Skip to main content

Posts

WATU WENYE ULEMAVU WAKABIDHIWA VISAIDIZI

  Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Abeida Rashid Abdallah amesema Wizara hiyo itaendelea kusimamia maendeleo ya jamii ikiwemo kundi la watu wenye ulemavu ili kuona wanaishi katika mazingira mazuri na salama. Akizungumza kwa niaba ya katibu mkuu huyo Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji na Utumishi Dkt. Salum Khamis Rashid wakati akikabidhi visaidizi vya watu wenye Ulemavu kwa Taasisi ya Maisha Bora Fondation, katika ukumbi wa Wazee Sebleni. Dkt Salum alivitaja visaidizi hiyo ikiwemo na lotion 72 kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi ALBINO, fimbo nyeupe 20 kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa uoni, pamoja na viti vya magurudumu mawili 30 (Wheel chair) kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa viungo Alisema Wizara itaendelea kutatua changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi kadiri hali itakavyoruhusu ili kuhakikisha hakuna kundi ambalo limeachwa nyuma. Alieza kwamba moja kati ya jukumbu la Wizara hiyo ni kujenga ustawi mzuri kwa jamii hivyo Wizara hiyo itaen...

MIAKA MITATU YA DK. MWINYI PEMBA WAJENGEWA KIWANDA CHA USARIFU MWANI

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ NOVEMBA 3 ya miaka mitatu iliyopita, ilikuwa ndio siku ya kwanza ya Rais mpendwa wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi, kuwasili ndani ya Ikuklu ya Zanzibar. Kwa wakati huo, hakuwasili akitokea nchi jirani..laaahasha alitokea kwenye viwanja alivyokula kiapo, kushika hatamu ya uongozi. Maana Dk. Mwinyi, baada ya kumalizika kwa kampeni za zaina yake, zilizotajwa kama za kisayansi kwa kule kukutana na makundi mbali mbali, kisha wananchi walimpigia kura. Baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa vyama vingi, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC, ilimtangaaza Dk. Mwinyi kuwa rais wa Zanzibar kwa kupata asilimia 76.27 na kuwaacha mbali wagombea wenzake. ‘’Nimepokea ushindi kwa mikono miwili na nawashukuru wananchi wa Zanzibar kwa kunichagua mimi na chama changu, kwa miaka mitano ijayo,’’alisema wakati huo. Kwa wananchi Zanzibar, kama alivyosema Mwenyekiti wa CCM mkoa wa kaskazini Pemba Mberwa Hamad Mberwa, kuwa duniani viongozi kama aina ya Dk. Mwinyi...

MBUNGE ASIYA AWAKUMBUSHA JAMBO WAZAZI WA QAMARIA WETE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MBUNGE wa Viti maalum mkoa wa kaskazini Pemba Alhajjat Asiya Sharif Omar, amewakumbusha wazazi na walezi, wenye watoto wao Almadrassatul-Qamariyya ya Wete, kulipa ada za watoto wao kwa wakati, ili kuwapa uhakika waalim kufundisha kwa ufanisi. Alisema, maendeleo yaliopo katika madarassa hiyo, hayakuja bure, hivyo ili yawe endelevu, hakuna budi kwa wazazi na walezi kujikumbusha namna ya ulipa ada. Mbunge huyo aliyasema hayo, ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi Wete, kwenye mahafali yalioambatana na siku ya wazazi kwa madrassa hiyo. Alisema, maendeleo endelevu katika madrassa hiyo, hayatokuja kwa haraka na kudumu, ikiwa wazazi watapuuzia suala la ulipa ada kwa watoto wao. Alieleza kuwa, madarassa hiyo haina mfadhili wala ruzuku kutoka serikalini, hivyo na inategemea moja kwa moja ada kutoka kwa wazazi na walezi, wenye watoto wao katika madrassa hiyo. “Nichukuwe nafasi hii, kuwasisitiza wazazi na walezi kuhakikisha wanalipa ada zao kwa waka...

