo sheria zisizo rafiki kwa waandishi wahabari na hata wananchi. “Zanzibar ni kitovu cha Utamaduni wakupata habari, na hata waandishi wahabari wanawake walianzia Zanzibar enzi hizo,’’ Dk Mzuri Issa. Akiwasilisha ripoti hiyo ya Uchambuzi wa sheria zinazokwaza uhuru wa habari Muhadhir kutoka Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU) Said Suleiman amesema kuna baadhi ya sheria zimepitwa n...

SHUNGI: 'WATAKA KUJENGEWA BARABARA YAO KWA KIWANGO CHA LAMI'

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI wa shehia ya Shungi wilaya ya Chake chake Pemba, wameikumbusha serikali, kuwajengea barabara yao ya Chanjamjawiri- Tundaua kwa kiwango cha lami, ili wapate kuitumia kwa utulivu. Walisema, kwa sasa imesambaa mashimo na msingi yenye kina kirefu, jambo ambalo haliwapi utulivu, wakati wanapokwenda kwenye shughuli zao za kimaisha. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi shehiani hapo, walisema barabara hiyo ambayo awali ilikuwa na lami, kwa sasa zaidi ya miaka minne imekuwa ikihataraisha waenda kwa miguu, achia mbali wanaotumia vyombo vya moto. Mmoja kati ya wananchi hao Moza Suleiman Mohamed wa Misooni alisema, hasa wao akinamama wamekuwa wakipata usumbufu mara pale wanapokuwa wajawazito. ‘’Hutokezea sisi kutakiwa kuripoti hospitali ya Chake chake kwa huduma na uchunguuzi zaidi, lakini tunapoitumia barabara kutokana na mashimo yaliomo, hupata mtikisiko,’’alieleza. Nae Asma Said Abdalla wa Chanjamjawiri, alisema barabara hiyo ndio wanayo...

JAJI IBRAHIM ATUPILIA MBALI RUFAA KESI DAWA ZA KULEVYA

  NA MARYAM NASSOR, PEMBA @@@@        HUKUMU ya rufaa ya dawa za kulevya inayohusisha kete 1,678 iliyowasilishwa mahakama kuu Zanzibar, kanda ya Pemba, imekataliwa na Jaji wa mahakama hiyo, Ibrahim Mzee Ibrahim, baada ya kubaini kuwa, upande wa mashtaka tokea awali, ulithibitisha kosa pasi na shaka yoyote. Jaji Ibrahim akitoa uamuzi wa rufaa hiyo na baada ya kujiridhisha, aliamuru mshtakiwa huyo Zubeir Jerad Said wa Bopwe Pemba, kutumikia chuoa cha mafunzo, kwa muda wa miaka 10, kama alivyohukumiwa awali mahakama ya mkoa.   Alisema kuwa, mahakama yake imeitupilia mbali rufaa hiyo, kutokana na kuwa upande wa mashtaka, ulikuwa na mashahidi ambao walitoa ushahidi wa wazi na wakuaminika, hivyo hawezi kuipindua hukumu hiyo.   Jaji huyo alisema kuwa, mshtakiwa alikamatwa na na dawa hizo na kupewa jina la kielelezo ‘pw3 na pw4’, ambacho ni mfuko wa dawa za kulevya aina ya heroin kete uliokuwa na 1, 678   zenye uzito wa   gramu 41.53. ...

MADIWANI WANAWAKE WANAVYOSIMAMIA VYEMA UWONGOZI

  NA  AMRAT KOMBO, ZANZIBAR@@@@ SIKU zote baadhi ya watu wanaimani ya kuwa, mwanamke bado ni mama wa nyumbani pekee. Ambae anatakiwa kuchunga familia yake tu peke yake, lakini bila ya kufikiri kuwa mwanamke anaweza kufanya mambo makubwa ya kuwasaidia jamii na kuleta maendeleo katika nchi. Ushahidi wa hili, sasa usiangalia tena Marekani na kwengineko, njoo kwa Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania, alivokuwa jasiri na mchapa kazi, katika nafasi yake ya uwongozi. Hivyo inaonesha kuwa, mwanamke sio mdhaifu kama watu wanavoona, hebu tuangalie baadhi ya viongozi mwanamke wanavyowajibika katika nafasi zao. Fatma R as hid Juma ni diwani wa   Chukwani Unguja, anasema kabla ya kushika nafasi hiyo, alikuwa mfanya biashara   mjasiria mali mdogo, huku akiwa mwanancha wa chama cha mapinduzi CCM. Anasema katika mwaka 2020, alijishirikisha katika kugombea udiwani wakiwa na wagombea wenzake 11, wakiwa wanawake watatu na wanaume nane, na kubahatika kutokea mshindi kwen...

KATIB ABEIDA ATOA TAARIFA YA MTOTO ALIYEKUWA AKIPIGWA NA MAMA YAKE

  Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto bi Abeida Rashid Aballah amesema mtoto Farhia Omar Mohamed (10) ambaye aliyekuwa anapigwa na mamaake wa kambo huko Bububu, Unguja hali yake inaendelea vizuri. Ameyasema hayo jana wakati alipomtembea mtoto huyo katika nyumba ya kulea watoto Mazizini, Unguja.   Bi Abeida amesema mtoto Farhia atapatiwa haki zake zote za msingi kama sheria ya mtoto inavyoeleza . Amefahamisha kwamba sheria ya mtoto sheria Na 2 ya mwaka 2011 imeainisha haki za mtoto ikiwemo haki ya kupata elimu, matibabu, kuishi, nk.   Ameeleza ni wajibu wa Wizara ya Maelendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto kusimamia utekelezaji wa sheria hiyo kwa maslah ya taifa.   Aidha katibu Mkuu Abeida ametoa wito kwa wazazi na walezi kutumia busara zaidi wakati wa kumuadhibu mtoto endapo amefanya kosa, kwani ikumbukwe kwamba mtoto ni wa Serikali hivyo, Serikali haitovumilia kuona mtoto anafanyiwa vitendo vya udhalilishaji wa ain...

SHEHA SHUNGI: ‘CHIMBENI MASHIMO SALAMA KUHIFADHIA MAJI TAKA’

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ UONGOZI wa shehia ya Shungi wilaya ya Chake chake Pemba, umewataka wananchi, ambao bado hawajachimba mashimbo ya kuhifadhi maji taka, kufanya hivyo haraka, ili kuzuia uwezekano wa kukumbwa na magonjwa ya mripuko. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi shehiani hapo, Sheha wa shehia hiyo Hamad Ramadhan Soud, alisema shehia haitomvumilia mwananchi yeyote, anetiririshaji maja taka, kwani athari yake inaweza kuenea kwa shehia nzima. Alisema, kila mwananchi ahakikishe amechimba shimo maalum na kisha kulifunika vyema, ili kuhifadhi maji anayotumia kutoka nyumbani mwake, badala ya kuyaacha yasambae. Alieleza kuwa, maji yanayotumiwa hata kwa kukoshea vyombo au kukogea chooni, ndio chanzo cha magonjwa kama matumbo ya kuharisha damu, kipindu pindu na minyoo. Sheha huyo alieleza kuwa, amekuwa akitoa elimu hiyo kila muda kwa wananci wake, ili kuona wanajikinga na magonjwa mbali ambayo yanaweza kusababishwa na maji taka. ‘’Niwatake wananchi wangu, haraka s...