Skip to main content

Posts

WANAODAIWA KUUA KWA MAKSUDI WAWI, KUUKARIBISHA MWAKA MPYA WAKIWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WATUHUMIWA wa kesi ya kuua kwa makusdi, inayowakabili vijana wanne akiwemo Ali Mussa Omar ‘Mkapa’ na wenzake, wote wakaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake, wamerejeshwa tena rumande, baada ya Jaji anayesikiliza kesi yao kutokuwepo mahkamani. Watuhumiwa wingine waliorejeshwa rumande hadi Januari 23, 2024 ni Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 na Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, ambao wanatuhumiwa kumuua kwa maksudi kijana Said Seif Kombo. Mara baada ya kuwasili mahakamani hapo wakitokea rumande, walitulia tuli wakisubiri taratibu za mahakama kuu ziendelee, ingawa Mwanasheria wa serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Awamu Zubeir Awamu, alidai kuwa Jaji husika hayupo mahakamani hapo. Wakili huyo wa serikali, alimueleza hakimu wa mahkama ya mkoa Chake chake anayeshughulikia makosa ya udhalilishaji Ziredi Abdull-kadir Msanifu, juu ya dharura ya Jaji husika wa kesi hiyo. ‘’Mheshimiwa Hakimu, ilikuwa kesi hii...

WANAWAKE WAWAONESHA WENZAO NJIA KUINGIA KWENYE SIASA, CHANGAMOTO ZIGEUZENI FURSA SAFARI IENDELEE

    NA AMRAT KOMBO, ZANZIBAR@@@@ UONGOZI ni haki ya kila mtu, awe mwanaume au mwanamke. Tena hapa tunajifunza kuwa, hata kundi la watoto wa kike ama wakiume, wanaweza kuwa viongozi kwa aina yao na sehemu waliyo ndani ya jamii yao. Jamii imeshazowea kuona mwanaume ndio anaeweza kuwa kiongozi na kusimamia nchi katika hali zote, kuliko wanawake na hii kutokana na mitazamo yao isijengwa kimamtiki. Ingawa mtazamo huu, unaweza ukaondoka kwasababu mwanamke ameweza kuongoza familia na kuweza   kusimama imara,   kwahivyo hatoshindwa kuisimamia nchi nzima. Mfano hai na wa kweli kwa sasa ndani ya taifa la Tanzania, rais anayewaongoza wananchi wastani wa milioni 60 ni Dk. Samia Suluhu Hassan (mwanamke), na kila mmoja ni shahidi hajatetereka kwenye nafasi hiyo. Tena anasimamia vyema familia yake, pamoja na wananchi wake na kutatua changamoto mbalimbali zinazotokea katika nchi na mengi yameongelewa kuhusu yeye bali hakukata tamaa. KWA NINI WANAWAKE HAWAONEKANA KW...

Vikausha damu vya mjamzito hivi hapa, umo mchele, udongo, mkaa, chaki Uwezekano wa kuzaliwa watoto wenye udumavu, utapiamlo ni mkubwa

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ ‘’KILA ninapobeba mimba nimezoea kula mchele kwa wingi naweza kusamehe pilau au biriani,’’ ndio maneno ya mwanzao ya Bahati Mohamed Ali (sio jina lake halisi). Nilimfuma akiwa barazani kwake, mjini Ole wilaya ya Chake chake, pembeni yake akiwa na kibakuli cha mwazi, kwa umbali utaona amejaza chakula aina ya pepe, kumbe ni mchele wa Mbeya. Hujichotea kidogo kidogo na kuushindilia mdomoni mwake, huku akiendela kupiga storia na wenzake, bila ya kujali kuwa ujauzito alionayo na mchele huo hauna mwisho mwema. Kawaida yake akiwa mjamzito, kila anapoamka asubuhi anaroweka mchele upatao robo kilo hivi…na baada ya kumaliza kupika, yeye huchukua mchele wake kutafuna (kula). Wakati mwenza wake na watoto wao, wanakula chakula cha mchana, Bahati yeye hukaa pembeni na kibakuli chake cha mchele akiendelea kubahatisha afya yake. ‘’Mimba nyengine hupenda sana kutafuna mchele wa Mbea na nyengine hupenda mchele wa mapembe, kwa kweli huwa nina hamu (kileo), kwan...