SHAHIDI DAKTARI: ''NILIGUNDUA MAREHEMU ALISHAMBULIWA KWA MARUNGU''

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ SHAHIDI nambari 14 kwenye kesi ya mauwaji, ambae ni Daktari wa hospitali ya Vitongoji Chake chake Pemba Ali Juma Ali, amedai mahakamani kuwa, baada ya uchunguzi alibaini kuwa, mjeruhiwa alishambuliwa kwa vitu vyenye cha kali na silaha mfano wa marungu. Alidai kuwa, wakati akiwa kazini kwake hospitalini hapo, Septemba 21, mwaka 2021, alimpokea mjeruhumiwa Suleiman Said Saleh (55) akiwa katika hali mbaya. Shahidi huyo akiongozwa na Wakili wa serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Ali Amour Makame, mbele ya Jaji wa mahakama kuu Zanzibar Ibrahim Mzee Ibrahimu, alidai kuwa uchunguuzi ukabini kuwa kina cha jeraha la kichwani ni nchi nne kwa upana na urefu nchi mbili. Alidai kuwa, jeraha jingine ambalo lilikuwa bega la mkono wa kushoto, lilikuwa na nchi tatu kwa urefu na kina cha kwenda chini likuwa nchi mbili. Akiendelea kuongozwa na Wakili wake, shahidi huyo alidai kuwa, wakati anamfanyia uchunguuzi, alibaini pia mkoja wake wakati ukitoka...

WAZEE WATAKA UZEE UTAMBULIWE KWA MIAKA 60 NA SI0 70

  Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Abeida  Rashid Abdallah amesema Wizara hiyo imepokea maoni yaliyotolewa na Wazee kuhusu kuifanyia marekebisho sheria ya Masuala ya Wazee, sheria namba mbili (2) ya mwaka 2020 katika kifungu kinachozungumzia umri wa mzee. Akizungumza baada ya kikao cha pamoja baina ya watendaji wa wizara hiyo ,Kamati ya Kanuni na Sheria ndogo ndogo ya Baraza la Wawakilishi, wazee kutoka Jumuiya ya wazee (JUWAZA) pamoja na wazee wanaoishi katika makao ya wazee, kilichofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa Makao ya Wazee Sebleni, Unguja. Alisema wazee wametaka kifungu cha sheria hiyo kifanyiwe marekebisho umri wa mzee uwe miaka 60 badala ya miaka 70. Hivyo watendaji wa wizara hiyo watakaa chini na kutafakari. “Kamati imekuja kututembelea katika makao ya wazee, pamoja kupata maoni ya kanuni, ya masuala ya wazee iliyotungwa hivi karibuni lakini majadala mkubwa umejitokeza, baada ya kanuni hiyo kuonesha umri wa mzee n...

UKUSANYAJI MAONI SERA YA MSAADA WA KISHERIA WATUA PEMBA

NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@

WEMA ZANZIBAR YAPEWA RAI KUIMARISHA LISHE SKULINI

  ZANZIBAR Wizara ya Elimu imeombwa kuhamasisha na kutoa elimu ya kilimo cha mboga mboga mashuleni kwa lengo la kuboresha lishe bora kwa wanafunzi. Wakizungumza katika kaikao cha pamoja huko hoteli ya SEA CLIFF Mangapwani   kilichowashirikisha watendaji Sitini na tano kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kilichajadili mafanikio na changamoto zinazoikabili sekta ya kilimo hasa cha mboga mboga, VIUNGO na matunda na kutafuta ufumbuzi ili kuleta tija kwa jamii. Wamesema Wizara ya Elimu ya Zanzibar na Tanzania Bara washirikiane kwa pamoja kuongeza nguvu kutoa elimu kwa wanafunzi wa kulima kilimo cha bustani mashuleni kwa lengo la kuimarisha Afya zao kwa kupata lishe bora na kwa ajili ya   maisha yao ya baadae. Mapema Mratibu wa mradi wa Agriconnect Zanzibar Omar Abuubakar Muhammed amesema ipo haja kwa jamii kuhamasishwa juu ya ulaji wa lishe bora hususan kina baba ambao wanaongooza kupeleka majumbani kwao vyakula visiv...

UWT TAIFA, WAMPA KONGOLE MBUNGE ASYA SHARIF PEMBA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania ‘UWT’ taifa Mery Pius Chatanda, amesema aina ya Mbunge wa viti maalum mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, katika kuwakomboa wanawake kiuchumi, ndio mfano unaofaa kuigwa, na wabunge wengine Tanzania. Alisema, Mbunge huyo ameendelea kutekeleza kwa vitendo maagizo ya UWT taifa, ya kuwakomboa wanawake kiuchumi, kufuatia kukabidhi mashine ya kuzalisha mikate na tosi na fedha taslim, kwa wanawake wa mkoa wake, yenye thamani ya shilingi million 10.5 Mwenyekiti huyo wa UWT taifa, aliyasema hayo leo Oktoba 25, 2023, Micheweni mara baada ya kukabidhi mashine hiyo, kuweke jiwe la msingi ofisi ya ushoni wa nguo na kukabidhi shilingi milioni 1, zilizotolewa na Mbunge huyo. Alieleza kuwa, anaamini kupitia uwekezaji wa Mbunge huyo, wanawake wa CCM mkoa wa kaskazini Pemba, watapiga hatua kubwa ya kimaendeleo, kupitia njia ya kujiinua kiuchumi. Alifahamisha kuwa, wakati umefika kwa wabunge wengine wa mikoa ya Ta...

MRADI WA VIUNGO WALETA MAPINDUZI YA KIUCHUMI ZANZIBAR

  Na Nafda Hindi, Zanzibar @@@@ Uwepo wa mradi wa VIUNGO, mbogamboga na matunda   Zanzibar umesaidia wananchi   kujikita katika sekta ya   kilimo hali iliyoleta mapinduzi ya kiuchumi katika familia zao. Hayo yamebainishwa na wanufaika wa mradi huo mara baada ya kutembelewa na Kikosi Kazi cha ufundi kwa Taasisi zinazotekeleza mradi huo kwa   lengo la kugunduwa Mafanikio   pamoja na changamoto zinazowakabili wakulima na kuzitafutia ufumbuzi. Wamesena kuna mafanikio waliyoyapata kupitia kilimo ikiwemo kuimarisha Afya za familia kwa lishe bora kwa kula mboga mboga na kuongeza kipato kupitia mfumo wa biashara. Ali Shauri ni katibu wa uhirika wa kilimo hai kiitwacho TUMAINI LA KIJANI uliopo Chuini Zanzibar, amesema wao wanatengeneza bustani za nyumbani ambazo zinajumuisha mbogamgoga pamoja na mimea ya dawa lengo likiwa kukibadilisha kijiji kuwa   cha kijani na wananchi kurudi katika uasili wa kutumia dawa za mitishamba jambo linalotoweka kwa vizazi v...

KASORO ZA KISHERIA ZAWAWEKA NJIA PANDA WATU WENYE ULEMAVU KUPATA HAKI ZAO

  HABIBA ZARALI, PEMBA@@@@ KATIBA ya Zanzibar ya 1984 kifungu 11 (1) imeeleza kuwa binadamu wote ni huru, na wote ni sawa na kila mtu anastahiki heshima ya kutambuliwa   na kuthaminiwa utu wake. Ikafafanuliwa tena kifungu cha 12 (1) kuwa watu wote ni sawa mbele ya sheria   na wanayo haki   bila ya ubaguzi   wowote , kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria. Katiba ya Jamuhuri ya Muungano ibara ya 12 (1) nayo imeelezea kuwa binadamu wote huzaliwa huru na wote ni sawa, na kila mtu anastahiki heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake. Tena kwenye Ibara ya 13 (4) ikaweka marufuku kwa mtu yoyote kutobaguliwa na mtu au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji   wa kazi au shughuli yoyote ya nchi. Kimataifa upo Mkataba wa haki za watu wenye ulemavu   katika ibara ya 5, imeeleza kutokuwepo ubaguzi, na kwamba watu wote ni sawa mbele ya sheria.   Mkataba huo pia unapinga aina zote za ubag...