WANAKONGAMANO: ‘’TUITUMIENI TUME YA KUREKEBISHA SHERIA KUTOA MAONI KWA SHERIA MUITAKAYO’

NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI kisiwani Pemba, wameshauriwa kuitumia Tume ya Kurekebisha sheria wanapokuwa na vikao vyao vya kupokea maoni, ya kutaka kurekebishwa sheria, ili kuwa na sheria zinazoendana na dunia ya sasa. Ushauri huo umetolewa na wanakongamano la siku moja, la kuelekea siku 16 za kupinga ukatili na udhalilishaji, lililoandaliwa na Jumuiya ya wasaidizi wa sheria, wilaya ya Chake chake Pemba ‘CHAPO’, na kufanyika ukumbi wa Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA-Zanzibar ofisi ya Pemba. Walisema, ni vyema wananchi wanapokutana na Tume hiyo, kuacha jazba na kuzitolea maoni sheria, ambazo zimeshapitwa na wakati, ili kueleza wanavyotaka ziwe, kwa mujibu wa mazingira ya sasa. Mjumbe wa Jumuiya ya TUJIPE Pemba, Sheikh Abdalla Nassor Maulid, alisema utoaji wa maoni katika tume hiyo, ni njia muhimu kwa jamii kuwa na sheria rafiki. ‘’Tume ya kurekebisha, hupita katika maeneo yetu, sasa sisi wananchi tuitumieni ili kutoa maoni, juu ya sheria ambayo tuna...

ZAWADI AMOUR NASSOR, MWAKILISHI KONDE ALIYEPITIA MENGI KABLA YA KUINASA NAFASI HIYO

  NA AMRAT KOMBO, ZANZIBAR@@@@ KILA mwanadamu huwa na malengo katika maisha na huhitajika mipango na ujasiri kuweza kuitekeleza. Ujasiri ni silaha nzito kuibeba, lakini ina faida kama utakuwa na sulubu ya kuibeba. Neno ujasiri limebeba maana kubwa kwenye tafsiri ya mtu aliefanikiwa katika maisha yake. Mmoja wa wanawake aliyeweza kupata mafanikio kutokana na kuwa na ujasiri ni Zawadi Amour Nassor . Mwana mama huyu, ambaye ni mtoto wa kwanza katika watoto tisa wa familia yao,amezaliwa   1978 katika kijiji cha Konde Pemba na kupata elimu yake ya msingi katika Skuli ya Kinyasini, Unguja, mwaka 1991. Aliendelea na elimu ya sekondari katika Skuli ya Konde mwaka 1994 na kupata elimu ya juu katika chuo cha Zanzibar Muslim College, Mazizini hadi ngazi ya stashahada na shahada. Vile vile amesomea uwalimu katika Chuo Kikuu Huria Tanzania ‘OUT’. Alisomesha katika skuli ya msingi za Pangale na Konde"A" kuanzia mwaka 2000 hadi 2020. Jasiri huyu alianza kuwa mwalimu wa s...

LFS, YAWAONESHA NJIA MAAFISA MAWASILIANO WA JUMUIYA ZA WASAIDIZI WA SHERIA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAAFISA mawasiliano na habari wa Jumuia za wasaidizi wa sheria Tanzania zimetakiwa kujenga ushirikiano wa karibu na watendaji wenzao, ili kuhakikisha wanakuwa na mifumo sahihi ya utoaji wa taarifa za jumuia. Hayo yameelezwa na Mtaalamu wa masoko kutoka LSF Gilsant Mlaseko, wakati akizungumza na maafisa   hao kwenye mkutano wa kujengewa uwezo kwa njia ya kielektroniki. Alisema bidhaa ya mwasiliano sio haki ya Afisa Mawasiliano na Habari pekee kwenye jumuiya, bali anatakiwa kuwa karibu na wakurugenzi, waratibu na watendaji wengine. Alieleza kuwa, wakati mwingine ndani ya Jumuiya Afisa huyo anaweza kuwa mwisho katika utoaji wa taarifa na hasa baada ya kuidhinishwa na kuthibitishwa na kamati iliyoteuliwa. ‘’Suala la mawasiliano hasa ya kutoka nje ya Jumuiya, linapaswa watoa taarifa wawe makini na sio jukumu la mtendaji mmoja, bali iwe ni timu ya Jumuiya na kisha muhusika anateuliwa,’’alieleza. Akieleza umuhimu wa mawasiliano Mtaalamu huyo, a...

MJASIRIAMALI WA MBAO PEMBA AKERWA KUCHELEWESHEWA KIBALI UKATAJI MITI

  NA KHADIJA OMAR, PEMBA@@@@ MJASIRIAMALI wa uchongaji na utengenezaji wa bidhaa za miti, Mohamed Hamza Khamis wa Kuyuni shehia ya Ngwachani wilaya ya Mkoani, ameziomba mamla husika kutoa ruhusa ya haraka ya ukataji miti, mara wanapokamilisha taratibu.   Alisema, inawezekana kufuata taratibu zote kuanzia kwa sheha hadi Idara ya misitu, kwa ajili ya kukata miti ya mbao ingawa changamoto ni ucheleweshaji wa utaji wa kibali husika.   Hayo yamelezwa na mjasiriamali huyo, wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizim kijijini hapo, juu ya changamoto anazopitia katika kazia yake.   Alisema, jambo hilo la kucheleweshwa kupewa kibali, humuwawia vigumu na kusababisha migogoro isiyokuwa ya lazima na wateja wake, kwani wanakuwa hawamuelewi.   Alieleza kuwa, kufanya hivyo wakati mwingine kunasababisha kumkimbizia wateja kwani, wengi wao hupenda kazi zao zifanywe kwa haraka mno.   ''Changamoto yangu kubwa ni kucheleweshwa kupewa ki...

MIUNDOMBINU USHAHIDI WA KIELEKTRONIKI KAA LA MOTO MAHAKAMANI

  Na Mwandishi Wetu SHERIA ya ushahidi ya Zanzibar ya mwaka 2016 iliyoanza kutumika Januari 18, 2017, imeanzisha utaratibu maalum wa kisheria wa kupokea ushahidi wa kielektroniki. Sheria inatoa uhakika katika kupokea na kukubali ushahidi wa kielektroniki. Kifungu cha 71 hadi 73 vya sheria vinaeleza jinsi ushahidi wa kielektroniki unavyoweza kukusanywa na kushughulikiwa. Uwepo wa sheria hii ni dhahiri kwamba ushahidi wa kielektroniki unaweza kutumika wakati wa uchunguzi wa kesi za udhalilishaji wa kijinsia. Hata hivyo, utekelezaji unafanywa kwa kiwango kisichoridhisha sana, hali inayosababisha waathirika kutopata haki kwa wakati. Aidha, wakati sheria inaruhusu wapelelezi kukusanya ushahidi wa kielektroniki, polisi bado hawana ujuzi wa kutosha wa jinsi ya kukusanya ushahidi wa kielektroniki. Ofisa wa makosa ya mtandao kutoka Jeshi la Polisi Zanzibar, Issa Mohamed Salum, "Hatujapewa mafunzo ya kukusanya ushahidi wa kielektroniki. Bado tunaandika maelezo ya waathiriwa kwenye karatasi....

WAZAZI WENYE WATOTO THAMARAT NISSAI WAKUMBUSHWA JAMBO

  NA ASHA ABDALLA, PEMBA@@@@ UONGOZI wa skuli ya kiislamu Thamaratu-nnisai iliyopo Machomane wilaya ya Chake chake Pemba, imewakumbusha wazazi na walezi, kulipa ada zao kwa wakati, ili kurahisisha ufanisi wa usomeshaji skulini hapo. Akizungumza na wazazi na walezi wenye wanafunzi skulini hapo, Mwalimu Mkuu wa skuli hiyo Bimkubwa Habibu, alisema wapo baadhi ya wazazi, bado wamenakuwa wazito kulipa ada za watoto wao.   Alieleza kuwa, hilo linachangia uzoroteshaji wa skuli hiyo, ikiwemo usomeshaji na hata malipo ya mishahara ya waalimu walipo skulini hapo, ambao wanazitegemeza ada hizo.   ‘’Nyinyi wazazi na walezi, ambao mmewaleta watoto wenu skulini hapa, jambo la kwanza mhakikishe suala la ada halichelewi, maana ndio tegemezi kuu, kwa maendeleo yote ya skuli hii,’’alieleza.   Aidha Mwalimu Mkuu huyo amewakumbusha wazazi na walezi hao kuwa, wakumbuke kuwa, skuli hiyo hina mfadhili, anaeiendesha bali inategemea mno ada watakazozilipa kwa ajili ya watot...